TUache Ushabiki wa Vyama: Nadhani hawa ndio wazee waliokuwa wanakilinda chama wakati CCM ikiwa yenye Nguvu, ila hawakuwaandaa vijana wao kuwa na uwezo kama wao wa ku-deal na hoja motot bila kulipua moto zaidi yaani ni wataalamu wa kupooza hoja za moto. Ila nimependa pia tofauti na vimeo kama akina Makamba, yeye anaafiki udhaifu wa chama chake, anaushika na utovu wa nidhamu akisistiza kutokuwepo kwa maadili ndani ya chama chake, nawajua mamluki wa CCM waliomuuliza swali la maadili nadhani walimtaka mzee akiokoe chama kwa kusisitiza tatizo sio chama ila ni utovu wa nidhamu. NIMEPENDA HOJA YA mhusika mmojawapo aliposisitiza kuwa Mfumo (ambao ni katiba) usipokuwa imara unatoa mwanya kwa kutokuwepo kwa maadili na kutokuwepo mfumo wa kuwawajibisha wahusika. Sidhani kama maoni aliyotoa ni ya chama chake.
Sipati picha kilaza Makamba atakavyoropoka kesho maana duh! Ya leo ni oposite na wajinga wengi waliomo ndani ya CCM.
NIMEPENDA Zito Kabwe alivyotumia vizuri mbinu za Propaganda kwa kumuingiza kingi mzee na akauvaa.... nilicheka sikuweza kuvumilia mzee akauvua U-CCM na kuanza kubwabwaja maana angebaki kwenye U-CCM angetuboa zaidi maana si angeng'ngania vimsimamo viozo vya vilaza na mafisadi wenzao... ila ubaya alishindwa kumaintain hiyo ya kujivua maana yawezekana kabisa aliagizwa ... vijana wamemchakachua mpaka akaingia chaka saaafi sana vijana wa People's Power... naifagilia CCM kama chama ila nawachukia wooote waliomo ndani yake kwa sasa maana ni waozo wa kila aina name it wajinga wazembe wezi mafisadi wanafiki nisaidieni kumalizia jamani.....
Big up vijana wa Pople's Power leteni mabadiliko wakati ndio huu wa kuandika Historia Msifanye fujo waacheni wafanye wao halafu sijui watajificha wapi masikini....