Msanii tajiri jiingize kwenye siasa pale uwezo wako unaposhuka kama ambavyo wanasoka maarufu huhamia ligi za Uarabuni au Asia kumalizia soka lao

Huwezi kuwa huko makini... Nani alikuweleza kuwa Joseph Mbilinyi na Joseph Haule walikuwa wameshuka viwango!? Mbilinyi alikuwa on fire vivyo hivyo na Haule. Ndiyo maana walipata wepesi wa kushinda majimbo yao, wale siyo viti maalumu ni wa kuchaguliwa. Upo au umeisha potea!?
..kwa maoni yangu, Sugu na Prof walikuwa wameanza kufifia ktk tasnia ya muziki. Hivyo basi ubunge uliwapatia shughuli ya kufanya baada ya kuwa wamefifia kimuziki.
 
Huwezi kumnusuru Zitto dhidi ya Diamond Plutnumz kwa thread ya kijinga kama hii.

Sent from my Infinix X627 using JamiiForums mobile app
Waweza kuwa sahihi kabisa. Lakini tuwe wakweli, kumtoa Zitto Kabwe bungeni ili wamuingize Diamond jee watu wa Kigoma watakuwa wanatumia akili au kuchenguka na viuno tuu? Zitto ambaye kuna majimbo yangejisikia fahari kuwa naye Leo Kigoma wanamuona hana hadhi ya kuhushimika Bali Diamond?
Nyerere aliwahi sema zuzu anaweza kumiliki kipande cha Vito vya almasi lakini ukamdanganya na kumpa kipande cha chupa akupe Vito na akachekelea.
Maana yake Wakigoma wamekuwa mazuzu kubalilishiwa na wanachekelea? Sidhani kama wako hivyo!
 
Hakuna tena strategists wa kueleweka kwenye huo upande ndiyo maana wanatuletea vikosi dhaifu mitandaoni eti vikosi hivi ndivyo vya kubadili upepo...wa maoni kuelekea kuunga mkono huo upande!

Wasubiri majibu ya wananchi baadaye mwaka huu.
Atakuwa alijisahau
 
Kuna watu wanafiki hadi wanakera. Mfano ni huyu Salary Slip. Kwake yeye Sugu na Prof. Jay kuwa wabunge wa Chadema ni sawa kabisa na haipukunguzi umaarufu wao wala pesa zao. Lakini kwa Diamond kuongea na Rais anakujakuja humu kuloloma! Sijui kwanini watu kama hawa "hawapotei"!!
Umemsoma vizur ukamuelewa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na hasa kama msanii mwenyewe hana mzuka wa siasa zaidi ya kuburuzwa kwa maslahi ya wengine
 
Sanaa inaakuunganisha na jamii, ila siasa inaweza kukutenga na kundi fulani katika jamii.
Hofu imekutawala
Kila raia mwenye umri wa kuanzia miaka 18,anaejua kusoma na kuandika,ana haki ya kugombea ubunge
Kamshauri sugu na professor Jay waache siasa basi
 
Waweza kuwa sahihi kabisa. Lakini tuwe wakweli, kumtoa Zitto Kabwe bungeni ili wamuingize Diamond jee watu wa Kigoma watakuwa wanatumia akili au kuchenguka na viuno tuu? Zitto ambaye kuna majimbo yangejisikia fahari kuwa naye Leo Kigoma wanamuona hana hadhi ya kuhushimika Bali Diamond?
Nyerere aliwahi sema zuzu anaweza kumiliki kipande cha Vito vya almasi lakini ukamdanganya na kumpa kipande cha chupa akupe Vito na akachekelea.
Maana yake Wakigoma wamekuwa mazuzu kubalilishiwa na wanachekelea? Sidhani kama wako hivyo!
wewe diamond amewahi kuwa mbunge jimbo gani,mpaka ukahisi hafai kabisa?
 
..usitumie maneno makali, wala usijadili kwa hasira ili twende pamoja.

kwanini nadhani ilikuwa sahihi kwa Sugu na Prof.J kugombea ubunge?

..kwa maoni yangu, Sugu na Prof walikuwa wameanza kufifia ktk tasnia ya muziki. Hivyo basi ubunge uliwapatia shughuli ya kufanya baada ya kuwa wamefifia kimuziki.

Kwanini naamini Diamond na Hamornize hawapaswi kugombea ubunge sasa hivi?

..Kwa mtizamo wangu, hawa wako ktk KILELE cha mafanikio ktk muziki. They are doing so well na mimi nadhani ni afadhali tuwa-encourage waendeleze muziki wao kuliko kuingia ktk shughuli za kisiasa.

Diamond na Harmonize washiriki vipi ktk uchaguzi wa 2020?

..kwa maoni yangu waipigie kampeni CCM. Lakini wasikubali kutumikishwa bila MALIPO.
Diamond na Harmonise ni watu wazima wenye kujua jema na baya.

Kumbuka kuwa vipaji haviishi, watakuja wengine na kuziba mapengo yao iwapo wataingia katika siasa.
 
wewe diamond amewahi kuwa mbunge jimbo gani,mpaka ukahisi hafai kabisa?
Hapimwi mtu kuwa anafaa au hafai eti mpaka apewe kazi hiyo kwanza, uelewa wake juu ya mambo ya kazi iliyo mbele yake ndio kipimo.
Au mnataka muendelezo was wabunge kama Deo Sanga?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tunachoangalia ,wasanii hao tayari ni wabunge nje ya bunge wanaosubiri kuapishwa tu mengine mtajua huko ukawa.
Una elimu gani? Ya akhera au ya duniani? Ulienda shule kupata maarifa au kutimiza wajibu?
 
Mkuu @Chakaza,siamini na kamwe sitaweza kuamini kuwa Diamond anaweza kushinda ubunge hapo kigoma dhidi ya yeyote,narufia tena YEYOTE,(kukiwa na uchaguzi huru na wa haki),sembuse ZZK.
Naamini wana Kigoma hawawezi kuwa wapumbavu kiwango hicho.
Waweza kuwa sahihi kabisa. Lakini tuwe wakweli, kumtoa Zitto Kabwe bungeni ili wamuingize Diamond jee watu wa Kigoma watakuwa wanatumia akili au kuchenguka na viuno tuu? Zitto ambaye kuna majimbo yangejisikia fahari kuwa naye Leo Kigoma wanamuona hana hadhi ya kuhushimika Bali Diamond?
Nyerere aliwahi sema zuzu anaweza kumiliki kipande cha Vito vya almasi lakini ukamdanganya na kumpa kipande cha chupa akupe Vito na akachekelea.
Maana yake Wakigoma wamekuwa mazuzu kubalilishiwa na wanachekelea? Sidhani kama wako hivyo!
 
Mkuu @Chakaza,siamini na kamwe sitaweza kuamini kuwa Diamond anaweza kushinda ubunge hapo kigoma dhidi ya yeyote,narufia tena YEYOTE,(kukiwa na uchaguzi huru na wa haki),sembuse ZZK.
Naamini wana Kigoma hawawezi kuwa wapumbavu kiwango hicho.
Kweli kabisa! Kigoma kuwa eneo masikini lakini CCM isiwadhanie kuwa Kigoma wana umasikini wa akili kiasi hicho.
Unamtoa Zitto unamuweka Diamond kama sio akili matope ni nini?
 
Back
Top Bottom