TANZIA Msanii Waziri Ally Kissinger afariki dunia

TANZIA Msanii Waziri Ally Kissinger afariki dunia

23 July 2021
RIP Waziri Ally .

Toka maktaba online :
21 Mar 2019
MJUE MKONGWE WA MUZIKI WAZIRI ALLY WA KILIMANJARO BAND WANA NJENJE

Source : Muhidin Michuzi
 
Toka maktaba ya wazee, marehemu Waziri Ally alikuwa mpapasaji kinanda hatari sana kama wimbo huu hapa unavyodhihirisha :

Juwata Jazz Band - Sogea Karibu



Source : Zamani Leo
 
23 July 2021
Dar es Salaam, Tanzania

Waziri Ally wa The Kilimanjaro Band (Wana Njenje) afariki dunia


Habari zathibitishwa na vyanzo vya karibu na kuwa Waziri Ally alikuwa anapatiwa matibabu ktk Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Source : SimuliziNaSauti


Dunia Mapito!! Checkinorisi anatugalagaza sana kwenye Delta force.
 
Huyu amekufa mara ya pili? Mbona kama niliona tangazo lake hapa wakati wa wimbi la kwanza?
Yule wa mwanzo ni Hamis Omar aka Babu njenje.

100914322_3277857935559313_4581541768022287760_n.jpg
 
Muziki wa Dansi wakati nchi ina heshima na adabu unazidi kupoteza mibuyu yake na soon utabakia history,na huu uchafu tuliokua nao wa kizazi hiki umetuharibia mno utamaduni wetu(Taifa lisilokua na utamaduni wake ni Taifa mfu)sikiliza mziki wa nchi zetu jirani kama Malawi,Zambia,Botswana uasili wa utamaduni wao bado wanauendeleza,tumemezwa na mziki wa kikongo na S.A. haya ni makosa na uchezaji wetu wa mziki nao umemezwa na tamaduni nyingine!Amapiano ni mwendelezo wa Kwaito pale SA na sasa sisi tunajifanya kama wasouth!!;ulale pema Waziri Ally bingwa wa kinanda na ALLAH akuondoleee adhabu ya mauti!!sikiliza kibao cha Sogea Karibu (Juwata jazz)ahaaa sauti tamu ya Bitchuka ikimtamka Bwana Waziri wakati anapapasa kinanda akiumana na gita la solo la Mabera!!what went wrong nchi hii ?mbona kila kitu ni uozo tu?
 
Back
Top Bottom