dikteta2020
JF-Expert Member
- Aug 14, 2018
- 595
- 3,991
Shida ni watendajiDaah 😪
Hadi serikali inasuasua kuendesha kiwanda ...... sirikari🤯🤯
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Shida ni watendajiDaah 😪
Hadi serikali inasuasua kuendesha kiwanda ...... sirikari🤯🤯
Hata magari hawajaosha vizuriJkt wanajua kuosha magari tu
Kama wamekausha General Tyre Arusha usitegemee jipya kutoka kwao kiwanda kimebaki magofu tuu..mViongozi wa serikali nao kuwaza matumbo yao hawajambo mtu akipata chance basi lazima mpaka pakauke ndo anastuka
Kiko sekta binafsi kiache kwanzaHivi kile kiwanda cha madawa Arusha kimeishia wapi? Tanzania pharmaceutical industries nchi hii bhana ina mauza mauza.
Serikali ina asilimia 40% kwenye kiwanda hicho kimekufa kifo cha kawaida inasikitisha sana.Kiko sekta binafsi kiache kwanza
Hapa ni kulaumu serikali tu
Serikali hii pamoja na hao wawekezaji sijui tatizo ni nini kile kiwanda cha Madawa Arusha kinasikitisha sana.kuna vitu vyakijinga sana, yaani moja ya issue muhimu kabisa, kiwanda cha madawa nacho tunashindwa kuwa serious nacho.
Matokeo yake madawa yanatoka nje wabongo wanapigwa mabei yaajabu.
Wakati kiwanda kama hicho serikali ilipaswa kuwa macho nacho muda wote na ikiwezekana ikimiliki kwa 100% na kusimamia utengenezaji wa madawa huku ikisambaza kwenye hospitali zake kwa bei elekezi.
Sekta ya Afya ni muhimu sana kwa serikali kuwa macho nayo muda wote na sio kuruhusu maujingaujinga.
Kiwanda cha dawa?Wapewe jkt hicho kiwanda
TPI walisambaratika baada ya kashfa ya ARV Feki iliyoondoka na Joseph Mgaya aliyewahi kuwa DG wa muda mrefu pale MSD.Serikali hii pamoja na hao wawekezaji sijui tatizo ni nini kile kiwanda cha Madawa Arusha kinasikitisha sana.
Yalikuwa ni maamuzi ya hovyo kuvirudisha viwanda vilivyouzwa mwaka 1997. Magufuli alikurupuka tu, hakujua kwa nini viliuzwa na Mkapa . Serikali za kwenye free market economy hazifanyi biashara bali hutengeneza sera za biashara na kuzisimamia. Pia hutengeneza mazingira bora ya biashara na kujusanya kodi.Ni ajabu ila ni kweli. Bohari ya Dawa (MSD) ambayo ipo chini ya Wizara ya Afya ambayo Waziri wake ni Ummy Mwalimu ilikabidhiwa uendeshaji wa Kiwanda cha Dawa cha Keko na Msajili wa Hazina mwaka 2020, ambacho kinamilikiwa kwa Asilimia 70 na Serikali huku mbia binafsi akimiliki Asilimia 30.
Kiwanda hiki kipindi cha Dorothy Gwajima akiwa Waziri wa Afya kilifanikiwa kupewa zabuni na malipo ya awali ya zaidi ya fedha za Kitanzania Bilioni 6 ili kizalishe dawa za binadamu kwa MSD na hatimaye zisambazwe kwenye hospitali za umma baada ya kubainika kuwa hakina mtaji wa kujiendesha huku kikiwa na uwezo wa uzalishaji.
Ni kweli kwamba zilikuwepo changamoto za uzalishaji wa mahitaji hayo ya dawa kutokana na uongozi uliokuwepo kiwandani hapo kukosa ubunifu kwa kiasi kikubwa hivyo kupelekea uzalishaji kusuasua hata hivyo walifanikiwa kumaliza uzalishaji huo.
Cha ajabu baada tu ya Waziri Ummy kushika hatamu za kuiongoza Wizara ya Afya ni kama kiwanda hiki kinajifia. Hakuna mtaji wa uendeshaji wala malipo ya awali. Izingatiwe kuwa kiwanda hiki hakijawahi kupewa mtaji wa kujiendesha miaka 3 sasa baada ya kumilikiwa rasmi na Serikali kama mbia mkuu ikisaidiana na mbia mdogo binafsi.
Inashangaza kiwanda ambacho kilipiganiwa na hayati John Magufuli Rais wa Awamu ya Tano, kikarejea Serikalini na baadaye kikatembelewa na uongozi wa juu wa nchi huku kikiwa kwenye uzalishaji mzuri leo kinatelekezwa.
Nani anafaidika? Ni baadhi ya Watendaji Serikalini wakisaidiana na mbia binafsi ambaye alishindwa dhahiri kukiendesha na sasa anaona upo upenyo wa kuvuruga mambo baada ya Serikali kukikalia kimya?
Wafanyakazi wa kiwanda hiki nao wamegubikwa na sintofahamu kubwa baada ya mambo kuwa hayaeleweki. Ni sekta ipi hasa inawajibika kuondoa sintofahamu hii?
Ni jambo la ajabu kuona kiwanda kimechukuliwa na Serikali mwaka wa nne huku kikiwa hakisimamiwi kiutendaji na mamlaka za juu za nchi, mbaya zaidi kinajiendesha tu huku "chain of command" ikiishia kwa Wanao kiendesha ambao ni wawakilishi kutoka Serikalini wakiwa wanajiamulia tu waendeje na mambo.
Kama kiwanda hiki kilianza vizuri enzi ya Waziri Gwajima, inakuwaje baadaye kiwanda hiki kinageuzwa kuwa shamba la bibi kwa wanaokisimamia? Serikali inapaswa kuchukua hatua ili kuondoa sintofahamu hii ambayo inaathiri jamii ya wafanyakazi wa kiwanda hicho.