Msemaji wa Serikali akiri ndege mpya ya Bombardier Q 400-Dash 8 kushikiliwa nchini Canada. Awatupia lawama wanasiasa...

Msemaji wa Serikali akiri ndege mpya ya Bombardier Q 400-Dash 8 kushikiliwa nchini Canada. Awatupia lawama wanasiasa...

Hili la sasa ndio limewaonyesha ni watu wa aina gani yaani wanamuogopa aliyeitia hasara kumpa lawama na kumwajibisha wanalaumu upinzani wakati wanasahau kuwa waliapa kuulinda katiba na siyo mtu
 
Binafsi naomba niwe muwazi tu kwa hili naona kuna mchezo mchafu unafanyika sema aimjui anayeufanya.
Hiyo tenda ilikuwa mwaka 2010 na kuporwa mawka 2013.
Mkataba wa kunua ndege umefanyika mwaka 2016.
Kampuni iliyoporwa tenda inahusika na ujenzi wa barabara.
Kampuni inayouza ndege kwa Tanzania ni kiwanda cha kutengeneza ndege.
Sasa maswali yangu ni haya.
1.unaruhusu vipi bidhaa uliyoagizwa na kulipwa gharama zote itumike kulipa deni la mtu mwingine kabla bidhaa hiyo haijamfikia mnunuzi?
Kama serikali imeingia mkataba na Bombardier inakuwaje Bombadier waruhusu mzigo uzuiliwe na mtu ambaye sio mteja wao?
Hiyo kampuni ya ujenzi iliingia mkataba na serikali ya Tanzania au na kampuni ya Bombardier?
Nadhani kuna kitu hakipo sawa hapa.
Nadhani inategemea na mahali ilipokuwa na ilikuwa chini ya umiliki wa nani. Kama tulishakabidhiwa wanatudaka.
 
Nyie watanzania yani baba yako akinyanganywa shamba ama nyumba kisa anadaiwa watoto mtafurahia. Kizazi cha nyoka hiki-wicked society.

Je hamjui ya kwamba hizo pesa mtazilipa ninyi wana nchi kwa kupitia kodi zaidi? Je hamjui ninyi ndo mtaathirika zaidi na mfumko wa bei kwasababu dola zaenda nje? Mnafikiri serikali ama waziri ama rais ataathirika kwa lolote? Watu hawa wanaangamia kwa kukosa maarifa, iliwapasa kuhuzunika na kusikitika.


Mbona mlifurahia Sumaye kunyang'anywa shamba? acha upuuzi
 
Hata kama mtu unampenda vipi kama anakasoro utazificha kwa muda tu!

Hakuna serikali duniani isiyodaiwa! Na sidhani kama serikali ingekubali ndege yake itaifishwe kwa deni hilo

Hoja ya Msingi hapa ni pale Tundu Lisu anapoonekana mbele ya kamera kila kunapokuwa na swala linalohusiana na Canada na mara zote yuko upande wao!

Maswala ya madeni yana namna yake ya kushughulikiwa! Sina hakika kama siku zote hiyo kampuni inayotudai ilisubiri tuagize ndege ndio waanze kutudai!

Naamini kuna namna walivyokubaliana kuwa endapo tutashindwa kulipa nini kifanyike! Kwa hiyo wenye kupenyeza penyeza hoja za ushawishi wa wanasiasa kwa jambo hili wana weza kufanikiwa kublind baadhi ya wananchi hata kama sio kweli!

Kulikuwa na haja gani ya Tundu Lisu kuja haraka kiasi hicho mbele ya kamera kueleza alichokieleza!?

Je, ni kweli serikali ilikuwa haina mpango wowote wa kufuatilia hiyo ndege hadi lilipoibuliwa na Lisu !? Kwamba asingelianzisha ndege tungeikosa!?
Na kama mpango ulikuwepo, mbona hakuueleza!?

Sent using Jamii Forums mobile app
Tundu Lissu ni mwanasheria na kama mwanasheria, anaruhusiwa - kwa kweli anatakiwa- kumpa mtu yeyote haki ya kutetewa na wanasheria. Ndiyo maana hata wezi na wauaji huwa wanatetewa na wanasheria.

Hiyo ni kazi ya wanasheria.

Ni sehemu ya utawala wa sheria.

Marekani huwashitaki watu kwa ugaidi, halafu watu hao wanaoshitakiwa kwa ugaidi hutetewa na wanasheria wa Marekani wanaoheshimika sana.

Hilo linaonyesha ukomavu wa mfumo wa sheria wa Marekani.

Actually hata Saddam Hussein katika kesi yake alikuwa na mwanasheria mmoja Mmarekani.

Kwa hiyo, Tundu Lissu hata leo akiamua kuwa wakili wa Acacia katika kesi Acacia na Tanzania, mimi kwa kuwa naelewa utawala wa sheria unafanya kazi vipi na haki ya kuwakilishwa na mwanasheria ikoje, sitakuwa na kinyongo.

In fact, Acacia wakiwakilishwa na mwanasheria anayesemwa kuwa mahiri kama Tundu Lissu, halafu wakashindwa, hapo serikali itajigamba kwamba imeshinda kesi bila kuinyima Acacia haki ya kuwakilishwa na mwanasheria mahiri kama Tundu Lissu.

Kwa hiyo tuachane na Tundu Lissu. Yeye ni mwanasheria. Hata akimtetea muuaji, ni kazi yake. Marehemu Johnnie Cochran alikuwa wakili anayeheshimika. Alimtetea O.J Simpson mpaka O.J akashinda. O.J kuna watu kibao wanasema mpaka leo kaua. Lakini Johnnie Cichran kajizidishia heshima kushinda kesi kwa sababu watu weusi wameona ametoa mfano jinsi gani mfumo wa sheria unavyoweza kumpa nafasi mtu mweusi mwenye mwanasheria mzuri kushinda kesi mbaya sana ya mauaji.

Kwa hiyo Tundu Lissu hata akiamua kuwa wakili wa hao wa Canada mimi nitamshukuru kwanza kabisa kwa kuonyesha kwamba Tanzania si nchi ya kijima kwamba ukiwa na kesi na serikali mawakili wote wa Kitanzania watakususa. Huo utakuwa ni ushamba.

Kama umeona movie ya "Amistad" ambayo imetokana na habari ya kweli, utaona mtu anaitwa John Quincy Adams. Hiyu alikuwa rais wa zamani wa US ambaye baba yake (John Adams) alikuwa rais wa pili wa Marekani.

John Quincy Adams, licha ya kuwa rais wa Marekani wa zamani, aliichukua kesi kuwatetea watumwa wa Kiafrika walioua nahodha wa meli iliyowachukua kutoka Sierra Leone West Africa. Meli ilichukuliwa mpaka Connecticut baada ya dhoruba na wale weusi ambao walishikwa kuuzwa utumwani wakafungwa. John Quincy Adams akachukua kesi ike akiwatetea watumwa dhidi ya serikali ya Marekani.

Ni sawa na Mwinyi leo awe mwanasheria wa Acacia.

Lakini kati ya vitu ambavyo John Quincy Adams anaheshimiwa kwavyo mpaka leo, ni kuchukua kesi hii.

Kwa sababu alionyesha kwamba hata ukiwa mtumwa, kuna Wamarekani watakaotaka kutumia mfumo wao wa sheria kukutetea.

Tumuache Tundu Lissu awe mwanasheria. Kwa sababu kazi yake inamruhusu kumtetea hata muuaji.

Mimi nataka kuijadili serikali na ilivyoboronga.

Zaidi kuhusu Amistad soma hapa.

John Quincy Adams and the Amistad case, 1841 | The Gilder Lehrman Institute of American History




Sent from my Kimulimuli
 
Mbona mlifurahia Sumaye kunyang'anywa shamba? acha upuuzi

Ndiyo akili yako hiyo. Nakwambia utayeumiia ni wewe. Unajidunga mshale unafurahia. Ha ha ha ha
Serikali watachofanya ni kubana kodi wananchi walipe ili walipe hilo deni. Na bado unafurahia. Wicked people.
 
LISSU NI MJINGA MKUBWA HIVI ANACHOFURAHIA NI NINI ? LENGO ZIMA NI MAENDELEO NA KUJIKWAA SI KUANGUKA , NA KAMA IKIJA NDEGE ATAJINYONGA MAANA ANASUMBULIWA NA WIVU MTUPU.PENYE NIA PANA NJIA LISSU KAMA SHETANI ASHINDWE KWA JINA LA YESU AMEN !
 
View attachment 570274
Lissu katika mtandao wake wa twita ameonekana kuyacheka majibu ya serikali juu ya "kupotea" kwa Bombadia.

Serikali imetoa majibu yasiyoridhisha na ya kujikanganya kuhusu kashikiliwa kwa ndege yake nchini Canada. Serikali imelaumu wanasiasa kuingilia mchakato huku ikiogopa kuwataja wanasiasa hao

Nini maoni yako
Hata mimi nimecheka sita acha kukumbusha kwa usemi huu 'Any decision you make in life you are responsible for it'
 
Serikali yamjibu Lissu kuhusu ujio wa Bombadier
By Contributor | August 19, 2017 - 3:13 pm

Serikali kupitia kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu Idara ya Habari, Zamaradi Kawawa ,imejibu madai yalitolewa jana na Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissukuwa ndege ya Tanzania, Bombadier kuwa imeshikiliwa nchini Canada kutokana na serikali kudaiwa.

Soma taarifa kamili:

Mnamo tarehe 18 Agosti, 2017 siku ya Ijumaa, kuna taarifa zimetolewa kwenye vyombo vya habari kwamba kuna mgogoro wa utekelezaji wa ununuzi wa Ndege ya tatu inayonunuliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka kampuni ya Bombadier ya Nchini Canada.

Taarifa hiyo iliendelea kudai kwamba kuna wanasheria wa Kampuni fulani ya Nchini Italia, walioweka zuio la ununuzi wa Ndege hiyo kwa maelezo kwamba, wanakamata mali hiyo ya Serikali kwa kuwa kuna Kampuni inayodai Serikali ya Tanzania.

Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari na Msemaji Mkuu wa Serikali inapenda kuufahamisha Umma kuwa mgogoro huo upo ila kimsingi ni mgogoro ambao umetengenezwa na Watanzania wenzetu ambao kwa bahati mbaya sana wameweka maslahi ya kisiasa na ya binafsi mbele zaidi ya maslahi ya Taifa.

Mambo Muhimu ambayo Umma Ufahamu

Ndege zinazonunuliwa ikiwepo hii ambayo imetengenezewa Mgizengwe na hao Watanzania wenzetu sio ya Rais Magufuli bali ni za watanzania wote.

Hawa baadhi ya viongozi wa kiasiasa wanaoshabikia migogoro inayokumba jitihada za Rais wetu, za kutuletea maendeleo, hawana Uzalendo.

Serikali imesikitishwa sana tena sana kwa hujuma zinazofanywa waziwazi tena kwa ushabiki wa hali ya juu na baadhi ya viongozi wa kisiasa wa chama hicho, kupingana na mwelekeo mzuri wa Mhe. Rais kutuletea maendeleo
Kwa mtu yeyote mwenye uchungu na Nchi yake,angepambana ili jambo linalohusu maslahi ya Taifa, likiwepo la kununua Ndege, lisikwame na kama kuna mkwamo basi ashilirki kukwamua badala ya kushabikia.

Serikali pia ina fununu kwamba watu hawahawa wanaohujumu jitihada za kimaendeleo, pia wanahujumu hata hali ya usalama wa raia wetu kwenye baadhi ya maeneo ya Nchi yetu. Hili nalo linaendelea kufanyiwa kazi kwa kina.Wanaopinga mambo ya Maendeleo hawapingani na Mhe. Magufuli bali wanapingana na Watanzania wote kwa ujumla.

Hivyo basi ni vyema Watanzania mkaelewa ukweli wa hali halisi na mkapuuzia mambo ambayo yanashabikiwa na baadhi ya viongozi hao wa kisiasa wanaotafuta umaarufu rahisi (Cheap Popularity). Endeleeni kumuombea Rais wetu na Tanzania kwa Ujumla kwani Chini ya Uongozi wake, amedhamiria kwamba hakuna kurudi nyuma (no reverse gear).
Serikali ilikuwa inawahisi baadhi ya wanasiasa kuhusika na hujuma hizi na sasa sio hisia tena bali baadhi yao wameshaanza kujitokeza hadharani.

Hatua za Kuchukuliwa/Zianzochukuliwa:
Kuhusiana na Mgogoro kwenye ununuzi wa Ndege, hatua za Kidiplomasia na za kisheria zimeanza kuchukuliwa ili kumaliza jambo hili. Aidha kwa wale wanaoshabikia na kutengneza migogoro na hujuma mbalimbali dhidi ya maendeleo ya Nchi yetu, Serikali itaendelea na taratibu za kiuchunguzi na haitasita kuchukua hatua za kisheria zinazostahili.

Serikali inatumia pia fursa hii kuwaomba Watanzania wasiwe na wasiwasi wala tashwishi kuhusu mpango wa Ndege kununuliwa na kwamba waendelee kuiamini Serikali yao iliyopo madarakani inayoongozwa na Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli. Uzalendo wetu uwe ndio mtaji mkubwa kuliko siasa, dini au ukabila.

Serikali ilikuwa na fununu kwamba kuna viongozi wa baadhi ya Vyama vya Siasa ambao kwa namna moja au nyingine wangependa kuhujumu jitihada za Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa jitihada zake za kuwaletea Watanzania (hasa wanyonge) maendeleo.

Wanasheria hao waliokwenda kufungua madai kwamba Serikali yetu inadaiwa na kwamba Ndege hiyo ishikiliwe, hawana uhalali wowote wa kufanya hivyo na ni matapeli tu ambao wamesukumwa na baadhi ya viongozi wa kisiasa wasioitakia mema Nchi yetu.

Kwa kuwa Serkali ilishapata fununu kwamba kuna baadhi ya viongozi wa chama cha siasa wana mpango huo, sasa watu hao wamejidhihirisha hadharani kwamba wao ndio wako nyuma ya pazia la kuhujumu jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano kwa maslahi yao ya kisiasa.

Serikali ya awamu ya Tano Inawahakikishiwa Watanzania kwamba Ndege itakuja. Wanaokwamisha jitihada za Serikali za kuleta ndege watapanda na ndugu zao watapanda na wafuasi wao watapanda .

Serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe. Dkt John Pombe Magufuli haibagui watanzania kwa itikadi za Kisiasa, Dini, Kabila, rangi au utofauti wowote.

Kundi hilo la baadhi ya Viongozi wa siasa walishatoa maelezo ya kuvuruga au kukejeli jitihada za Serikali. Mambo ambayo wanasiasa hao walishayakingia kifua ni pamoja na;

Kushawishi wafadhili wasilete misaada tena Tanzania.Watu hawahawa walishawahi kuomba kwamba Washirika wetu wa Maendeleo wasilete tena misaada Tanzania.

Tunachojiuliza kama Serikali, hivi misaada isipoletwa anayekomolewa ni Rais Magufuli? Au ni Watanzania wanyonge ambao wangekosa madawa, Huduma za Maji, Umeme, n.k.

Jambo la kutia faraja ni kwamba pamoja na jitihada za hali ya juu za watu hao, Washirika wa Maendeleo sasa wameongeza kasi ya ushirikiano na Serikali inayoongozwa na Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli. Mifano ya wazi ya hivi Karibuni ni tamko la Serikali ya Marekani kupitia Balozi wake kwamba Marekani itaogeza kiasi cha Misaada Tanzania, Ziara ya Tajiri Masuhuri Duniani Bill Gate ambaye pia ameonyesha kuguswa na kasi ya uongozi wa Mhe. Magufuli na kuahidi kutoa fedha zaidi, Ujio wa Viongozi wakuu wa Nchi 15 ndani ya muda ambao Mhe. Magufuli amekuwa Madarakani na mambo mengine mengi.

Kubeza Juhudi za Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli; Imekuwa ni hulka ya hao baadhi ya viongozi wa siasa kufanya kila jitihada za kubeza jitihada za dhati ambazo Mhe. Rais anafanya kuwaletea Wananchi Maendeleo tena hata bila kujali kwamba eneo husika linaongozwa na Kiongozi wa Chama gani. Hata tukio ka Kihistoria lililofanyika hivi karibuni Jijini Tanga, la kuweka jiwela msingi Ujenzi wa Bomba la Mafuta, Mhe. Rais alionyesha dhahiri kutobagua hata maeneo yale ambayo hayaongozwi na CCM. Tulitegemea huu uzalendo wa Mhe. Rais Ungeungwa mkono na watanzania wote.

Kubeza jitihada za Kunusuru madini yetu na Maliasili. Mhe. Rais Magufuli anafanya jitihada za dhati kabisa kunusuru mali asili zetu na ndio maana akasimamia kwa uadilifu, uaminifu na uwajibikaji suala zima la Makinikia. Hii ilimfanya hata Rais wa Kampuni ya Barick kukodisha Ndege kuja kumuona Mhe. Rais, na tunaamini jitihada hizi zitazaa matunda. Lakini baadhi ya viongozi haohao wa siasa wamekuwa mstari wa Mbele kupingana na jitihada hizi kwamba tutashitakiwa kwa hiyo bora tuache makinikia yapelekwe tukiendelea na majadiliano.

IMETOLEWA NA

Idara ya Habari (MAELEZO)

19/08/2017.
 
duh mwanasheria ambaye kesi haimhusu anawezaje kwenda kuweka pingamizi mahakamani kuzuia mali ya mdaiwa??..

Tunadaiwa au hatudaiwi?..

Hii 2017, watanzania wa sasa sio wa 1970 jaribuni kutolea vitu ufafanuzi vieleweke na sio blah blah.
 
Sera za Chadema zimehamia kwenye kuhujumu uchumi
 
Mapuuzi sana haya majamaa ya chama kile sijui kwa nini hayapendi kushaurika kwenye mambo ya msingi na ya maslahi kwa wote,uchawi na unafiki tuu,ukurupuke wewe uanze kimsingizia aliyekupa tahadhari mapema ili iwe nini?
 
Back
Top Bottom