Msemaji Mkuu wa Serikali: Serikali inafuatilia kwa ukaribu mijadala ya JamiiForums, ile ya kufaa itachukuliwa na kufanyiwa kazi

Yote mazuri na ya kweli ila hapo katika "mkataba wa bandari" si hoja ya walio wengi.....

Una takwimu ya wapingao mkataba wa bandari??!! [emoji1787]
 
Hekima imetawala. Kuna vicheche walikuwa wanakimbilia kuufungia mtandao huu wasijue kuwa wanapata maoni ya Watanzania, opinion makers, kwa gharama nafuu sana. Lakini suluhu siyo maoni kupatikana ila ni upatikanaji wa viongozi wenye ufahamu,maono na uwezo wa uendeshaji, siyo Usultani. Mtandao hauwezi kututafutia viongozi wa kuirudishia heshima ya Tanzania iliyokuwa imefikia katika kutafuta haki, maendeleo jumuishi na elimu ya kujitegemea ambayo ilikuwa inaogopewa na mataifa hata yaliyoendelea! Viongozi waliopo wajipime kwa viwango ambavyo tumewahi kufikia badala ya mipasho tunayoisikia na sifa za Phd, mambo ambayo hayana mchango wo wote kwenye maendeleo ya Watanzania.
 
Yote mazuri na ya kweli ila hapo katika "mkataba wa bandari" si hoja ya walio wengi.....

Una takwimu ya wapingao mkataba wa bandari??!! [emoji1787]
Wenye akili wachache wakiunga au kupinga jambo la serikali ni vyema kujua wanawakilisha waliowengi, zingatia neno "wenye akili"
 
Kuna kitu ambacho Msemaji kasahau kusema au kaamua kutokusema... ni kuwa serikali imevutiwa zaidi na nyuzi zangu mimi. Binafsi namshukuru Mungu na kujishukuru mwenyewe kwa kuandika nyuzi zinazogusa jamii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…