TANZIA Msanii Sajuki afariki dunia

TANZIA Msanii Sajuki afariki dunia

Poleni sana wafiwa,but Elizabeth what do you mean by this?kuna mwingine tena alikukufa baada yakufanya interview Mikasi jamani nieleweshe mwaya.....

Wabongo mnapenda sana tantalila....jibu ni Kanumba.
Poleni wafiwa na wote mlioguswa na msiba, duniani hapa sio kwetu...kwetu ni mbinguni.
 
i feel sor for his wife! R.I.P sajuki tulikupenda ila Mungu amekupenda zaidi!
 
Pole zao wafia, Mungu ampe pumziko la milele .Amen.
 
R.I.P Sajuki. pole sana kwa familia yake.
 
Wabongo mnapenda sana tantalila....jibu ni Kanumba.
Poleni wafiwa na wote mlioguswa na msiba, duniani hapa sio kwetu...kwetu ni mbinguni.
Kwani wewe ni mnini ni mganda au.....?kwani kuliza ni kosa jamani?nihiyo Mbinguni wataiona tu watakaokufa wakiwa ni watenda mema tu......
 
R.I.P Sajuki, na pole sana mke wake Wastara, kweli yule mama ndiye aliyeonesha upendo wa mke wa kweli kwa mume. Alihangaika sana ila kwa mapenzi ya Mungu Mungu ameamua kumpumzisha muwewe. Maisha ni safari, kila mtu atasafiri kwa njia tofautitofauti.
 
tunakufa jamani khaa tunaisha jamani mweeeee
 
Pole sana wastara, nilikuwa nafatilia mazungumzo yao katika kipindi cha MKASI hapo juzi walikuwa very in the show, dah kifo bwana.
 
Nianzie hapo kwenye red,Sajuki alikwenda India kutibiwa,baada ya kurudi akaonekana kuchangamka kidogo(alirudi tofauti na jinsi alivyo ondoka).Lakini kwa upande mwingine nawalaumu wale wote walio enda kumtembeza mikoani,ili waweze kupata pesa,ukizingatia alikuwa bado mdhaifu sana,sio mtu wakumzungusha hapa na kule,ilitakiwa apumzike kwa muda mrefu sana,ndipo aendelee na shughuli nyingine,sasa ,mara utasikia yupo arusha,mara mwanza,kwa hali yake haya mambo ya kupanda majukwaani yalikuwa bado,ili bidi ajitazamie kwanza,Lakini ndio hivyo kuna wajanja wachache ambao wanapenda kutumia mianya ya ugonjwa wa mtu ilikuweza kujunifuisha,na kiasi kidogo kumpatia muhusika(mgonjwa),hii kitu inakuja kwa kasi sana bongo,watapigana vikumbo sasa hivi ili kila mmoja apate mwanya wa kuandaa mazishi,watatoa namba za simu na kadharika,hii yote ni mianya tu ya wachache.Mwisho sisi tulimpenda,lakini mungu amempenda zaidi,apumzike kwa amani.

Umeongea masuala ya msingi sana yanayokera jamii.
Uroho wa pesa wa wasanii wa bongo movies ndio ulisababisha kifo cha kulazimisha cha Sajuki, kwa kuzungushwa mikoani akiwa katika hali dhoofu. Kama ulivyoona kwenye kifo cha Kanumba, watachangishana ili 'wajidai' wanataka kumzika mwenzao, mwisho wanaishia kutokomea na pesa za rambirambi. Huu usanii inatakiwa ufike mwisho. Hata wakati wa ugonjwa wa Sajuki, michango mingi iliishia mikononi mwa wajanja wachache, mke wake aliambulia kidogo sana.
 
Who is Sajuki?

was this one:

Sadick Juma Kilowoko...SAJUKI AFARIKI DUNIA



Wasanii wa tasnia ya filamu na wapenzi wa filamu kwa ujumla wameanza mwaka kwa pigo jingine tena kwa kuamka asubuhi hii na taarifa za kusikitisha kuwa msanii ambaye amekuwa na matatizo ya afya kwa muda mrefu na katika kipindi cha siku za karibuni kuwa ICU Muhimbili, Sadick Juma Kilowoko aliyejulikana zaidi kama Sajuko amefariki dunia.
Mungu amlaze peponi pema Amin


13.gif



 
Back
Top Bottom