DOKEZO MSD ilikabidhiwa kiwanda cha madawa Keko lakini kinaelekea kufa…

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Viongozi wa serikali nao kuwaza matumbo yao hawajambo mtu akipata chance basi lazima mpaka pakauke ndo anastuka
Kama wamekausha General Tyre Arusha usitegemee jipya kutoka kwao kiwanda kimebaki magofu tuu..m
 
Ukitaka biashara yako ife wape wabongo inakufa mchana kweupe. Hicho kiwanda binafsisha kwa wahindi kitazalisha dawa zote muhimu.
 
Hivi kile kiwanda cha madawa Arusha kimeishia wapi? Tanzania pharmaceutical industries nchi hii bhana ina mauza mauza.
 
Hivi kile kiwanda cha madawa Arusha kimeishia wapi? Tanzania pharmaceutical industries nchi hii bhana ina mauza mauza.
Kiko sekta binafsi kiache kwanza

Hapa ni kulaumu serikali tu
 
kuna vitu vyakijinga sana, yaani moja ya issue muhimu kabisa, kiwanda cha madawa nacho tunashindwa kuwa serious nacho.

Matokeo yake madawa yanatoka nje wabongo wanapigwa mabei yaajabu.

Wakati kiwanda kama hicho serikali ilipaswa kuwa macho nacho muda wote na ikiwezekana ikimiliki kwa 100% na kusimamia utengenezaji wa madawa huku ikisambaza kwenye hospitali zake kwa bei elekezi.

Sekta ya Afya ni muhimu sana kwa serikali kuwa macho nayo muda wote na sio kuruhusu maujingaujinga.
 
Serikali hii pamoja na hao wawekezaji sijui tatizo ni nini kile kiwanda cha Madawa Arusha kinasikitisha sana.
 
Kiwanda kipewe mbia akiendeshe kibiashara, serikali iwe sehemu ya mmiliki kwa asimia 50% au 49%. Mabenki kama NMB, NBC na mashirika mengine ambayo serikali inamiliki hisa yanajiendesha kibiashara na kwa faida. Nchi hazipaswi kufanya biashara moja kwa moja, urasimu ni mwingi itapelekea kiwanda kufa.

Fikiria kipuri kimeharibika usiku, kinahitaji marekebishi ya haraka, sasa uanze taratibu za manunuzi za kiserakali na madokezo kutafuta fedha, si kitakufa??.
 
Serikali hii pamoja na hao wawekezaji sijui tatizo ni nini kile kiwanda cha Madawa Arusha kinasikitisha sana.
TPI walisambaratika baada ya kashfa ya ARV Feki iliyoondoka na Joseph Mgaya aliyewahi kuwa DG wa muda mrefu pale MSD.
Baada ya hapo , Wakurugenzi wao Mr+ Mrs Madabida wakatembea na kesi ya Uhujumu Uchumi Kwa zaidi ya miaka 5 na grants zote walizotarajia kupanua uzalishaji haswaa wa ARVs ndo zikaota mbawa.
Pamoja na serikali kuwa na hisa( Minority Shareholding) ndani ya TPI,Siasa ziliwaathiri sana Kwani Mkurugenzi wao Madabida,akiwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, wakati wa Tanzania 2015 Presidential Candidate Nomination alijitokeza wazi wazi kusimama na Team Lowassa, hivyo utawala wa mwendazake ulivyoingia akapigwa spana za kutosha na kupoteza welekeo ,hata kesi zao zimeisha baada ya Magufuli ku- RIP
Pengine Sasa ndo wanajipanga kufufuka
 
Yalikuwa ni maamuzi ya hovyo kuvirudisha viwanda vilivyouzwa mwaka 1997. Magufuli alikurupuka tu, hakujua kwa nini viliuzwa na Mkapa . Serikali za kwenye free market economy hazifanyi biashara bali hutengeneza sera za biashara na kuzisimamia. Pia hutengeneza mazingira bora ya biashara na kujusanya kodi.

Mnasema angekuwapo eti kisingekufa?. Angezuiaje yeye kisife?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…