Msemaji wa Serikali akiri ndege mpya ya Bombardier Q 400-Dash 8 kushikiliwa nchini Canada. Awatupia lawama wanasiasa...

Msitufanye Watanzania wote punguani kawadanganye Lumumba wenzako wenye akili za kushikiwa na Mkiti.

Sasa tuone kama hutalipa deni kwa nguvu, na utalia maisha magumu na kodi lazima ulipe utake usitake, ili hilo deni lilipwe. Na hutasikia serikali itayolia njaa, wewe ndo utakamuliwa na ndo utalia njaa. Chongeaneni tena tafuta deni jingine, ili wewe kamanda usiwe mjinga.
 
Mkuu akili ndogo KAMWE haiwezi kushinda akili kubwa ndiyo sababu wanataka kuifunga mitandao maana pamoja na kutoa buku saba kwa siku bado humu wanagaragazwa vibaya sana pamoja na kuwanunua wale waliokuwa upande wa kutetea maslahi ya Watanzania na Tanzania.

Naona tukija na hoja za mantiki wanasepa.

Kuna watu unaanza kubishana nao kwa kasi halafu mmoja mmoja anasepa hawajibu hoja.
 
Nimesoma andiko lako mpaka machozi yanataka kunitoka.Ila Mungu yuko
Mkuu UPOPO kama uliona kwenye tv vilio vile vya wamama wajane lazima utaona kuwa utawala huu hautakuwa salama hata kidogo. Hata kama ni sheria mpya haizuii kuwepo kwa utu
 
Nilisikia kwenye siasa ukitupiwa kitu ni lazima urudishe kabla hakijapoa,hata kama utarudisha uwongo,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Serikali ilipe deni tu.

Serikali ya nchi kuwa dhulumati si kitu kizuri.

Deni hili lisipolipwa linaenda kwenye rekodi ya nchi yetu kama watu tusiolipa madeni, kesho tukitaka kukopa tena tutakataliwa au kupewa mkopo wa interest kubwa ajabu, kwa sababu tunaonekana tunakataa kulipa madeni.

Dawa ya jipu kulipasua, usiogope uchungu.

Sasa inakuwaje daktari mkuu wa kutumbua majipu anaogopa kulitumbua jipu hili la kulipa deni sugu?

Au yeye anaweza majipu rahisi tu ya kufukuza watu kazi serikalini, akipewa majipu ya kulipa madeni anasuasua?

Mikataba ya kununua hizi ndege iko so complex na kikitokea kitu chochote hapo kati - ajali etc- kabla ya makabidhiano, Bima inahusika kulipa. Na kawaida bima huwa haifanyi coverage ya habari kama hii.
 
Argument yenyewe in lack mashiko. Kuingilia mgogoro kivipi?wawekeni bayana watanzania tujue siasa zimeingilia vipi mchakato wa procurement procedures ambazo ni international?Mbona serikali haipo tayari kukiri udhaifu unapo tokea?yaani wanatuaminisha they're perfect in everything?kila kitu wanajua wao .Haya tuendelee na haka kautamaduni
 
deni ni la 2009 acha ukuda bob


ha! ha!
Just hahaah!!! hahahaha!!!

ha ha Just ha ha ha baada ya kuvuta chake.

Wacha wewe usiwe mkuda ukamuliwe kodi, utalipa kwa kutaka ama siyo kutoka na ni wewe ndo utalia njaa. Serikali inapeta tu hado hado.
 
Kadiri unavyozidi kutiririsha pumba ndivyo unavyojianika zaidi na kuonyesha jinsi ulivyo upstairs, pole!
Jaribu kuchunguza zaidi maana ya maneno haya: kunanga na kunusuru.
 
kwan we hutalipia hilo deni?
anyway kama wewe haupo nchini c unatuma hela?
c kuna babu zako huku
uzuri wa bongo asie kua na kazi na aliekua nayo wote wanalipa kodi

ha! ha! ha! Just hahah.... hahaa!!!!!!
 
mbona wanatuchanganya? kati ya sirikali na aliyewafahamisha watanzania kinachoendelea nani mtetezi wa maslahi ya walipa kodi? hawana haja ya kuhubiria wananchi waiamini serekali kwa kuwa kila kitu kipo wazi, tatizo siyo kushikiliwa kwa ndege shida kubwa ni kuvuja kwa habari hii, maana wangejua mipango ya hao wanasiasa wangeliwaumbua mapema tu.
ccm ndo imetufikisha hapa na bado itaendelea kudidimiza maisha ya mtanzania hadi hapo watakapopata akili.shenzi
 
Mkuu huyu jamaa TL hata kipindi cha Mkapa sasa hivi ingekuwa story nyingine,ila dawa yake inachemka kwa kasi sana,kile kitambi kitashuka ghafla kama puto(balloon).Kagame huwa anawafata hata U.S anawatungua huko huko kwa maslahi mapana ya nchi.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] ....Kagame mti mkavu hana utani hata kiduchu.
 
kwan we hutalipia hilo deni?
anyway kama wewe haupo nchini c unatuma hela?
c kuna babu zako huku
uzuri wa bongo asie kua na kazi na aliekua nayo wote wanalipa kodi

ha! ha! ha! Just hahah.... hahaa!!!!!!

Kama umenisoma hapo juu nimesema tutalipa wote aliyekuemo na asiyekuwemo. Sasa nashangaa mtu kururahia kulipishwa kodi zaidi ili maisha yake yawe mabaya zaidi.
Ha ha ha Just ha ha ha kishavuta chake. Wacha maisha yawe taiti.
 
Habari zenu wakuu, serikali ya awamu ya tano inajitahidi kwa hali na mali kuhakikisha Tanzania inapiga hatua kiuchumi ili kujikwamu kutoka dunia ya tatu kwenda dunia ya pili.Tumeona Juhudi kubwa zikifanyika katika kuhakikisha hilo linawezekana.Tumeona jinsi serikali ilivyodhibiti ufisadi ambao kwa kiasi kikubwa uliturudisha nyuma.

Tunaona serikali ilivyojitahidi kujenga miondombinu nzuri ili kuhakikisha kila kona inafikika tena kirahisi ikiwezekena miaka ya mbele mtu awe anaishi morogoro anafanya kazi dar es salaam.Tumeona upokonywaji wa viwanda kwa watu walioshindwa kuviendeleza ili vienelezwe.Tumeona jinsi wawekezaji wanavyobanywa ili rasilimali zitunufaishe watanzania.

Lakini kumeibuka wanasiasa njaa wachache wenye njaa ambao wanatumika na watu wasiitakia mema Tanzania yetu kama vile mafisadi wauza madawa na wawekezaji wengi kurudisha nyuma juhudi za mh Rais katika kuleta maendeleo kwa kuwachochea na kuwashawish wananchi wasimuunge mkono mh Rais.Pia wanatumika katika kueneza habari za uongo zenye lengo la kuwakatisha tamaa wananchii.Tunaomba serikali iwachukulie hatua wanasiasa wa namna hii ikiwezekana washitakiwe kama wahujumu uchumi au wahaini.
 
Lipen deni hizi n drama tu mnafanya hku JF

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kadiri unavyozidi kutiririsha pumba ndivyo unavyojianika zaidi na kuonyesha jinsi ulivyo upstairs, pole!
Jaribu kuchunguza zaidi maana ya maneno haya: kunanga na kunusuru.
Wewe kwa kuwa hujanisahihisha kwa kunieleza maana za maneno hayo, umejionyesha unaleta pumba zaidi ya zozote nilizoweza kuleta mimi.

Unajaribu kusema nimekosea bila ya kueleza wazi kwa nini nimekosea na nilichokosea ni kipi na maneno hayo maana yake nini na kwa nini nilivyoyatumia hapo nimekosea.

Hujaeleza hilo.

Kwa sababu umezoea utamaduni wa kuongea pumba.Utamaduni wa kuongea bila ushahidi.Utamaduni wa kuongea bila ufafanuzi.

Wewe ndiye umeleta pumba zinazoonyesha jinsi usivyo na upeo, uelewa wala uwezo hapa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…