Msemaji wa Serikali akiri ndege mpya ya Bombardier Q 400-Dash 8 kushikiliwa nchini Canada. Awatupia lawama wanasiasa...

Mkuu Marekani, UK wamemuua Saddam Hussein na Gaddafi kwa sababu za uongo na za kutunga.
Kuna raia wao yupi kaenda kuwashitaki popote pale!
 
Mkuu Marekani, UK wamemuua Saddam Hussein na Gaddafi kwa sababu za uongo na za kutunga.
Kuna raia wao yupi kaenda kuwashitaki popote pale!
Sababu za Uongo umezisikia kwa baadhi ya raia wa US, ambao hawakukubaliana na sababu za nchi yao kuivamia Iraq. Pia Trump anashitakiwa katika baadhi ya maamuzi yake, na huo ndio utawala wa sheria.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakati mnaingia hiyo mikataba ya kipumbavu,LISU aliwashauri kabisa kuwa hiyo mikataba ni hasara kubwa kwa taifa, Nyie mkajifanya wajuaji mkamuita Lisu kuwa ni mpinga maendeleo.Leo yamewatokea puani mnataka awasaidie!!!!?.Maajabu ya karne hayo.Mnapenda kuingia na kuvunja mikataba ila matokeo ya kazi yenu hiyo hampendi wananchi wajue????.
 

Kuwa mzalendo ni kweli ni kuwa upande wa nchi yako lakini sio lazima kuwa upande wa Rais kama yeye mwenyewe hana huo uzalendo kwa nchi yake! Rais angekuwa mzalendo angepambana na waliosababisha tupigwe faini, na waliochelewesha kulipa faini mpaka deni likaongezeka zaidi ya mara dufu, na sio kukimbizana na aliye waamsha wananchi kujua kuwa kodi zao zitaenda kulipa madeni yaliosababishwa na watu walioaminiwa na kupewa dhamana ya kutumikia nyadhifa kubwa nchini!

Sikia wenzio wakitafsiri maana halisi ya uzalendo/patriotism:

 
Mnachotaka kusikia ni serikali kusifiwa, hivi LISU kashangilia uankatoa taarifa na kuonya juu ya kuvunja mikataba bila kufuata sheria? Kwani mnapoingia mikataba mibovu hamjui madhara yake hata pale mnapotaka kuivunja kiholela?
Hao waliowekwa kizuizini kipindi cha mwalimu ilisaidia nini kuondoa umasikini ulioanzia kipindi hicho?
 

Kwanza mlijaribu kujenga hoja za kupotosha, lakini ukweli wa Lissu umezidi kushika kasi. Hapa mlipofikia ndio mnataka kulazimisha hoja zenu zikubalike. Wekeni mikaba wazi kwani mliingia kwa nia mbaya hamtaki mmebaki kuimbisha watu uzalendo uchwara. Haya matitizo yote mmeyasababisha nyie, kisha mnajifanya kuruka kwa kumsingizia Lissu mkidhani sisi wananchi ni wajinga. Wabaya wetu kwenye nchi hii ni nyie ccm na sio Lissu. Yeye Lissu anatuamsha tu tuliolala tusiuziiwe uzalendo fake.
 
Lissu ni hero aliyesalia wa nchi hii, na wanaomwelewa si wengine bali wenye uzima wa akili. Ambao akili zimekufa hazina uhai, hawawezi kumwekewa Lissu
 
Siku mtoto/mama/baba yako akikushitaki popote pale kwa kutolipa kodi utaelewa!
Nchi haiendeshwi kifamilia, inaendeshwa kwa misingi ya sheria. Usimfananishe baba na rais, Rais hajajipeleka pale kachaguliwa kwa mujibu wa katiba na sheria.
 
kivipi mkuu, si huwa mnasema msema kweli ni mpenzi wa Mungu, sasa kasema ukweli mnasema msaliti, sasa huyo mpenzi wa Mungu mnaotangazia umma ni Mungu gani au ni miungu
 
Sote hatuelew chochote kuhusu hili, uwe upande wa nchi au kule kwingne sisi hatuangalii huko.mzalendo haswaa haangalii chama wala kabla naweza kuwa kaongea ukweli ndio but upo wapi uzalendo wake katka Nchi.see Waliosain hiyo mkataba Wenda wakafa leo je kzazi kitakachosimama juu vyeo vyao watafanya nini zaidi kufanya kama ilivyo sasa.pia ataogopwa kushitakiwaa.fact, kama huo upende ungepata mamlaka wangefanya nini tofauti na kuivunja na kusimamia nchi yake na watu wake.Nonsense, kusoma ila hatutumii hata robo ya elimu yako kuleta mafanikio katika nchi.QN Elimu ndivyo inavyotumika kuongelea madhaifu ya watu wadogo dhidi ya taifa nzima?. Amkeni siasi si nzuri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
WE ZEZETA KUSEMA UKWELI NDIO KUSHABIKIA? MMEZOEA KUAMBIWA UONGO KILA KUKICHA
 
Haya malalamiko yamekosa mwelekeo..

Wapinzani walishatoa ushauri bungeni wa kila aina mnataka leo nani awahabarishe wananchi? au mnataka mtuambie tu kukua kwa deni la taifa?
 

Nadhani waliyoingiza nchi kwenye matatizo ndiyo wakulaumiwa siyo anayetuelimisha watanzania nini kinachoendelea.

Pole kwe wengine wanayoipenda sana Tanzania huru tunampongeza Lissu kwa kutueleza ukweli japo hakika unauma.Alipoanza kuvunja mikataba Lissu aliwaonya wakamuona kwa vile mpinzani ana wivu wa kike,leo yametukuta tunamlaumu mnataka Lissu awasaidiaje enyi Chama Cha Majangili??

Wanaofanya upumbavu wa kulivuna Taifa letu na raslimali zake hamtaki waguswe ila wanaokemea ndiyo wenye hatia,lazima tupimwe akili zetu.

Haya ni maneno ya JKN kwenye kitabu chake Uhuru na Maendeleo:


Kama lengo la maendeleo ni uhuru kamili ya wananchi, basi haiwezi kuwa matokeo ya kutumia nguvu" Mwl Nyerere 'Uhuru na Maendeleo' 1968
 
Siding with Tanzanias enemy for whatever reason, makes one a target.

Lissu must be lynched!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…