Mshahara wa Daktari ni kiasi gani?

Mshahara wa Daktari ni kiasi gani?

Inategemea na mwajiri ni nanj .

Maana kuna wengine wanafanya chini ya Tamisemi.

Wengine wizara ya afya.

Wengine kwenye taasisi za kiserikali kila mmoja na mshahara wake japo kada ni moja.

Na unapoongelea Daktari.

Kuna MD
Kuna specialist.
Kuna Daktari bigwa .
Kuna Daktari mwandamizi.
Unafanya KAZI TAMISEMI.

Unafanya KAZI WIZARA YA AFYA.

Mshahara ni ULE ULE.
 
Mkuu nilikuwa najua unaakili kumbe zero brain!?
Ushaona wapi kampuni inatanganza hasara kila mwaka ya mabilioni lakini
wafanya kazi wake wanaongoza kwa mishahara!?
Duka lako kila siku lina pata hasara lakini mfanyakazi wako anajiipa mamilioni!?
wewe uko kwenye kundi la bureaucratic capitalist kama madelu na sio
real capitalist
Hujamuelewa Naona huyu dada mkuu. Naogopa kuharibu brain yangu. Ila kama hujamuelewa sijui. Ila your impact or value yako ndio inayo determine malipo yako ujue. Kutibu watu unaokoa maisha yao utakuwa ama watakuwa wamezalisha bilioni ngapi ama kufundisha watu wakafaulu hizo Ni bilions ngapi.
Yaani sijui nikuambiaje ili uelewe.
 
Sasa jamani unafanya kazi kwenye hospital inatibu wagonjwa 50 kwa siku, kila mgonjwa analipia elfu 20. Unataka kwa mwezi ulipwe Millioni 3 kweli?. Hizo hela za kukulipa hiyo pesa serikali inazitoa wapi.

Mwenzako anafanya kazi EWURA kama inspector, kila kwenye lita moja ya mafuta EWURA inachukua percent yake. Kila lita moja. Kwanini wasiwalipe wafanyakazi wao pesa ndefu?
We nae huwa ni mweupe sana kichwani
 
Hawa ni wazembe waite mimi niwasaidie eneo lililowazi la kujiajiri. Watapiga hela mpaka wasahau. Tatizo mindset ya kuajiriwa ndio inaharibu vijana. Lakini kiukweli kujiajiri ndio kunakufanya utoke hata kama umeajiriwa.
Wewe TAPELI unayeshinda humu JF unatafutia watu TEUZI za mshahara wa 3M na kuandika Application letter????

Labda UTAPELI ndio kazi unayoweza kufanya.
 
Kiyombo (TO 2006) nimesoma naye mwaka mmoja, alikua anapenda kufundisha tu alafu wala hakua kichwa kama unavyodhania ndani ya hiyo petroleum. TO wa mwaka 2013 yupo Pan African anapiga 13M kwa mwezi. Wengi wameajiriwa na wengine wamejiajiri ambao bado ni uzembe wao tu. Na wengine waliendelea na shule.
Kazidiwa na mwalimu wa shule nyingi za International

Sent from my LND-L29 using JamiiForums mobile app
 
Ndio ni risky, imagine. Outbreak ya ebola, COVID wakwanza kuumwa nani? HIV, watu wanajichoma na kumwagikiwa na damu kila kukicha. Kupigwa na vichaa Etc etc, kazi ta kudeal na watu ni ngumu na bado lawama kila mtu ana expect hao watu wawadekeze au wafanye kama wito, something is not right. Kuna mentality sio sahihi. Nilikataa huo ujinga muda sana.
Mwenyewe Advance nikichaguliwa pcb nikakataa nikaingia zangu pcm
 
Kwamba watu 50 watoe elfu 20 kama consultation fee pekee take bado vipimo.

Yaani hiyo hospital daktari mmoja anaingiza million consultation pekee, maana wakiwa zaidi ya mmoja means tayari kipato kinagawanyika. Basi hapo patakua na mzunguko mkubwa sana, na either we ni specialist au Hosp kubwa ambapo both scenarios utakua unalipwa pakubwa sio sawa na ma MD wa local government.
Mbona 20,000 hela ya kawaida sana, Dr mzuri mfano clinic Dr mashavu ama mzee wetu mgaya anachukua hadi 35,000 na kunakuwa na foleni ya kufa mtu, Kibongo bongo madokta wanahudumia watu wengi sana wanazidi 50.

Ndio maana Ma Dr wengi wanakuwa wanachepuka Hospitali Binafsi sababu kule dr anapata percentage fulani kwenye Hela anayoingizia Hospitali.
 
We nae huwa ni mweupe sana kichwani
Ego inakuendesha si Bora yeye Ni mweupe wewe utakuwa mweusi mkuu. So unadhani kuwa uwezo tulio nao Basi tumejiamulia kuwa tuwe hivi tulivyo ama unayo pride inakuendesha
 
Daktari anayeanza kazi basic ni TSH 1.3mil , take home 900+K...!!! Sema kuna viposho posho Kwa walio chini ya wizara ya Afya.... Maisha ni magumu Sana bado Kwa hawa watu, huwa wanakimbilia kwenye mikopo ya magar kuficha aibu...nazungumzia MD sio CO au tabibu
Umeitoa wapi hii mkuu
 
Back
Top Bottom