Upepo wa Pesa
JF-Expert Member
- Aug 8, 2015
- 21,772
- 35,770
Kwanini serikali walikaa kimya?Why CHADEMA are parting? Is it laughable?
Kwanini serikali walikaa kimya?Why CHADEMA are parting? Is it laughable?
Kwahiyo ndege ni zao au sio?Hata wafanyejeee. sisi tutazilinda rasilimali zetu jamaaaa. madini ni yetuuu
Kwani kilichotokea ni aibu?
Na ni magufuli na genge lakeTanzania tuna Judas Iscariot!!!
2028 kuna nini?Lissu anajiharibia 2028 hata udiwani hapati. Maana amesahau jimbo lake sasa anahangaika kupiga mikele kama mbayuwayu
Sent using Jamii Forums mobile app
We ndo bwege kwel kwaiyo deni la taifa nalo mzungu atasaau deni ahahaha sasa naona jinsi gani uongozi unatutia hasara kesho we ndo unaenda kuwa waziri kwann tusiingie matatizo ebu jipange soma hoja yako then shilikisha hata mkeo kidg akusaidia wazo lako la mzungu kusaau deni liko sawa au umekurupuka likakutoka
Wewe una muuliza nani na wewe ni NANI?MASWALI 10 KUHUSU MAJIBU YA SERIKALI JUU YA NDEGE YETU KUKAMATWA CANADA.
Jana Lissu aliibua mjadala kuhusu ndege yetu kukamatwa huko Canada kutokana na deni la TZS Bilioni 87 tunalodaiwa na kampuni ya Stirling Engineering Ltd, kutokana na kuvunja nao mkataba wa ujenzi wa barabara ya Wazo Hill - Bagamoyo mwaka 2009.
Mjadala ukawa mpana baada ya kupata attention kubwa kwa watu na vyombo vya habari. Mbunge wa Kigoma mjini ZZK akauendeleza mjadala huu kwa kumuita Waziri Mbarawa kwenye ukurasa wake ili ajibu kama ni kweli ndege yetu imekamatwa au lah.
Alhamdulilah. Waziri akajitokeza. Kama mjuavyo Waziri Mbarawa ni mtumiaji mzuri wa mitandao. Mbarawa akakanusha taarifa hizo na kusema ni uongo na uzushi. Akaema ndege ipo na HAIJAKAMTWA, isipokua kuna mambo ya kiufundi hayajakamilika. So yanamaliziwa and soon ikiwa tayari itawasili nchini.
Vijana wa CCM wakamshangilia majibu hayo "mazuri" na wakaanza kumtukana ZZK kwamba anashabikia propaganda za uongo za Lissu.
Leo Naibu Murugenzi ya Idara ya Habari Maelezo, ambaye pia ni Naibu Msemaji Mkuu wa serikali Bi.Zamaradi Kawawa amefanya mkutano na waandishi wa habari. Kwa kinywa chake amekiri kwamba NI KWELI NDEGE YETU IMEKAMATWA CANADA kutokana na kesi iliyofunguliwa mahakama ya usuluhishi ya kimataifa na kampuni ya Stirling Construction Ltd. Lakini akasema wanasiasa ndio wamechochea hadi kesi hiyo kufunguliwa na ndege hiyo kukamatwa. Kwa kifupi amewalaumu sana wanasiasa na kuwabebesha mzigo wote wa kukamatwa ndege yetu.
Maelezo ya Zamaradi leo na yale ya Prof.Mbarawa jana yamenipa maswali yafuatayo:
1. Kwanini Zamaradi amesema Wanasiasa ndio wamechochea ndege hiyo kukamatwa? Ina maana "driving factors" za kukamatwa ndege hiyo ni wanasiasa tu? Just that? How?
2. Kuna uhusiano gani kati ya wanasiasa na kitendo cha kuvunja mkataba na kampuni ya Stirling Constructuon?
3. Wale vijana waliomtukana Lissu na ZZK jana mitandaoni na kuungana na Prof.Mbarawa kusema hakuna ndege ya Tanzania iliyokamatwa, wamejisikiaje baada ya Zamaradi kukiri kuwa ni kweli ndege yetu imekamatwa?
4. Kwanini maafisa waandamizi wa serikali (Waziri na Msemaji mkuu wa serikali) wanapingana hadharani? Waziri anasema ndege haijakamatwa, Msemaji mkuu wa serikali anasema ndege imekamatwa. Je Waziri hakua na taarifa au alidhamiria kudanganya?
5. Je, inawezekana Waziri husika asijue kuhusu suala hili la ndege wakati lipo chini ya Wizara yake?
6. Kwanini Zamaradi hajawataja hao wanasiasa waliozuia ndege yetu kukamatwa? Na kwanini hajaeleza wamezuiaje?
7. Kama serikali ilivunja mkataba na kampuni ya Stirling Construction, na kampuni hiyo ikaenda mahakamani na kupewa kibali cha kukamata ndege yetu, kwanini Zamaradi asiseme kwamba aliyezuia ndege yetu kukamatwa ni Waziri wa ujenzi (wa wakati huo) aliyefanya maamuzi ya kukurupuka, badala ya kuwasingizia wanasiasa?
8. Kwanini serikali haikusema mapema jambo hili kabla Lissu hajaliibua? Walitaka kuficha nini?
9. Lissu alieleza jana kwamba serikali italipa Dola milioni 12.5 (Kama TZS Bilioni 30) ili ndege hiyo iachiwe, wakati mazungunzo mengine yakiendelea (kuondoa pingamizi lililopo mahakamani). Maana yake ni kwamba tukiona ndege hiyo imetua tujue tumeshalipa Bilioni 30 za awali. Je pesa hizo zinatoka wapi? Ni kodi za wananchi? Kwanini Waziri aliyevunja mkataba huo asiwajibishwe kulipa peke yake?
10. Basil Mramba na Grey Mgonja walisababishia taifa hasara ya dola 7.5M sawa na TZS Bilioni 11, wakashtakiwa na kufungwa jela. Je serikali haioni kuna umuhimu pia wa kumshtaki waziri wa ujenzi aliyevunja mkataba na kampuni ya Stirling kwa kukukupuka?
Ndo hapo sasa..Uwongo haujawahi kushinda ukweli hata siku moja. Kwani kuna ubaya gani kukubali kuwa tunadaiwa.
Sent using Jamii Forums mobile app
Hapa wapinzani wanahusikaje sasa? Hapa twaweza wanahusikaHaya ndio tumekuwa tukiyasema kila siku....Hawa wapinzani wa nchi hii wakae wakijua hawamkomoi MAGUFULI bali wanatukomoa sisi WATANZANIA
Nimesoma andiko lako mpaka machozi yanataka kunitoka.Ila Mungu yukoMie niliangalia vile vilio vya wakina mama wajane pale Kimara walioishi maeneo yale kisheria zaidi ya miaka 40 na wengine kule Tabora Tambukareli vikongwe kabisa wakibomolewa vijumba vyao eti sheria imebadilika nikajua vilio vile haviwezi kuacha utawala huu salama. Huwezi mbomolea mama mjane hata kama ni kuleta maendeleo huku unacheka kwa furaha kama vile yule sio kiumbe wa Mungu! Na Mungu huyo akakuacha salama.
Mikosi hii itaendelea hadi utawala utakapo fitinika kwa machozi yale, hivi hamjifunzi kwa JK wakati mwingine alikuwa anamwambia huyuhuyu tingatinga kuwa "taratibu bwana, sheria zipo tuu na uanadamu nao upo. Hapo acha!"
Ila sasa hivi kuleta maumivu kwa wengine nikama fashion na hilo linaleta mikosi kwa utawala bila kujua
Hamna haja ya kura mkuu! kwani humjui mhujumu uchumi wetu?? hujui na magufuli na genge lake la ccm??Tupige kura ya wazi na kutoa maoni yetu juu ya wanaoshirikiana na wahujumu wa uchumi.
Ongeza sss au zzz kabisa kuweka msisitizo maana wako wengiTanzania tuna Judas Iscariot!!!
Time will tellJana nilimsikia wakili na mbunge Tundu Lissu akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam na kusema ana taarifa kutoka kwenye vyanzo vyake serikali vilivyomwambia kuwa ndege ya serikali aina ya Bombadier imekamatwa na kutishia kupigwa mnada!.
Kauli ya Lissu iliibua mjadala mkali kwenye mitandao ya kijamii,katika pita pita zangu mtandani nikakuta "Conversation" kati ya Zitto Kabwe na Waziri mwenye dhamana Prof Mbarawa,kwenye maelezo yake Prof alisema si kweli kuwa ndege imekamatwa na hakuna mgogoro bali kuna mambo madogo madogo yanakamilishwa kati ya serikali ya kampuni ndiyo maana ndege imechelewa na kuja na itakuja siku si nyingi.
Asubuhi ya leo,idara ya maelezo ambayo ndiyo mdomo wa serikali imezungumza na waandishi wa habari kupitia naibu Mkurugenzi wake mkuu Zamaradi Kawawa na kujibu kuwa ni kweli kuna kesi ya msingi iliyosababisha ndege hiyo kuzuiwa huku akiwatuhumu baadhi ya wanasiasa kuwa wapo nyuma ya kesi hiyo.
Zamaradi amedai kesi hiyo imesababishwa na baadhi ya wanasiasa ila ameshindwa kuwataja majina na kusema tayari serikali imechukua hatua za kisheria na kidiplomasia kumaliza kesi hiyo!.
My take.
Serikali ilikuwa inamsubiri Lissu aseme ndiyo nayo ijitokeze kumjibu?Rais aliahidi ndege kuwa ingewasili mwezi July mwaka huu,mwezi umekwisha ndege haijaja.
Kulikuwa na ugumu gani kwa serikali kulisemea hili mapema kuliko kumsubiri Lissu aiseme ndiyo ijitokeze kujibu,Je Lissu angekaa kimya serikali nayo ingekaa kimya?
Matokeo yake,majibu ya wizara husika kutoka kwa waziri husika na yale ya idara ya habari maelezo yanatofautiana,wananchi washike lipi?
Serikali imetoa maelezo ya kulaumu zaidi bila kuuambia umma,hiyo kesi inahusu nini? na kama kweli kuna wanasiasa wapo nyuma ya kesi hiyo,kuna ugumu gani kuwataja?
Siku zote ukweli utakuweka huru.
Imebidi ni ku - quote tu japo maelezo yako ni mengi sana!Tundu Lissu ni mwanasheria na kama mwanasheria, anaruhusiwa - kwa kweli anatakiwa- kumpa mtu yeyote haki ya kutetewa na wanasheria. Ndiyo maana hata wezi na wauaji huwa wanatetewa na wanasheria.
Hiyo ni kazi ya wanasheria.
Ni sehemu ya utawala wa sheria.
Marekani huwashitaki watu kwa ugaidi, halafu watu hao wanaoshitakiwa kwa ugaidi hutetewa na wanasheria wa Marekani wanaoheshimika sana.
Hilo linaonyesha ukomavu wa mfumo wa sheria wa Marekani.
Actually hata Saddam Hussein katika kesi yake alikuwa na mwanasheria mmoja Mmarekani.
Kwa hiyo, Tundu Lissu hata leo akiamua kuwa wakili wa Acacia katika kesi Acacia na Tanzania, mimi kwa kuwa naelewa utawala wa sheria unafanya kazi vipi na haki ya kuwakilishwa na mwanasheria ikoje, sitakuwa na kinyongo.
In fact, Acacia wakiwakilishwa na mwanasheria anayesemwa kuwa mahiri kama Tundu Lissu, halafu wakashindwa, hapo serikali itajigamba kwamba imeshinda kesi bila kuinyima Acacia haki ya kuwakilishwa na mwanasheria mahiri kama Tundu Lissu.
Kwa hiyo tuachane na Tundu Lissu. Yeye ni mwanasheria. Hata akimtetea muuaji, ni kazi yake. Marehemu Johnnie Cochran alikuwa wakili anayeheshimika. Alimtetea O.J Simpson mpaka O.J akashinda. O.J kuna watu kibao wanasema mpaka leo kaua. Lakini Johnnie Cichran kajizidishia heshima kushinda kesi kwa sababu watu weusi wameona ametoa mfano jinsi gani mfumo wa sheria unavyoweza kumpa nafasi mtu mweusi mwenye mwanasheria mzuri kushinda kesi mbaya sana ya mauaji.
Kwa hiyo Tundu Lissu hata akiamua kuwa wakili wa hao wa Canada mimi nitamshukuru kwanza kabisa kwa kuonyesha kwamba Tanzania si nchi ya kijima kwamba ukiwa na kesi na serikali mawakili wote wa Kitanzania watakususa. Huo utakuwa ni ushamba.
Kama umeona movie ya "Amistad" ambayo imetokana na habari ya kweli, utaona mtu anaitwa John Quincy Adams. Hiyu alikuwa rais wa zamani wa US ambaye baba yake (John Adams) alikuwa rais wa pili wa Marekani.
John Quincy Adams, licha ya kuwa rais wa Marekani wa zamani, aliichukua kesi kuwatetea watumwa wa Kiafrika walioua nahodha wa meli iliyowachukua kutoka Sierra Leone West Africa. Meli ilichukuliwa mpaka Connecticut baada ya dhoruba na wale weusi ambao walishikwa kuuzwa utumwani wakafungwa. John Quincy Adams akachukua kesi ike akiwatetea watumwa dhidi ya serikali ya Marekani.
Ni sawa na Mwinyi leo awe mwanasheria wa Acacia.
Lakini kati ya vitu ambavyo John Quincy Adams anaheshimiwa kwavyo mpaka leo, ni kuchukua kesi hii.
Kwa sababu alionyesha kwamba hata ukiwa mtumwa, kuna Wamarekani watakaotaka kutumia mfumo wao wa sheria kukutetea.
Tumuache Tundu Lissu awe mwanasheria. Kwa sababu kazi yake inamruhusu kumtetea hata muuaji.
Mimi nataka kuijadili serikali na ilivyoboronga.
Zaidi kuhusu Amistad soma hapa.
John Quincy Adams and the Amistad case, 1841 | The Gilder Lehrman Institute of American History
Sent from my Kimulimuli
sawa ila deni utalipa tu na kodi inakutaiti serikali na utalipa uwe unataka ama hutaki kama kawaida, na mchongeani zaidi maisha yawe mazuri.
hizi akili zilizotumika hapa mmechongeana wenyewe kwa mzungu, na mtaendelea kuchongeana ili maisha yenu yawe magumu zaidi ndo furaha zaidi.
Mnaona jinsi gani bado tuna safari ndefu?Haya ndio tumekuwa tukiyasema kila siku....Hawa wapinzani wa nchi hii wakae wakijua hawamkomoi MAGUFULI bali wanatukomoa sisi WATANZANIA
unajua maana ya uzalendo au unaropoka tu??m. kuwa mzalendo kidogo... .
Kwanini walitaka iwe siri..??Kwani kilichotokea ni aibu?