Msemaji Mkuu wa Serikali: Kumekuwa na upotoshaji kuhusu tozo, Wizara ya Fedha itatoa ufafanuzi tozo zilizopunguzwa

Msemaji Mkuu wa Serikali: Kumekuwa na upotoshaji kuhusu tozo, Wizara ya Fedha itatoa ufafanuzi tozo zilizopunguzwa

Tozo zilete unafuu kwa wananchiu tena?😂😂😂 Huyo mnsemaji anastahili makofi kabisa. Watu wanalalamiuka hela zao zinakwapuliwa nyie mnasema kuna unafuu kwa mwananchi like serious, katika serikali ambazo zishawahi feli hii ya awamu hii itakuwa mfano duniani.
Atakuwa anadhani nasi tunalamba asali kama wao.
 
Ule ufafanuzi kuhusu nyongeza kiduchu ya mshahara alishaitoa?
 
"TAARIFA

Kuna upotoshaji mkubwa kuhusu tozo za miamala ya kielektroniki iliyoanza katika mwaka huu wa fedha (2022/23). Serikali imepunguza kwa kiasi kikubwa tozo hizo. Wizara ya Fedha itatoa ufafanuzi kuhusu tozo hizi na namna zilivyoleta nafuu kwa wananchi. NAOMBA TUTULIE."
Hivi hadi inafikia hatua ya kupunguza, nani aliyezi-initiate?

Au ndo mambo ya kujitia dole na kisha kunusa (hahaha haa)

Sema nisiseme sana.
 
Wapi nyepesi from Kigoma yupo kimya na kopo la asali.kweli kila mtu apambanie tumbo lake
 
Msemaji amekuwa akitetea wizi ili cheo chake kibaki ila mjue mwisho wa ubaya ni aibu...endeleeni kutukamua wananchi kwa mitozo yenu isiyokuwa na maana kabisa ambayo inasababisba kupanda kwa bei ya vitu na kuwafanya wanachi wasifurahie maisha katika nchi yao iliyoumbwa na Mungu mwenye upendo ila ninyi ndio mashetani mnaondoa furaha yao.
 
Wanatufanya wananchi wajinga, si ni huyu alidai serikali itakuja kulitolea ufafanuzi swala la nyogeza kiduchu ya mshahara? Na alipokuja PM kutapika uchafu ndio ikawa imeisha
 
Cha muhimu ni kuziondoa siyo kuzipunguza kwani hawakushirikisha wananchi. Yaani hazitakiwi hakuna atakayeshangilia hata kama watabakiza 0.0001



Sahihi kabisa.

Umenena vyema kabisa.

Kama ni mshahara ulishakatwa kodi ya PAYE kama ni biashara kodi zake zishalipwa corporate tax, VAT, WHT n.k
Kama ni kipato toka uwekezaji kodi ya zuio ilishakatwa sasa hayo matozo msingi wake ni nini ?

Hapana aisee!

Hatutaki.
 
Back
Top Bottom