Swagger is alive
JF-Expert Member
- Jul 8, 2016
- 559
- 467
Ndio umezinduka leo?! We Unadhani ccm kujiita Chama Dola maanake niniKumbe jwtz ni ccm pure,ndiyo maana Seif akishinda urais Zanzibar,fasta wanapeleka vifaru kumtisha aisee!!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ndio umezinduka leo?! We Unadhani ccm kujiita Chama Dola maanake niniKumbe jwtz ni ccm pure,ndiyo maana Seif akishinda urais Zanzibar,fasta wanapeleka vifaru kumtisha aisee!!
- Lakini Lowassa alipoteuliwa kugombea Urais Chadema haikukushangaza imekushangaza huku? Duh!
le Mutuz Nation
Kila mara nakuambia huwa unakuwa umri kwa maana ya miaka kusonga na sio akili wala uelewa. Mada hapa ni mwanajeshi kuingizwa kwenye vyeo vya kisiasa kulingana na takwa la katiba yetu. Je nikuulize, Lowassa ni mwanajeshi?
Ni hivi hakuna anayepuuzia masuala ya katiba. Hao walioona kuwa katiba imevunjwa mimi nimewauliza then what? Miaka yote kilio ni kile kile. Uzi ukishafika page ya 8 au 10 basi inaishia hapo. Kama mmeona ni kosa then nini kinafuatia. Au mkishapost humu watu wakawatukana hao CCM basi kifungu cha sheria kilichovunjwa kitanyooka.
- Nilidhani utai quote Katiba ya Chadema kuhusu Mwanachama mwenye sifa za kugombea urais kwani inasemaje kuhusu Mgombea mgeni ambaye hajamaliza hata miezi mitatu? hahahahaha kila mara nakuambia watoto wachanga kama wewe wapo wodi ya Mwaisela husikii why?
le Mutuz
Akili ndogo ni tatizo. Rais akiamua kutumia Katiba kifalme atafanya yote pamoja na hayo unayoyasema. Lakini Rais mwenye upeo mkubwa wa uongozi ni lazima atambue kuwa "si utamaduni wa kitanzania" nikiazima maneno ya Mwalimu Nyerere, kupuuzia misingi ya utawala bora katika nchi ya kidemokrasiaWwe ndo hujui taratibu sasa nikueleze pamoja na ujinga wako!!ukiacha sheria na katiba na nini sijui;rais ana mamlaka ambayo amepewa kikatiba kufanya unayoyaona!tatizo watz wengi hatujui sheria na elimu imetupita kushoto!isome katiba,mamlaka ya rais halafu ndo uje unitolee povu lako;Ndo maana alimtoa chagonja akambadilisha jeshi na kumpeleka fire,alimtoa mlowola polisi akampeleka takukuru,na hao wote walikuwa wako kazn halaf bado unahoji anakiuka tartibu zipi??
Mimi sio mwanacdm hivyo kwa bahati mbaya sijui katiba yao inasemaje kuhusu hilo. Ila nikiri ni shabiki wa chama hicho. Pitia post zangu hapa jukwaani, mimi ni mmoja kati ya watu niliopinga na bado naendelea kupinga uwepo wa Lowassa ndani ya cdm tena kama mgombea wa urais. Ila kwa kuwa sio mwanachama hivyo sina nguvu ya kumpinga kwani nadhani wanachama ndio wenye nguvu hiyo kikatiba. Je una lingine mzee?
fanya kazi kwa bidii na kujituma mkuu. kwa style hii ya kulalamika nyuma key bodi mbona utasaga meno kwa kipindi kirefu sanaYani kweli kuna watu wanabahati zao,mtu yupo katika ajira ya serikalini anaachishwa na kuletwa kwenye chama, dah vyeti vyangu ngoja viliwe na panya tu
Tulia kaka tupige hela we hutaki nivute RactisUmeshaona fursa kijana ... ?! [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Hata Mahakama sasa ziko Lumumba .., usijisumbue ...
Ni wale vilaza kuamka tuu ndio itasaidia, and it might take a decade such a thing to happen ...
Ndugu nimekuwa nikifuatilia majibu yako mengi hapa jukwaani kwenye uzi huu na nyingine pia. Unaoneka kujibu kwa kejeli, dharau na kiburi cha madaraka. Sishangai kwani hata awamu hii inaonyesha kuenda na haiba yako. Hiki kinachofanyika kwako na wengineo wa aina yako hakuna shida kwani mnaamini mna ruhusa ya kufanya chochote kwa utashi wenu na katiba mnaitumia mnapodhani haiwabani. Ila mtambue kuna kitu mnapandikiza bila kujua madhara ya muda mrefu kwa mapenzi yenu ya muda mfupi mtakaokuwa madarakani. Hao wanajeshi kuanza kuwapa vyeo vya kisiasa iko siku mtataka watoke mtashindwa, hao walioona hiyo hatari huko nyuma sio wajinga kulingana na aina yao ya mafunzo. Kumbuka siasa ni ushawishi na sio amri, je kuna mwanajeshi anayefundishwa ushawishi?
Kiburi kilichowajaa kwa sasa ni kweli kitawafanya mfurahi na kujipongeza kwamba mmenyoosha nchi. Lakini kumbuka nchi hii ina vyama vingi vya siasa, hao jamaa watastaafu na wakati huohuo wataona fursa kwenye siasa, huenda wakaamua kujiunga huko. Sipati picha watakapotumia ushawishi wao wa wengine waliowaacha huko vikosini wapate support kupata madaraka ili wawape vyeo pindi wakiingia madarakani. Ni nani akitarajia mawaziri wakuu wastaafu na hata mawaziri wangejiunga kwenye vyama vya upinzani tena kwa kiu ya madaraka? Sumu haionjwi kwa kuilamba. Leo ongozweni na kiburi cha madaraka ila mtakuja kugundua mmechemsha mkiwa wazee na huku madhara yakiwa ndani ya nchi, leo wote tunaona malezi na tamaa ya mali ya vijana wetu, sasa nini kitatokea huko mbeleni muda utaamua.
- Ok sasa unashangaa CCM kuchagua kiongozi wake ambaye ni mfanyakazi wa Serikali yake! Are serious or just kidding?
le Mutuz
Tunga kitabu au ungeweza hata ku summarize hizo pumba zote hadi ziwe mchele. Maana nimeshindwa hata kusoma. Tofautisha maana ya comment na insha
Jazba. Hiyo ndio raha ya demokrasia unaweza kusema upendacho na kila mtu anaweza kuchangia anavyoona. Huna ulazima kusoma kitu kinachopunguza ufahari wako.
That is a hoax!! Let us be serious. Kwa nini tuwaingize wanajeshi wetu kwenye siasa kabla hawajastaafu? Tumeona Trump akiwateuwa wanajeshi kuwa mawaziri wake, lakini ni wale waliostaafu jeshi walio katika mrengo wa Republican, na wala si walio kazini. Vinginevyo ni kuwapandisha vyeo basi.akiteuliwa anastaafu uanajeshi, itachukuliwa kuwa amestaafu
Jazba unaniletea mimi ambae sikulishi wala sikuvishi. Hunijui sikujui. Kweli bavicha mna matatizo ya akili iko siku mnaweza hata kuweka BIFU na UKUTA AU KIVULI CHAKO