Mparee2
JF-Expert Member
- Sep 2, 2012
- 3,092
- 5,386
Natamani siku moja Serikali ifute kabisa Posho badala yake Izihamishie zooote kwenye MishaharaSasa jamani unafanya kazi kwenye hospital inatibu wagonjwa 50 kwa siku, kila mgonjwa analipia elfu 20. Unataka kwa mwezi ulipwe Millioni 3 kweli?. Hizo hela za kukulipa hiyo pesa serikali inazitoa wapi.
Mwenzako anafanya kazi EWURA kama inspector, kila kwenye lita moja ya mafuta EWURA inachukua percent yake. Kila lita moja. Kwanini wasiwalipe wafanyakazi wao pesa ndefu?
watu walipwe mishahara yenye uhalisia na sio kiini macho
Hivi kuna haja gani umlipe mtu mshahara wa laki 8 na 50, halafu mwisho mwezi Umpatie Milioni mbili?
Kwanza mfanyakazi anakosa PSSF, Lakini pia Serikali Kuonekana inalipa Kidogo wakati ukweli ni kuwa inalipa mishara Mizuri.
Huko Private Sector hakuna maposho ya kujiachia na ndio sababu mishahara huonekana ni Mikubwa