Msemaji Mkuu wa Serikali: Serikali inafuatilia kwa ukaribu mijadala ya JamiiForums, ile ya kufaa itachukuliwa na kufanyiwa kazi

Msemaji Mkuu wa Serikali: Serikali inafuatilia kwa ukaribu mijadala ya JamiiForums, ile ya kufaa itachukuliwa na kufanyiwa kazi

Ni muelekeo mzuri sana kwa Serikali kutambua na kuthamini michango ya JamiiForums.

Kulingana na kauli ya Msemaji Mkuu wa Serikali, kuwa Serikali inapanga kuchukua hatua za kupongezwa na muhimu, kama vile kufuata ushauri wa wana JF, kukabiliana na changamoto zinazoikabili Taifa and so on, nashauri wazingatie Akili bandia,Habari potofu na Habari zisizo za kweli.

Nasisitiza, Serikali iendelee kuheshimu na kulinda utamaduni na mila za Watanzania.



Hatahivyo,Watanzania wanasema hatujardhika na Mkataba mbovu wa Bandari.
Yote mazuri na ya kweli ila hapo katika "mkataba wa bandari" si hoja ya walio wengi.....

Una takwimu ya wapingao mkataba wa bandari??!! [emoji1787]
 
Msemaji Mkuu wa Serikali Bw. Mobhare Matinyi amesema ukisoma JamiiForums hata kama umeingia umenuna utacheka tu kwa kuwa ni sehemu inayowapa watanzania uhuru wa kuzungumza.

Ameipongeza JamiiForums kwa kuandaa shindano la stories of Change ambalo halfa ya utoaji wa zawadi kwa washindi inafanyika leo, Oktoba 7, 2023 kwenye hoteli ya Hyatt Regency, the Kilimanjaro.

Amesema jukwaa la stories of change linatoa fursa nyingi ikiwemo ya kukuza kiswahili, lakini Tanzania ina mtandao huu mmoja unaotumiwa na watu zaidi ya milioni 20.

Ameisifu JamiiForums kwa kuanzisha jukwaa la JamiiCheck linalowashirikisha wananchi Mchakato wa kuhakiki usahihi wa maudhui yanayopatikana ndani na nje ya mtandao.

Pia, amesema Serikali inafuatilia kwa ukaribu mijadala ya JamiiForums, ile ya kufaa itachukuliwa na kufanyiwa kazi.

Katika hatua nyingine, Bwana Mobhare amesema JamiiForums ni taasisi ya mfano katika kuwajengea uwezo waandishi wa habari ambapo sasa mojawapo ya miradi yake ni kuwajengea uwezo waandishi wa habari 600 nchi nzima ili kusaidia upatikaji wa taarifa za kutosha.

Zaidi, soma: Yanayojiri katika Usiku wa Utoaji Zawadi kwa Washindi wa Shindano la Stories of Change 2023
Hekima imetawala. Kuna vicheche walikuwa wanakimbilia kuufungia mtandao huu wasijue kuwa wanapata maoni ya Watanzania, opinion makers, kwa gharama nafuu sana. Lakini suluhu siyo maoni kupatikana ila ni upatikanaji wa viongozi wenye ufahamu,maono na uwezo wa uendeshaji, siyo Usultani. Mtandao hauwezi kututafutia viongozi wa kuirudishia heshima ya Tanzania iliyokuwa imefikia katika kutafuta haki, maendeleo jumuishi na elimu ya kujitegemea ambayo ilikuwa inaogopewa na mataifa hata yaliyoendelea! Viongozi waliopo wajipime kwa viwango ambavyo tumewahi kufikia badala ya mipasho tunayoisikia na sifa za Phd, mambo ambayo hayana mchango wo wote kwenye maendeleo ya Watanzania.
 
Yote mazuri na ya kweli ila hapo katika "mkataba wa bandari" si hoja ya walio wengi.....

Una takwimu ya wapingao mkataba wa bandari??!! [emoji1787]
Wenye akili wachache wakiunga au kupinga jambo la serikali ni vyema kujua wanawakilisha waliowengi, zingatia neno "wenye akili"
 
Kuna kitu ambacho Msemaji kasahau kusema au kaamua kutokusema... ni kuwa serikali imevutiwa zaidi na nyuzi zangu mimi. Binafsi namshukuru Mungu na kujishukuru mwenyewe kwa kuandika nyuzi zinazogusa jamii.
 
Back
Top Bottom