Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sio lazima awe alikuwa mwanachama.Aweza kuwa kaanza jana hiyo hiyo kila kitu kina tarehe ya kuanza
Rudi kasome katiba vzr acha kupotosha ummaSiku unayoteuliwa unaacha jeshi huwi mwanajeshi na unashika madaraka siku hiyo hiyo kama ambavyo lowasa alivyofanya.Siku alipoteuliwa na CHADEMA kuwa mgombea siku hiyo hiyo aliacha CCM na kuwa mgombea uraisi
jadili hoja, wewe unaleta propaganda. Lowassa hapa wapi na wapi? RPC anastaafu leo kesho anachukua fomu kugombea nafasi ya siasa ndani ya CCM, alikuwa mwanachama tangu lini?Lowasa walipomchukua CHADEMA walimjua siku nyingi? Mbona aliingia tu na kupewa ugombea uraisi wakati hajawahi kuwa kiongozi wa tawi la chadema
Safi sana ndugu, umemjibu sawasawa mleta mada.Siku unayoteuliwa unaacha jeshi huwi mwanajeshi na unashika madaraka siku hiyo hiyo kama ambavyo lowasa alivyofanya.Siku alipoteuliwa na CHADEMA kuwa mgombea siku hiyo hiyo aliacha CCM na kuwa mgombea uraisi
Hiyo ni "argument" ya kitoto mno,serikali iliyojipambanua kuwa itateua makada wa Chama chake katika nafasi za uongozi ili waweze kutekeleza ilani ya uchaguzi,itaanzaje kumteua mtu ambaye hana historia ndani ya Chama kuwa kiongozi katika Chama?
Akishindwa kutekeleza ilani,misingi na kanuni za Chama utamwajibishaje?Teuzi hizi za wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama ndani ya Chama na serikali ni kielelezo cha namna vyombo hivyo vinavyotumika kisiasa kwa madhumuni ya kukibeba Chama tawala.Chama kilichopoteza mvuto,sasa kimeamua kujiegesha kwenye"kwapa" la vyombo ya usalama ili kipate nguvu za kijeshi.
Hivi huyo mteule ni ndiye yule aliyetuambia kuwa wamemchukua mwandishi aliyeripoti kuibiwa kwa kifaru cha jeshi na kwamba yupo kambini anasurubiwa ili akibahatika kutoka akawahadithie wenzake?"
Tukifikia mahali tikaamua kuiweka kando katiba yetu na katiba ya vyombo vyetu vya ulinzi,tukaanza kuajili na kuteua "wababe wa kivita" katika sehemu nyeti za uongozi wa Chama na serikali,taratibu tunaanza kuliondoa Taifa letu kwenye demokrasia tunayoihubiri.
Kina Nkurunzinza walioamua kung'ang'ania madaraka kwa kujiongezea mihula ya uongozi kinyume na katiba,walifanya hivyo baada ya kuona wana uungwaji mkono wa "jeshi lililoiasi katiba".Uasi huu wa katiba ufanywao na vyombo vyetu unamaana gani kama si maandalizi ya watu kuja kung'ang'ania madarakani huko tuendako?Au haya ndiyo yanayopelekea hadi jf ambayo ndiyo platform pekee iliyobaki tutumiayo kuihoji serikali baada ya magazeti,redio na TV kusalimu amri mbele ya dola na sasa wanaanza kumuwinda mkurugenzi wetu wa jf?
Tuendako ni Mungu tu ajuwaye,Yeye ndiye mweye uwezo wa kuichunguza mioyo yetu,Mungu wa Mbinguni Atuepushe na hili,amen.
huoni aibu ndg yangu???mbona unajibu ujinga?ungekua kimya yehodaya .Sio lazima awe alikuwa mwanachama.Aweza kuwa kaanza jana hiyo hiyo kila kitu kina tarehe ya kuanza
Nimegundua si kosa lako, tatizo lako unataka kuonyesha wana JF kuwa unajua lakini hujui chochote. Acha tukukumbushe-wakati tukiwa na chama kimoja asilmia kubwa ya wafanya kazi wote na wafanyabiashara walikuwa wanachama wa ccm, majeshi yote walikuwa wanachama wa ccm na siasa ilifundishwa hadi majeshini, na ndo maana tokea nyakati hizo wanajeshi waliteuliwa katika nyadhifa mbalimbali mfano-Mh. Jakaya Kikwete, Mh.Kinana na wengine wengi-si ajabu hicho kinachofanyika
Hujajibu swali bado. Hoja kuu ni kwamba je alikuwa mwanachama wa CCM wakati angali mwanajeshi? La sivyo isingepatikaka base ya kumteua kwasababu kuwa mwanachama wa CCM ndio base kuu ya kuchaguliwa au kuteuliwa kwenye nafasi mbalimbali za kichama.Siku unayoteuliwa unaacha jeshi huwi mwanajeshi na unashika madaraka siku hiyo hiyo kama ambavyo lowasa alivyofanya.Siku alipoteuliwa na CHADEMA kuwa mgombea siku hiyo hiyo aliacha CCM na kuwa mgombea uraisi
Usilete habari ya Zambia hapa angalia kwanza katiba yetu inasemaje kuhusu wanajeshi kushiriki siasaZambia kiongozi wa chama cha upinzani ni Brigadier General Godfrey Miyanda.Wanajeshi kwenye siasa mbona kawaida tu
Hujajibu swali bado. Hoja kuu ni kwamba je alikuwa mwanachama wa CCM wakati angali mwanajeshi? La sivyo isingepatikaka base ya kumteua kwasababu kuwa mwanachama wa CCM ndio base kuu ya kuchaguliwa au kuteuliwa kwenye nafasi mbalimbali za kichama.
Mkuu, unaweza ukawa na hoja lakini unasahau ukweli kwamba ndani ya CCM kuna wanajeshi.
1. Luteni kanali Abdulrahman Kinana
2. Kapteni George Mkuchika
3. Luteni Kanali Jakaya Kikwete
4. Kapteni John Zefania Chiligati
Na wengine wengi tu, sembuse huyu kanali Lubinga?
Kanali Lubinga alitoka jeshini akaenda kuwa DC Mlele Mkoani Katavi na baadae jeshi likamhitaji kuwa mkurugenzi wake wa habari na mahusiano (eneo ambalo ana utaalam nalo).
Hawa ni watu ambao ambao unaweza kusema kwamba wanacheza mpira kama "box to box midfielders" na ndicho kilichomsukuma JPM kumteua kuziba nafasi ya mama Migiro khasa lugha ya mawasiliano jamaa ametulia.
Umesikia tamko au yeye mwenye kuacha uanajeshi?Katiba inasema mwanajeshi haruhusiwi.Ina maana nikiacha hata dakika hii,dakika ya pili inayofuata mimi sio mwanajeshi naweza chukua kadi ya chama chochote cha siasa na nikateuliwa kushika cheo chochote cha kisiasa na hakuna katiba iliyovunjwa.Swala la kuwa sina uzoefu kwenye chama huo ni umbeya.Wao walionipa cheo kama wananiamini tatizo liko wapi.Katiba haijavunjwa na hao wamenipa cheo kwa mapenzi yao hamna shida.
duuuuuuuh......na mtemi kapitaNI UKIUKWAJI WA KATIBA AU MAJINA YAMEFANANA KATI YA MSEMAJI WA JWTZ NA HUYU MTEULE WA NEC YA CCM?
JPM JITOKEZE KUUELEZEA UMMA KUHUSU UTATA HUU.
Msemaji wa JWTZ ni Kanali Ngemela Lubinga.
Katibu Mteule wa NEC ya CCM Siasa na Uhusiano wa Kimataifa ni Kanali Ngemela Eslom Lubinga.
Katiba ya Jamhuri 1977 inasema :-
SURA YA TISA
MAJESHI YA ULINZI
Ibara ya 147.
Ibara ndogo ya (3),
Itakuwa ni marufuku kwa mwanajeshi yeyote kujiunga na chama chohote cha siasa, isipokuwa tu kama atakuwa na haki ya kupiga kura iliyotajwa katika ibara ya 5 ya Katiba hii.
Ibara ndogo ya (4),
Kwa madhumuni ya ibara hii, "mwanajeshi" maana yake ni askari aliyeajiriwa kwa masharti ya muda au ya kudumu katika Jeshi la Ulinzi, Jeshi la Polisi, Jeshi la Magereza au Jeshi la Kujenga Taifa.