Msemaji wa Serikali akiri ndege mpya ya Bombardier Q 400-Dash 8 kushikiliwa nchini Canada. Awatupia lawama wanasiasa...

Msemaji wa Serikali akiri ndege mpya ya Bombardier Q 400-Dash 8 kushikiliwa nchini Canada. Awatupia lawama wanasiasa...

Mapepo yanashangilia nchi ikienda kombo tena mijitu mingine ingependa Tanzania ipigwe nukiria au vita itokee
Mashetani mshindwe na mlegee
 
If possible miradi isiyo na tija kwa taifa kama ile ya ujenzi wa airport ya Chato isimamishwe na fedha zilipe madeni na tuache kuvunja hovyo mikataba bila kufuata sheria ili maisha yaendelee.
 
Mapepo yanashangilia nchi ikienda kombo tena mijitu mingine ingependa Tanzania ipigwe nukiria au vita itokee
Mashetani mshindwe na mlegee

Nchi itaendaje kombo kama hakuna watu walioko busy kuipeleka nchi kombo?, cha Muhimu ni kuwa wajibisha wote waliohhhusika na kuliingiza taifa kwenye hiyo kadhia
 
MASWALI 10 KUHUSU MAJIBU YA SERIKALI JUU YA NDEGE YETU KUKAMATWA CANADA.

Jana Lissu aliibua mjadala kuhusu ndege yetu kukamatwa huko Canada kutokana na deni la TZS Bilioni 87 tunalodaiwa na kampuni ya Stirling Engineering Ltd, kutokana na kuvunja nao mkataba wa ujenzi wa barabara ya Wazo Hill - Bagamoyo mwaka 2009.

Mjadala ukawa mpana baada ya kupata attention kubwa kwa watu na vyombo vya habari. Mbunge wa Kigoma mjini ZZK akauendeleza mjadala huu kwa kumuita Waziri Mbarawa kwenye ukurasa wake ili ajibu kama ni kweli ndege yetu imekamatwa au lah.

Alhamdulilah. Waziri akajitokeza. Kama mjuavyo Waziri Mbarawa ni mtumiaji mzuri wa mitandao. Mbarawa akakanusha taarifa hizo na kusema ni uongo na uzushi. Akaema ndege ipo na HAIJAKAMTWA, isipokua kuna mambo ya kiufundi hayajakamilika. So yanamaliziwa and soon ikiwa tayari itawasili nchini.

Vijana wa CCM wakamshangilia majibu hayo "mazuri" na wakaanza kumtukana ZZK kwamba anashabikia propaganda za uongo za Lissu.

Leo Naibu Murugenzi ya Idara ya Habari Maelezo, ambaye pia ni Naibu Msemaji Mkuu wa serikali Bi.Zamaradi Kawawa amefanya mkutano na waandishi wa habari. Kwa kinywa chake amekiri kwamba NI KWELI NDEGE YETU IMEKAMATWA CANADA kutokana na kesi iliyofunguliwa mahakama ya usuluhishi ya kimataifa na kampuni ya Stirling Construction Ltd. Lakini akasema wanasiasa ndio wamesababisha ndege hiyo kukamatwa. Kwa kifupi amewalaumu sana wanasiasa na kuwabebesha mzigo wote wa kukamatwa ndege yetu.

Maelezo ya Zamaradi leo na yale ya Prof.Mbarawa jana yamenipa maswali yafuatayo:

1. Kwanini Zamaradi amesema Wanasiasa ndio wamechochea ndege hiyo kukamatwa? Ina maana "driving factors" za kukamatwa ndege hiyo ni wanasiasa tu? Just that? How?

2. Kuna uhusiano gani kati ya wanasiasa na kitendo cha kuvunja mkataba na kampuni ya Stirling Constructuon?

3. Wale vijana waliomtukana Lissu na ZZK jana mitandaoni na kuungana na Prof.Mbarawa kusema hakuna ndege ya Tanzania iliyokamatwa, wamejisikiaje baada ya Zamaradi kukiri kuwa ni kweli ndege yetu imekamatwa?

4. Kwanini maafisa waandamizi wa serikali (Waziri na Msemaji mkuu wa serikali) wanapingana hadharani? Waziri anasema ndege haijakamatwa, Msemaji mkuu wa serikali anasema ndege imekamatwa. Je Waziri hakua na taarifa au alidhamiria kudanganya?

5. Je, inawezekana Waziri husika asijue kuhusu suala hili la ndege wakati lipo chini ya Wizara yake?

6. Kwanini Zamaradi hajawataja hao wanasiasa waliozuia ndege yetu kukamatwa? Na kwanini hajaeleza wamezuiaje?

7. Kama serikali ilivunja mkataba na kampuni ya Stirling Construction, na kampuni hiyo ikaenda mahakamani na kupewa kibali cha kukamata ndege yetu, kwanini Zamaradi asiseme kwamba aliyezuia ndege yetu kukamatwa ni Waziri wa ujenzi (wa wakati huo) aliyefanya maamuzi ya kukurupuka, badala ya kuwasingizia wanasiasa?

8. Kwanini serikali haikusema mapema jambo hili kabla Lissu hajaliibua? Walitaka kuficha nini?

9. Lissu alieleza jana kwamba serikali italipa Dola milioni 12.5 (Kama TZS Bilioni 30) ili ndege hiyo iachiwe, wakati mazungunzo mengine yakiendelea (kuondoa pingamizi lililopo mahakamani). Maana yake ni kwamba tukiona ndege hiyo imetua tujue tumeshalipa Bilioni 30 za awali. Je pesa hizo zinatoka wapi? Ni kodi za wananchi? Kwanini Waziri aliyevunja mkataba huo asiwajibishwe kulipa peke yake?

10. Basil Mramba na Grey Mgonja walisababishia taifa hasara ya dola 7.5M sawa na TZS Bilioni 11, wakashtakiwa na kufungwa jela. Je serikali haioni kuna umuhimu pia wa kumshtaki waziri wa ujenzi (wa wakati huo) aliyevunja mkataba na kampuni ya Stirling kwa kukurupuka na kuliingiza taifa kwenye hasara?

Malisa GJ

Sent using Jamii Forums mobile app
Rais hawezi kuwajibishwa kisheria kwa sab ana kinga Hata kosa alilifanya akiwa shule ya msingi. Alitakiwa kushtakiwa Wakati huo sio leo. Its too late.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Awe mkweli na kwa kukili yakuwa kwa ss nchi iko na hali mbaya ki uchumi,je na hilo nalo ni wapinzani wa ccm nfo wamesababisha?samaki wa makufuri pia ni wapinzani wa ki siasa wamesababisha?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Upuuzi, tena upuuzi mtupu.
Mbona hatukuwasikia kabla mkitueleza kuwa wanasiasa wenye hila wanaingilia manunuzi ya bombardier yetu.??¿
Mlikuwa mkisubiri nini????
Mbona hata sasa hamjibu maswali mloulizwa na wazalendo waliotushirikisha hili jambo.???
Hivi kwa nguvu ya Serikali hii hao wanasiasa mnashindwaje kuwakamata na kuwaweka ndani badala yake mnalalamika tu?????

INAUMA SANA. KUWENI WAPENZI WA MUNGU KWA KUSEMA UKWELI WOTE



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hiyo bila Lisu serikali haikuwa na mpango hata wa kulizungumzia hili?seriouzly?harafu wanatoa visingizio vya nursary kbs.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
JPM alishasema kuna baadhi ya Mawaziri Wapumbavu.....

Mambo mengi ya hovyo hovyo hapa Nchini yamefanywa na Serikali ya CCM...

Angalia kwenye Mikataba mbali mbali ya manunuzi na hata ile ya uwekezaji ni madudu matupu huko....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
U
Mbaya zaidi aliyekiuka mkataba huo ni Pombe himself akiwa waziri wa ujenzi 2009.

Ukurupukaji umesababisha taifa hasara ya billion 87 ambayo imesababisha Bombadier kutekwa Canada.
Ukitaka kujua vijana wa Lumumba hawana akili kabisa ni siku hii ndege kama itatokea ikaja watashangilia kweli kweli washasahau tumelipa madeni plus penalty huko.
 
wakija kutuka watakuja kushangaa treni za umeme na mafly over na ndege za kumwaga
mkuu leo nlikua na wazo kama hili lako halaf hiyo kesi si haina dhamana , yaani wanakaa ndani hadi wakija toka ni 2022 Magu yuko awamu ya pili mwaka wa pili
Teh teh teh! Naona magamba mnatekenyana tu hapo! Mnafanya madudu halafu watu wakisema mnawalaumu.

Sent from my SM-G610F using Tapatalk
 
Inatakiwa wananchi tusitoe taarifa ili kulinda maslahi na dhambi za serikali!
 
Tatizo lenu mnapenda kisifiwa tu, kwani mkikosolewa mnapungukiwa nini enyi mafalisayo na watoza ushuru.
 
Back
Top Bottom