Kwa mujibu wa video ya mauaji ya joshua tukio lilifanyika ndani ya israeli maana Joshua hakuwa akisoma Gaza mkuu. Na ni wazi ilikuwa ni siku ya uvamizi tarehe 7.10.2023 sidhani baada ya hapo Hamas walirudi israeli kufanya tukio jengine baada ya tarehe 7.10.2023.
Umeona lakini jamaa alivyokua anajibu maswali yangu Kwa weledi, ufasaha na bila mihemko? Vyanzo vya taarifa za majibu yake ameviweka hapa.
Taarifa kwamba miongoni mwa mateka waliotekwa na Hamasi, Kuna watanzania wawili, ameweka hapa, taarifa kwamba mmoja amefariki, ameviweka hapa.
Hii vita imezongwa na upotoshaji, hisia, chuki na udanganyifu mwingi sana kutegemea mtu anashabikia upande upi wakati hapa tunaongelea uhai wa watu.
Ni jambo ambalo najizuia sana kulijadili Kwa mihemko, hata kubishana sana kuhusu haya mambo ukizingatia Kuna watu lazima waingizie udini kwenye huu mjadala.
Kama hauna taarifa sahihi za kuhusu utekwaji na mauaji huyu jamaa, kupata majibu ya maswali yako ni ngumu sana.
Haujawezathibitisha kwamba jamaa aliywawa 07 October au alitekwa wakaenda nae Gaza. Na Hamas hawajakanusha kuwa na mwili wa huyo jamaa Kwa vile taarifa za awali, alikua miongoni mwa mateka. Na hawajakanusha kwamba wamemuua au amejeruhiwa na Jeshi la Israel. Kumbuka hili jeshi limewaua raia wao wenyewe ( Kwa mujibu wao ni Bahati mbaya) na hili jambo limezidi kuchochea ghadhabu ya waisrael dhidi ya waziri Mkuu. Wangeweka wazi kwamba mtanzania mwenzetu nae alikua miongoni mwa waliouawa kwenye mashambulio kati Yao na Hamas.
Si unataarifa hadi Leo milipukon ya September 11 huko Marekani bado imeacha maswali mengi yasiyo na majibu?
Cha msingi serikali yetu inatakiwa kutoa taarifa za kilichotokea kutuliza hii tafran.