Nianzie hapo kwenye red,Sajuki alikwenda India kutibiwa,baada ya kurudi akaonekana kuchangamka kidogo(alirudi tofauti na jinsi alivyo ondoka).Lakini kwa upande mwingine nawalaumu wale wote walio enda kumtembeza mikoani,ili waweze kupata pesa,ukizingatia alikuwa bado mdhaifu sana,sio mtu wakumzungusha hapa na kule,ilitakiwa apumzike kwa muda mrefu sana,ndipo aendelee na shughuli nyingine,sasa ,mara utasikia yupo arusha,mara mwanza,kwa hali yake haya mambo ya kupanda majukwaani yalikuwa bado,ili bidi ajitazamie kwanza,Lakini ndio hivyo kuna wajanja wachache ambao wanapenda kutumia mianya ya ugonjwa wa mtu ilikuweza kujunifuisha,na kiasi kidogo kumpatia muhusika(mgonjwa),hii kitu inakuja kwa kasi sana bongo,watapigana vikumbo sasa hivi ili kila mmoja apate mwanya wa kuandaa mazishi,watatoa namba za simu na kadharika,hii yote ni mianya tu ya wachache.Mwisho sisi tulimpenda,lakini mungu amempenda zaidi,apumzike kwa amani.