Msemaji wa JWTZ kuteuliwa kwenye NEC ya CCM, hii imekaaje?

Msemaji wa JWTZ kuteuliwa kwenye NEC ya CCM, hii imekaaje?

Zamani kabla ya mfumo wa vyama vingi, jeshi letu lilikua sehemu ya mfumo wa siasa. Hilo lilifanywa makusudi kwa vile chama ndio kilidhika hatamu hivyo jeshi wakawa na mkoa wa jeshi wa chama..ulikua uamuzi wa busara.
Mara baada ya kuingia mfumo wa vyama vingi Mwalimu alishauri kulitoa jeshi katika mfumo wa vyaka. Katiba ikabadilishwa na kukataza jeshi kujiunga au kuwa mwana chama wa chama chochote cha siasa. Waliruhusiwa kupiga kura tu.
Huu nao ni uamuzi wa husara na hekima kubwa kuchukuliwa. Lengo kulifanya jeshi letu liwe la Tanzania wote bila ya kujali chama cha mtu yoyote. Hii pia ni kuendana na mfumo wa vyma vingi tukiruhusu jeshi kuingilia siasa , wapo watakao na mapenzi na chadema , nccr au cuf....hivyo tutaligawa jeshi letu.
Waasisi wa taifa na mfumo huu waliliona hili. Hivyo ni utaratibu mzuri ....
Sasahaya yasasa hatujui sababu zake ni zipi kuwaingiza katika siasa...
Nimekupa like kubwa bro. Sasa ona akili ndogo za viongozi wa ccm wa leo inavyolirudisha jeshi letu sote kuwa jeshi lao. Jeshi linajua kuwa ni la Watanzania wote lakini viongozi wa ccm wanalibinafsisha kwenye chama, halafu mataahira yanakuja kutetea upuuzihuo humu!!!
 
Hatuiombei nchi yetu mabaya lkn hii ya kuchomoa wanajeshi na kuwapachika kwenye nyazifa za chama itakuja kuwarudi CCM. Kipindi hiki ni tofauti na enzi za chama kimoja. Kuwa mwajeshi hakumbadilishi mtu attitude yake. Wakati huu wa vyama vingi mtatengeneza gaps ndani ya mioyo yao badala ya umoja. Wanajeshi tuwatengezee mazingira ya wao kujifeel wanawalinda watanzania badala ya kujisikia wanawalinda wanaccm au wanaukawa.
 
Akili ndogo ni tatizo. Rais akiamua kutumia Katiba kifalme atafanya yote pamoja na hayo unayoyasema. Lakini Rais mwenye upeo mkubwa wa uongozi ni lazima atambue kuwa "si utamaduni wa kitanzania" nikiazima maneno ya Mwalimu Nyerere, kupuuzia misingi ya utawala bora katika nchi ya kidemokrasia

Siasa na jeshi havitengani, na imeanza zamani toka enzi za Nyerere.Ngemela sio wa kwanza.
 
That is a hoax!! Let us be serious. Kwa nini tuwaingize wanajeshi wetu kwenye siasa kabla hawajastaafu? Tumeona Trump akiwateuwa wanajeshi kuwa mawaziri wake, lakini ni wale waliostaafu jeshi walio katika mrengo wa Republican, na wala si walio kazini. Vinginevyo ni kuwapandisha vyeo basi.
Waziri wa Ulinzi aliyeteuliwa na Trump juzii alimaaarufu km mbwa kichaa, ni mwanajeshi.
 
Umepandisha jazba mpaka umetoka kwenye hoja ya msingi na kuweka wazi udhaifu wako. Kwa bahati mbaya mimi sio mwanacdm wala sijawahi kuwa mwanacdm. Sasa nimegundua kwanini unaongea kwa kejeli, jazba na dharau. Samahani kwa nilichokuambia nilitaraji ujengaji wa hoja kumbe nimeishia hapa.
Nipandishie Jazba ukuta au Mtu ambaye sijui kuwa ni mwanamke au mwanaume. Pole sana kama fikra zako zinakupeleka huko.
 
Siku unayoteuliwa unaacha jeshi huwi mwanajeshi na unashika madaraka siku hiyo hiyo kama ambavyo lowasa alivyofanya.Siku alipoteuliwa na CHADEMA kuwa mgombea siku hiyo hiyo aliacha CCM na kuwa mgombea uraisi
Hata tulia mlimzoa kwa Style hyo.Mmezoea kuwatumia.
NI UKIUKWAJI WA KATIBA AU MAJINA YAMEFANANA KATI YA MSEMAJI WA JWTZ NA HUYU MTEULE WA NEC YA CCM?
JPM JITOKEZE KUUELEZEA UMMA KUHUSU UTATA HUU.​

Msemaji wa JWTZ ni Kanali Ngemela Lubinga.

Katibu Mteule wa NEC ya CCM Siasa na Uhusiano wa Kimataifa ni Kanali Ngemela Eslom Lubinga.

Katiba ya Jamhuri 1977 inasema :-

SURA YA TISA
MAJESHI YA ULINZI

Ibara ya 147.

Ibara ndogo ya (3),
Itakuwa ni marufuku kwa mwanajeshi yeyote kujiunga na chama chohote cha siasa, isipokuwa tu kama atakuwa na haki ya kupiga kura iliyotajwa katika ibara ya 5 ya Katiba hii.

Ibara ndogo ya (4),
Kwa madhumuni ya ibara hii, "mwanajeshi" maana yake ni askari aliyeajiriwa kwa masharti ya muda au ya kudumu katika Jeshi la Ulinzi, Jeshi la Polisi, Jeshi la Magereza au Jeshi la Kujenga Taifa.

----------
 
Hapa ni ubabe tu.....Leo CCM wanashangilia lkn naamini sio siku nyingi tutaungana nao kulia....maana mtu aliyezoea ubabe ananogewa
 
Ukweli usiofichika huyujamaa nimwanajeshi coz August 14 /2016 alikua anazungumzi kuwa wanajeshi watapiga kura
 
Wwe ndo hujui taratibu sasa nikueleze pamoja na ujinga wako!!ukiacha sheria na katiba na nini sijui;rais ana mamlaka ambayo amepewa kikatiba kufanya unayoyaona!tatizo watz wengi hatujui sheria na elimu imetupita kushoto!isome katiba,mamlaka ya rais halafu ndo uje unitolee povu lako;Ndo maana alimtoa chagonja akambadilisha jeshi na kumpeleka fire,alimtoa mlowola polisi akampeleka takukuru,na hao wote walikuwa wako kazn halaf bado unahoji anakiuka tartibu zipi??
Kwahiyo amemteua Kanali Lubinga kuwa msemaji wa ccm kama rais au mwenyekiti wa ccm?
 
Ukamuulize na kinana alifikaje ccm wkt alikuwa mwanajeshi

Ukamuulize Kikwete alifikaje ccm wakat alikuwa mjesh

Ukamuulize na Lowasa alifikaje ccm wakat alikuw mjesh
Kinana na Kikwete waliachana na jeshi enzi za mfumo wa chama kimoja yaani chama kushika hatamu(party supremacy),je huo ndo mfumo uliopo sasa au unajitoa ufahamu tu? Swali ni kwamba, je, Col. Lubinga alistaafu?
 
- Nilidhani utai quote Katiba ya Chadema kuhusu Mwanachama mwenye sifa za kugombea urais kwani inasemaje kuhusu Mgombea mgeni ambaye hajamaliza hata miezi mitatu? hahahahaha kila mara nakuambia watoto wachanga kama wewe wapo wodi ya Mwaisela husikii why?

le Mutuz
Unamaanisha kosa la Chadema limehalalisha Magufuli kumteua Lubinga?
 
Turudin kwenye historia kwanza ndio tuhoj hya jmn mi sion cha ajab apo.
 
Back
Top Bottom