Msemaji wa JWTZ kuteuliwa kwenye NEC ya CCM, hii imekaaje?

Msemaji wa JWTZ kuteuliwa kwenye NEC ya CCM, hii imekaaje?

Joined
Sep 29, 2016
Posts
34
Reaction score
84
NI UKIUKWAJI WA KATIBA AU MAJINA YAMEFANANA KATI YA MSEMAJI WA JWTZ NA HUYU MTEULE WA NEC YA CCM?
JPM JITOKEZE KUUELEZEA UMMA KUHUSU UTATA HUU.​

Msemaji wa JWTZ ni Kanali Ngemela Lubinga.

Katibu Mteule wa NEC ya CCM Siasa na Uhusiano wa Kimataifa ni Kanali Ngemela Eslom Lubinga.

Katiba ya Jamhuri 1977 inasema :-

SURA YA TISA
MAJESHI YA ULINZI

Ibara ya 147.

Ibara ndogo ya (3),
Itakuwa ni marufuku kwa mwanajeshi yeyote kujiunga na chama chohote cha siasa, isipokuwa tu kama atakuwa na haki ya kupiga kura iliyotajwa katika ibara ya 5 ya Katiba hii.

Ibara ndogo ya (4),
Kwa madhumuni ya ibara hii, "mwanajeshi" maana yake ni askari aliyeajiriwa kwa masharti ya muda au ya kudumu katika Jeshi la Ulinzi, Jeshi la Polisi, Jeshi la Magereza au Jeshi la Kujenga Taifa.

----------
Kumekuwa na mitazamo mingi, thread nyingi zikisifisia na zingine zikihoji uhalali wa CCM kumteua Kanali wa Jeshi kuwa Mtumishi wa chama, Namimi nimeona nitoe maoni yangu kuhusu jambo hili ikienda sambamba na utoaji wa ufafanuzi wa baadhi ya mambo…..

HISTORIA YA JESHI LA JWTZ

Baada ya Uhuru, 1961, Tanganyika ilirithi jeshi la kikoloni la Uingereza lilojulikana kama Kings African Rifles ingawa Tanganyika ilibadili jina la Jeshi hilo na kuwa Tangayika Rifles (TR). Pamoja na kubadilika jina Tanganyika Rifles ilikuwa na muundo sawa na Kings African Rifles (KAR). Maafisa wenye mamlaka bado walikuwa Waingereza, pamoja na Waafrika watano waliopandishwa cheo wakati wa uhuru na kupokea mafunzo katika vyuo vya kijeshi vya Kiingereza. Afisa mkuu alikuwa Brigedia Jenerali Patrick Sholto Douglas.

UASI WA TANGANYIKA RIFLES (TR)

Tarehe 20 Januari 1964, wakati wa usiku, kikosi cha kwanza cha TR kwenye kambi la Colito Barracks mjini Dar es Salaam kiliasi na kujipatia silaha kutoka kwenye ghala la jeshi. Maafisa Waingereza walikamatwa na kufungwa lakini mkuu Douglas aliweza kujificha. Waasi walivamia kituo cha redio, uwanja wa ndege, ikulu na ofisi ya posta na simu. Maafisa Waingereza na Waafrika wasioshiriki na waasi walisafirishwa nchini Kenya. Rais Nyerere alienda mafichoni katika kanisa moja la kikatoliki ng'ambo ya bandari(kigamboni) akamwachia waziri Oskar Kambona kazi ya kuwasiliana na wanajeshi.

Madai ya wanajeshi yalikuwa kuachishwa kwa maafisa Waingereza na kupandishwa kwa mishahara. Siku za kwanza ya mgomo wa jeshi ilifuatwa na vipindi vya fujo mjini vilivyobadilika na vipindi vya kimya, mashambulizi dhidi ya maduka ya Wahindi na kukamatwa kwa Wazungu wachache. Hata mbalozi wa Uingereza alikamatwa kwa kipindi kifupi.

Tarehe 24 Januari serikali ya Tanzania iliomba rasmi Uingereza kuingia kati na kuzimisha uasi. Asubuhi ya 25 Januari kikosi kidogo cha wanajeshi wa Kiingereza waliondoka kwenye meli iliyokwepo karibu na Dar es Salaam kwa njia ya helikopta. Walivamia kambi la Colito barracks na jenerali Douglas alidai kwa kipazia sauti wanajeshi wajisalimishe. Mwanzoni walikataa lakini baada ya mashambulio mafupi walio wengi walijisalimisha wengine wakakimbia. Viongozi walikamatwa, na pia askari wa Dodoma na Nachingwea waliowahi kujiunga na uasi walijisalimisha bila upinzani kwa askari Waingereza wachache.

Wakazi wengine wa Daressalaam walikuwa na hofu ya kwamba Uingereza ulikuwa umerudi ili kurudisha ukoloni lakini baada ya kusita masaa machache Nyerere alieleza kwa njia ya redio ya kwamba kuingilia kwa Uingereza ulifuata ombi la serikali yake. Askari Waingereza waliondoka kwenye Aprili 1964 na nafasi yao ilichukuliwa na kikosi kutoka Nigeria iliyofika kwa niaba ya Umoja wa Afrika kufuatana na ombi la serikali ya Tanganyika


UUNDWAJI WA JESHI JIPYA

Jeshi jipya lilijengwa kwa kuajiri hasa wanachama wa Umoja Wa Vijana wa TANU. Jeshi hili jipya liliwekwa chini ya usimamizi ya chama cha TANU (baadaye CCM) kwa kufuata mtindo wa nchi kama Urusi na China. Kamanda wa kwanza alikuwa Mrisho Sarakikya aliyewahi kusimama upande wa serikali wakati wa uasi akapandishwa cheo kutoka luteni hadi kanali, baadaye kuwa jenerali. Na hapo ndipo Jeshi likabadilishwa jina toka Tanganyika Rifles (TR) na kuwa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ),September, 1964.

MSIMAMO WA KATIBA JUU YA WANAJESHI NA VYAMA VYA SIASA

Kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1977) ibara ya 147(3) imeweka marufuku kwa mwanajeshi yeyote kujiunga na chama chohote cha siasa na imempa haki ya kupiga kura, hii inafuatia mabadiliko ya katiba yaliyofanywa mwaka 1992 chini ya sheria ya 1992 Na.4 ib. 36.



COL. NGEMELA ESLOM LUBINGA NI NANI??

Kwasasa Col Ngemela Eslom Lubinga ni Katibu mteule wa NEC Siasa na Uhusiano wa kimataifa( CCM). Col Ngemela alishawahi kuteuliwa na Rais Mstaafu Jakaya Kikwete kuwa mkuu wa wilaya ya Mlele mara baada ya kustaafu utumishi wake katika Jeshi la JWTZ. Ngemela aliachwa kwenye orodha ya Madc waliotangazwa February 19, 2015, Baadae akarudi jeshini kwa mkataba wa mwaka mmoja ulioisha November, 2016.


VITU VYA KUZINGATIA

· Ngemela alijiunga na jeshi la JWTZ kabla ya 1992

· Ngemela alistaafu jeshi kabla ya 2015

· Ngemela alshawahi kuhudumu kama mkuu wa wilaya ya Mlele mara baada ya kustaafu kuwa mtumishi wa Jeshi.
 
Mtukufu wetu yuko juu ya kila kitu na hata akiamua kusema watz wote ni vilaza tutampigia makofi na kushangilia
Siku unayoteuliwa unaacha jeshi huwi mwanajeshi na unashika madaraka siku hiyo hiyo kama ambavyo lowasa alivyofanya.Siku alipoteuliwa na CHADEMA kuwa mgombea siku hiyo hiyo aliacha CCM na kuwa mgombea uraisi
 
Siku unayoteuliwa unaacha jeshi huwi mwanajeshi na unashika madaraka siku hiyo hiyo kama ambavyo lowasa alivyofanya.Siku alipoteuliwa na CHADEMA kuwa mgombea siku hiyo hiyo aliacha CCM na kuwa mgombea uraisi



Hoja si uteuzi wake tu,alianza lini kuwa mwanachama wa Chama cha mapinduzi huku akiwa mwanajeshi?
 
Siku unayoteuliwa unaacha jeshi huwi mwanajeshi na unashika madaraka siku hiyo hiyo kama ambavyo lowasa alivyofanya.Siku alipoteuliwa na CHADEMA kuwa mgombea siku hiyo hiyo aliacha CCM na kuwa mgombea uraisi
Swali ni kuhusu uteuzi bro, kwa sababu mtu hawezi kuteuliwa tena kwenye nafasi kama ya msemaji kama sio mwanachama wa muda mrefu
 
Siku unayoteuliwa unaacha jeshi huwi mwanajeshi na unashika madaraka siku hiyo hiyo kama ambavyo lowasa alivyofanya.Siku alipoteuliwa na CHADEMA kuwa mgombea siku hiyo hiyo aliacha CCM na kuwa mgombea uraisi
kama kaacha,mbona haitwi "mstaafu" au atumie jina lisilo na asili ya jeshI,atumie majina yake tu?

halafu hii ya kurundika wanajeshi,je ikitokea ccm imeshindwa kwenye uchaguzi,hawa wanajeshi wataelewa? au wanachonganishwa na wananchi?
 
Siku unayoteuliwa unaacha jeshi huwi mwanajeshi na unashika madaraka siku hiyo hiyo kama ambavyo lowasa alivyofanya.Siku alipoteuliwa na CHADEMA kuwa mgombea siku hiyo hiyo aliacha CCM na kuwa mgombea uraisi
Sawa lkn hii ni picha kuwa wakati alipokua jeshini alikua ni mwanachama wa ccm. Haiwezekani kuwa wamemchukua MTU wasiomjua. Ndio maana tunasema vyombo vyetu vya usalama sio huruma na haviko tayari kuona ccm ikishindwa ndio maana hutumia mbinu yote hata za wizi kuleta ushindi kwa ccm
 
Sawa lkn hii ni picha kuwa wakati alipokua jeshini alikua ni mwanachama wa ccm. Haiwezekani kuwa wamemchukua MTU wasiomjua. Ndio maana tunasema vyombo vyetu vya usalama sio huruma na haviko tayari kuona ccm ikishindwa ndio maana hutumia mbinu yote hata za wizi kuleta ushindi kwa ccm
Lowasa walipomchukua CHADEMA walimjua siku nyingi? Mbona aliingia tu na kupewa ugombea uraisi wakati hajawahi kuwa kiongozi wa tawi la chadema
 
Trend ya Magufuli na wanajeshi inaashiria maandalizi fulani. Huwezi kujua kwa hakika ni nini ila sio mambo mema.

Vijana wa ccm wanaoshabikia haya huku wakiwa na ndoto za kufanya siasa ndani ya demokrasia wajitafakari sana.
 
Back
Top Bottom