tonicimmobility
JF-Expert Member
- Jun 17, 2025
- 493
- 1,040
Msemaji Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, DCP David Misime, amesema jeshi hilo limekuwa na utaratibu wa kujiweka tayari kila Uchaguzi Mkuu unapokaribia, huku likiwajengea uwezo askari wake kuhakikisha nchi inabaki salama.
DCP Misime ameyasema hayo leo Julai 30, 2025, jijini Dodoma, wakati wa mdahalo wa kitaifa wa kuimarisha amani na umoja wa kitaifa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2025.
Amesema askari wamekuwa wakipatiwa mafunzo ya kusimamia amani kila mara ya uchaguzi na wakati wote, wakipata mafunzo hayo kutoka vyuo vya ndani na nje ya nchi kwa kuzingatia mikataba ya kimataifa.
Soma pia: Sheikh Akilimali: Tudumishe amani na utulivu kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Hata hivyo, DCP Misime alisisitiza kuwa jeshi hilo halitakuwa tayari kuvumilia mtu yeyote au kikundi chochote kitakachojaribu kuvuruga au kuharibu amani ya nchi.
"Kila mtu akiamka asubuhi nyumbani kwake anatakiwa kufikiria namna ya kutunza na kulinda amani ya nchi kwanza ili tuweze kuwa na maendeleo," amesema.
Source: Nipashe