Msemaji wa JWTZ kuteuliwa kwenye NEC ya CCM, hii imekaaje?

Msemaji wa JWTZ kuteuliwa kwenye NEC ya CCM, hii imekaaje?

ukisha jua 2020 hutoboi lazima upange safu ya kulazimisha kuingia king ili ule kete zingine kiulaini.

jamaa ameshajua hatoboi ndo maaana safu inapangwa ya kibabe tu hakuna kufata misingi
 
Shida kubwa ya Watanzania tuna tabia ya kusahau.marehemu Mosses Nauye, marehemu Captain Komba, Canali Abdahaman Kinana wote hawa walitumikia Jeshi still walitumikia chama so hakuna kitu kipya.Jamani can we use our energy to participate in the productive sectors and so widen the tax base of our Nation than continue with this kind of issues
Acha ungese wakitumikia tukiwa ktk vyama vingi au Chama kimoja?
 
NI UKIUKWAJI WA KATIBA AU MAJINA YAMEFANANA KATI YA MSEMAJI WA JWTZ NA HUYU MTEULE WA NEC YA CCM?
JPM JITOKEZE KUUELEZEA UMMA KUHUSU UTATA HUU.​

Msemaji wa JWTZ ni Kanali Ngemela Lubinga.

Katibu Mteule wa NEC ya CCM Siasa na Uhusiano wa Kimataifa ni Kanali Ngemela Eslom Lubinga.

Katiba ya Jamhuri 1977 inasema :-

SURA YA TISA
MAJESHI YA ULINZI

Ibara ya 147.

Ibara ndogo ya (3),
Itakuwa ni marufuku kwa mwanajeshi yeyote kujiunga na chama chohote cha siasa, isipokuwa tu kama atakuwa na haki ya kupiga kura iliyotajwa katika ibara ya 5 ya Katiba hii.

Ibara ndogo ya (4),
Kwa madhumuni ya ibara hii, "mwanajeshi" maana yake ni askari aliyeajiriwa kwa masharti ya muda au ya kudumu katika Jeshi la Ulinzi, Jeshi la Polisi, Jeshi la Magereza au Jeshi la Kujenga Taifa.

----------
Bro huyu mtu hajastaafu..kwenye maadhimisho ya JWTZ juzi septemba mosi ndo alikua msemaji je kastaafu lini?
 
Wwe ndo hujui taratibu sasa nikueleze pamoja na ujinga wako!!ukiacha sheria na katiba na nini sijui;rais ana mamlaka ambayo amepewa kikatiba kufanya unayoyaona!tatizo watz wengi hatujui sheria na elimu imetupita kushoto!isome katiba,mamlaka ya rais halafu ndo uje unitolee povu lako;Ndo maana alimtoa chagonja akambadilisha jeshi na kumpeleka fire,alimtoa mlowola polisi akampeleka takukuru,na hao wote walikuwa wako kazn halaf bado unahoji anakiuka tartibu zipi??
Tofautisha govt na Chama acha mahaba halafu si ajabu una kadegree kutoka St nini sijui
 
That is a hoax!! Let us be serious. Kwa nini tuwaingize wanajeshi wetu kwenye siasa kabla hawajastaafu? Tumeona Trump akiwateuwa wanajeshi kuwa mawaziri wake, lakini ni wale waliostaafu jeshi walio katika mrengo wa Republican, na wala si walio kazini. Vinginevyo ni kuwapandisha vyeo basi.
Pamoja na Trump kuwateua bado inatakiwa aiombe Senate iwaondolee Kinga ya kutokufanya kazi za kiraia iliyopo kwa mwanajeshi mstaafu kwa miaka 7 baada ya kustaafu so tusilinganishe hivi vitu viwili. Wanaocjaguliwa ni wastaafu na bado wanhitaji ruhusa ya Congress kwetu they are just taped from the army to civilian offices without any procedural to remove their influence in the army.
 
Lowasa walipomchukua CHADEMA walimjua siku nyingi? Mbona aliingia tu na kupewa ugombea uraisi wakati hajawahi kuwa kiongozi wa tawi la chadema
Mimi nionavyo JF sasa hivi imekuwa jukwaa la siasa tena viwili. Ushauri wangu kwetu waJF tuchangie maada kikatiba na kisheria kama mtoa thread alivyoleta. Jamii ya watz ni kubwa kuliko wanaccm na wanachadema. Yaani tusiokuwa na chama tuko wengi.
 
Pigeni kelele weeeeee lakini treni ndio imeshakolea mwendo hivyo...endeleeni kulima bagamoyo na kupeana vyeti kwenye matenti porini huku mkiendelea kutengeneza movie ya mwana mpotevu
 
Huyu Mjeshi Ndiyo Kasema Ukweli Mtupu Kuhusu Ccm Yaani Tangu 1979 Ni Mwanachama Mpaka Anastaafu
Hapo Ndiyo Kasema Ukweli Mtupu
 
02ea95f75d8b682e1bd28f98895da9e6.jpg
 
Lowasa walipomchukua CHADEMA walimjua siku nyingi? Mbona aliingia tu na kupewa ugombea uraisi wakati hajawahi kuwa kiongozi wa tawi la chadema
JPM alishawahi kuwa mwenyekiti wa level yoyote lichama kabla?
 
akiteuliwa anastaafu uanajeshi, itachukuliwa kuwa amestaafu
Ukeyasikia majibu yake huyo aliyeteuliwa..?? Amesemw kwamba alikiwa mwanaCCM tangu enzi za chama kimoja.. kwa hiyo alikuwa mwanajeshi huku akiwa mwanacham wa chama cha siasa, jambo ambalo ni kinyume cha katiba
 
Shida kubwa ya Watanzania tuna tabia ya kusahau.marehemu Mosses Nauye, marehemu Captain Komba, Canali Abdahaman Kinana wote hawa walitumikia Jeshi still walitumikia chama so hakuna kitu kipya.Jamani can we use our energy to participate in the productive sectors and so widen the tax base of our Nation than continue with this kind of issues
No wonder hata historia yako huijui, seuze ya nchi. Huo upuuzi wote ulipigwa chini na Tume ya Nyalali kuelekea multiparty system. Ndio maana hao uwatajao wote walitoka jeshini akiwemo Kikwete, Jakka Mwambi, Mkuchika et al.

Hoja ya mtoa hoja anahoji how comes ktk mfumo huu tuliopo kwa nini ujinga wa single party ruling Sizonje anauleta zama hizi za Multiparty system? Na kikatiba hairuhusiwi kwa mtu wa umma kujihusisha na siasa angali yupo ktk utumishi.

"MKUKI MTAMU KWA MCHUNGU, KWA BINADAMU NGURUWE".
 
Back
Top Bottom