Msemaji wa JWTZ kuteuliwa kwenye NEC ya CCM, hii imekaaje?

Msemaji wa JWTZ kuteuliwa kwenye NEC ya CCM, hii imekaaje?

Katiba ya JMT inasemaje kuhusu mwanajeshi kujiunga na chama cha siasa?
Wanaruhusiwa baada ya kuacha jeshi.Yule keshaacha.Na kuacha haitajwi muda anaweza kuacha jeshi robo saa iliyopita ndani ya hiyo saa akateuliwa cheo cha kisiasa hata kama kaacha dakika moja iliyopita.
 
Wanasiasa wanaoweka matumaini yao katika Majeshi kama source ya nguvu zao ni kwa sababu hawajui ipasavyo falsafa za Majeshi, Jeshi huwa halina Urafiki na mtu, bali hutoa ushirikiano tu kwa mujibu wa kiapo!.
 
''...Nape alisema, wapili ni Kanali Ngemela Eslom Lubinga, kuwa Katibu NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa...''

Hapa mimi sijaelewa mteule ni mwanajeshi cheo cha kanali inakuwaje apewe dhamana ya kukiongozana chama wakati tunajua hawa waajiriwa wa wananchi hawatakiwi wawe wanachama wa chama cha kisiasa

SURA YA TISA
MAJESHI YA ULINZI

Ibara ya 147.

Ibara ndogo ya (3),
Itakuwa ni marufuku kwa mwanajeshi yeyote kujiunga na chama chohote cha siasa, isipokuwa tu kama atakuwa na haki ya kupiga kura iliyotajwa katika ibara ya 5 ya Katiba hii.
 
Kaanzia wapi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika mtaani kwake au baada ya kusikiliza vipindi vya redio uhuru?
Anaweza itwa njoo tukupe kadi ya CCM akasema nakuja mbio mwendo wa kunyakua wa kijeshi kuja kuchukua
 
nina harufu ya damu kutapakaa 2020 kwani kijani hawatakubali kushindwa, na zaidi itabidi njugu zisambazwe kwa raia wasio na hatia ili tu wabaki madarakani, tuandae makaburi, kwanza watapoteza pesa nyingi sana kuliko walizopoteza 2015, na watakuwa wako juu ya sheria, kama walinzi wetu nao wanaingizwa kwenye siasa, mark my words
 
Lowasa walipomchukua CHADEMA walimjua siku nyingi? Mbona aliingia tu na kupewa ugombea uraisi wakati hajawahi kuwa kiongozi wa tawi la chadema
Haina uhusiano, na kadri unavyolazimisha jambo hili katika mjadala huu unazidi tu kujifunua wewe ni mtu wa namna gani! Hoja iliyoko mbele ni muhimu hata kwa familia yako; kuna siku utaamini ukweli huu.
 
Wewe ni manunda, lowasa ni mwanajeshi wa wapi??

Ni sehemu ya wanajeshi wa CHADEMA mnawaita makamanda.Mtu aweza kuwa kamanda bila kuwa mwanajeshi?.Cheki wanajeshi wa CHADEMA yaani makamanda wakiwa wametinga miwani yao ya kuchomea vyuma

Mbeya3.jpg
 
Siku unayoteuliwa unaacha jeshi huwi mwanajeshi na unashika madaraka siku hiyo hiyo kama ambavyo lowasa alivyofanya.Siku alipoteuliwa na CHADEMA kuwa mgombea siku hiyo hiyo aliacha CCM na kuwa mgombea uraisi
Acha mambo ya kijinga, utateuliwa post ya kisiasa bila kuwa mwanachama?
 
Hiyo ni teuzi kama nyingine....yeye ni kama wewe utoke kwako uteuliwe kuwa mkuu wa majeshi.Piga kazi
 
Back
Top Bottom