TANZIA Msanii wa HipHop SALU T afariki dunia

TANZIA Msanii wa HipHop SALU T afariki dunia

Nasikia alikuwa ni Shabiki mkubwa sana wa Yanga SC hivyo huenda mambo yakawa yameshatiki kwa Babu.

Simba SC Kesho mkipona sijui kwani nasikia tena kuna Mchezaji wao Kafiwa na Baba yake Mzazi.

Shikamooni Yanga SC na huyo Babu.
Watch your back young man! Wenye Jamii Forums yao wakikuotea na huku, sijui utakimbilia wapi tena.
 
Rest in Peace
#saluT . Kweli hip pop tuongeze kasi sana , na wapenda Fasihi tujaribu kupush sana kazi... huyu mwamba ni watu wengi hawakuwa wanamfahamu .... mpaka sasa ziko comment nyingi kwenye page ya JamiiForums watu wanatoa pole japo nyingi ni R.I.p japo simjui...
... Hip Hop imedolola bongo.... waimba ngono ndo wameshika kasi.

FB_IMG_16815760278283323.jpg
 
Msanii mkongwe wa Hip Hop nchini, Salutaba Mwakimwagile maarufu kama Salu T amefariki dunia jijini Mbeya leo tarehe 15 Aprili 2023. Msanii huyo amefariki akiwa anaendelea kupewa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya.

Akitoa taarifa ya awali, Msanii mwingine wa HipHop, Taikun Ally maarufu kama Mchizi Mox ameeleza kuwa jumanne tarehe 12 Aprili 2023, Salu T akiwa mkoani Mbeya katika harakati zake za maisha, alipata ajali ya gari iliyomsababishia majeruhi na maumivu ya mgongo. Imeelezwa kuwa hali ya Salu T ilikuwa mbaya na hivyo kupewa rufaa ya kwenda hospitali ya Taifa Muhimbili lakini hali yake haikuruhusu kusafiri na hivyo aliendelea kubaki hospitali ya Rufaa Mbeya mpaka umauti ulipomkuta.

Salu T amewahi kutamba na ngoma kama Chunga Sana aliomshirikisha msanii AY (2006) na kutayarishwa na Producer Lindu.

na ngoma nyingine nyingi, ikiwa ni pamoja na album iitwayo HAZINA.

Mchizi Mox ameeleza kuwa msiba wa Salu T upo nyumbani kwao marehemu mitaa ya Round about ya Mbuyuni, Kinyerezi Dar es Salaam na mazishi yanatajiwa kufanyika Jumatatu tarehe 17 Aprili 2023 jijini Dar es Salaam.

Pole kwa familia ya Salu T na wanaHipHop wote.

Mungu ailaze pema roho ya Salu T.
View attachment 2588702View attachment 2588703
View attachment 2588709
Majonzi yananikwaza nawaza nilopetza,

Misiiba haiishi Ardhi inatumeza,

Kila kukicha kifo wengi wanaomboleza,

Kufiwa ukiwa huzuni inajieleza,

Mtaa mzima kimya watoto sioni kucheza,

Wanawake machozi wapweke wasio jiweza,

Furaha imetoweka watani wanazebeza,

Sio lazima kugeza Mila zisizo pendeza,

Majamvi yametandazwa mwiko viti na meza,

Tuheshimu desturi vuziri kutozibeza,

"Siri ya mauti nini jibu analo muweza",

Wanaofariki hawarudi nani katokeza,

Vitu utatengeneza utainuka ukiteleza,

Uhai ungekua tajiri kama ungeuzwa kwa fedha,.....

" Nyota imedondoka, Taa imezimika"..... Nyota By Salu T
 
Msanii mkongwe wa Hip Hop nchini, Salutaba Mwakimwagile maarufu kama Salu T amefariki dunia jijini Mbeya leo tarehe 15 Aprili 2023. Msanii huyo amefariki akiwa anaendelea kupewa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya.

Akitoa taarifa ya awali, Msanii mwingine wa HipHop, Taikun Ally maarufu kama Mchizi Mox ameeleza kuwa jumanne tarehe 12 Aprili 2023, Salu T akiwa mkoani Mbeya katika harakati zake za maisha, alipata ajali ya gari iliyomsababishia majeruhi na maumivu ya mgongo. Imeelezwa kuwa hali ya Salu T ilikuwa mbaya na hivyo kupewa rufaa ya kwenda hospitali ya Taifa Muhimbili lakini hali yake haikuruhusu kusafiri na hivyo aliendelea kubaki hospitali ya Rufaa Mbeya mpaka umauti ulipomkuta.

Salu T amewahi kutamba na ngoma kama Chunga Sana aliomshirikisha msanii AY (2006) na kutayarishwa na Producer Lindu.

na ngoma nyingine nyingi, ikiwa ni pamoja na album iitwayo HAZINA.

Mchizi Mox ameeleza kuwa msiba wa Salu T upo nyumbani kwao marehemu mitaa ya Round about ya Mbuyuni, Kinyerezi Dar es Salaam na mazishi yanatajiwa kufanyika Jumatatu tarehe 17 Aprili 2023 jijini Dar es Salaam.

Pole kwa familia ya Salu T na wanaHipHop wote.

Mungu ailaze pema roho ya Salu T.
View attachment 2588702View attachment 2588703
View attachment 2588709

mmmh
 
Jamaa alikuwa illest rapper
Ana goma lake moja linaitwa darasa
Hutu mwamba mistari yake yote imeja
Ujumbe tu
Wanabana pua wapaka lipstick hawawez kumjua

Ova
Moja ya fun facts kumhusu mchizi ni kwamba katika carrier yake yote hakuna ngoma yeyote ambayo kaifanya halafu ndani yake katumia neno la kiingereza

Nash na Zavala walikuwa hawamfikii huyu jamaa kwa ku-stick kwenye kiswahili bila kuchanganya na kiingereza
 
Back
Top Bottom