Msemaji wa JWTZ kuteuliwa kwenye NEC ya CCM, hii imekaaje?

Tukubali hoja kuwa mteule ameacha kuwatumikia wananchi,ila nina maswali.

1; nini sababu ya kuacha jeshi,je ni umri au ni ili ateuliwe kuwa na cheo kwenye chama cha siasa.
2;kama ameacha jeshi ili apewe cheo cha chama cha siasa ambapo ataanza kuwa mwanachama mpya, je kazi zetu atafanya nani(tufanye alikuwa mtendaji mzuri wa jeshi)
3;Je zilikuwa ni hekima kumteua kanali wa jeshi kama mwanachama mpya na kupewa wadhifa kukitumikia chama cha siasa.
 
Hoja si uteuzi wake tu,alianza lini kuwa mwanachama wa Chama cha mapinduzi huku akiwa mwanajeshi?
Nimegundua si kosa lako, tatizo lako unataka kuonyesha wana JF kuwa unajua lakini hujui chochote. Acha tukukumbushe-wakati tukiwa na chama kimoja asilmia kubwa ya wafanya kazi wote na wafanyabiashara walikuwa wanachama wa ccm, majeshi yote walikuwa wanachama wa ccm na siasa ilifundishwa hadi majeshini, na ndo maana tokea nyakati hizo wanajeshi waliteuliwa katika nyadhifa mbalimbali mfano-Mh. Jakaya Kikwete, Mh.Kinana na wengine wengi-si ajabu hicho kinachofanyika
 
Kwa utawala usiofuata misingi ya sheria hili linawezekana kabisa...
 
Mkuu anaweza kustaafu jeshini kisha akaendelea na siasa. Mnaogopa ukatili hautaepukika mkileta mambo ya ajabu? Hahaaa😛😛
 
labda kastaafu, kama alivyokuwa kinana, kikwete, makamba, chiku galawa, akina maganga kule kigoma, labda waseme kanali mstaafu!!! maana kama atasemea CCM akiwa na magwanda sidhani ni hivyo, sema ukishakuwa mjeshi na cheo chako basi utabakia na rank yako hata ustaafu!!
 
Siku unayoteuliwa unaacha jeshi huwi mwanajeshi na unashika madaraka siku hiyo hiyo kama ambavyo lowasa alivyofanya.Siku alipoteuliwa na CHADEMA kuwa mgombea siku hiyo hiyo aliacha CCM na kuwa mgombea uraisi
Kuna wakati hata kama mtu unampenda kiasi gani, akikosea msahihishe....

Mwenzio kaweka kifungu cha katiba kukisapoti anachosena, NA WEWE WEKA ILI UELEWEKE

Kuna watu alipotaka kuwateua kuwa mawaziri, aliwateuwa kwanza kuwa wabunge... sasa kama ni kweli mwanajeshi kateuliwa, angemvua kwanza uanajeshi..
 
Hii ni aina ya mfumo anaotumia kagame kutaka kuitawala Rwanda milele. Hebu angalia waliomo kwenye RPF ni akina nani
 
Mwenzio kaweka kifungu cha katiba kukisapoti anachosena, NA WEWE WEKA ILI UELEWEKE

Katiba inasema mwanajeshi haruhusiwi.Ina maana nikiacha hata dakika hii,dakika ya pili inayofuata mimi sio mwanajeshi naweza chukua kadi ya chama chochote cha siasa na nikateuliwa kushika cheo chochote cha kisiasa na hakuna katiba iliyovunjwa.Swala la kuwa sina uzoefu kwenye chama huo ni umbeya.Wao walionipa cheo kama wananiamini tatizo liko wapi.Katiba haijavunjwa na hao wamenipa cheo kwa mapenzi yao hamna shida.
 

Mbona huulizi ilikuwaje JK akamteua Kanali Lubinga kuwa DC wa wilaya ya Mlele huko nyuma?

Unafahamu nini kuhusu kanali Lubinga?

Tatizo linaendelea kuwa lilelile la habari nusunusu za waandishi wa Tanzania na kila mmmoja wao amefanya "copy and pasting", kwenye kila gazeti wote wakimnukuu Nnauye.

Hakuna mwandishi hata mmoja alietafuta historia ya kanali Lubinga ili awafahamishe watu kama wewe.
 
Kama ni kweli huyo ni mtu mmoja basi hiyo inamaanisha watumishi wengi ndoto zao ni kujiunga na siasa, pengine ana ndoto za kuwatumikia wananchi kwahiyo safari yake ndiyo inaanza au la siasa inalipa sana na kila mtu anapigania malisho ya majani mabichi.
 
Trend ya Magufuli na wanajeshi inaashiria maandalizi fulani. Huwezi kujua kwa hakika ni nini ila sio mambo mema.

Vijana wa ccm wanaoshabikia haya huku wakiwa na ndoto za kufanya siasa ndani ya demokrasia wajitafakari sana.

Tyrant Regime inatengenezwa.
 
Siku unayoteuliwa unaacha jeshi huwi mwanajeshi na unashika madaraka siku hiyo hiyo kama ambavyo lowasa alivyofanya.Siku alipoteuliwa na CHADEMA kuwa mgombea siku hiyo hiyo aliacha CCM na kuwa mgombea uraisi
Halafu hapo hapo unapewa Kadi ya CCM?
Hii haina tofauti na saga ya Dk Tulia Akson na Jaji Ramadhani.
 
Ccm watakoma wameanza kuletewa wanajeshi lumumba.......na hao jamaa tatizo ukiwapa cheo basi kuja kuwatoa ni issue.

Greenguard wacha waendelee kulinda mageti.
 
Kwani katiba ya Chadema inasemaje, mwanachama mpya lazima amalize miaka 2, bila kupewa wadhiwa wowote, lakini lowasa aliingia asubuhi jioni mgombea urais mbona hili hamkuhoji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…