Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,390
- 152,301
Wewe kama ni msanii mwenye mafanikio makubwa na uliepata utajiri au fedha nyingi kupitia fani yako, kamwe usijingize kwenye siasa wakati bado uko kwenye chati, bali fanya hivyo pale amapo umri unapokutupa mkono kutumikia fani yako, au pale kiwango chako kinapoanza kuporomoko kwa maana ya uwezo wako jukwaani n.k unapokuwa umeshuka.
Mjifunze kwa wanasoka maarufu duniani ambao baadhi yao wanapoona umri umeenda au viwango vyao vinaanza kushuka n.k, huamua kumaliza soka lao nchi za Uarabuni, Asia au Marekani na kamwe hawafanyi hivyo wakati bado wanatamba katika soka tena wao wakiwa na bahati ya kuendelea kulipwa vizuri huko wanakomalizia soka lao.
Kwenye fani, unaweza kuingia masikini ukatoka tajiri, ila kwenye siasa, unaweza kuingia tajiri na ukatoka umeyumba kiuchumi huku hata heshima au jina ulilolijenga katika jamii likiwal imeharibika vibaya hasa ukichagua upande mbovu katika siasa.
Aidha, ukiingia kwenye siasa ukiwa na jina kubwa na ukatumia umaarufu wako kupigania watu wa kawaida (sio kuwa upande wa watawala), basi una nafasi kubwa sana ya kukubalika zaidi katika jamii.
Sanaa inaakuunganisha na jamii, ila siasa inaweza kukutenga na kundi fulani katika jamii.