Humu kuna watumishi wengi sana , ila uhalisia ni huu, mshahara haujawahi kutosha na ndio maana kila mwisho wa mwezi wapwa huwa wako watupu kabisa , yani wanajikuta na madeni kila kona na hatima yake inakuwa kusubilia siku kama hizi na mambo ya kichelewa kidogo inakuwa ni msiba mkubwa.
Watumishi wengi wanaishi maisha yasiyoendana na hali zao halisi.
Wengi wao wanaendesha magari—tena si magari ya kawaida bali yale yenye injini kubwa—na pesa zao zote zinaishia kwenye mafuta.
Hii ni matumizi mabaya ya pesa zao chache.
Siku wakiamua kubadilika, maisha yatakuwa rahisi na mishahara itaonekana inatosha.
Hapa Dar es Salaam, kwa mfano, kama mtu anatumia daladala, pesa zake zinadumu kwa muda mrefu.
Rafiki yangu mmoja aliye Japan anasema kwamba zaidi ya asilimia sabini ya watu wanaoishi mijini hawatumii magari binafsi.
Hii inafanya mishahara yao itosheleze mahitaji yao vizuri.
Lakini hapa Tanzania, mtu mmoja anaweza kuwa na gari wakati anapokea mshahara wa shilingi laki nane tu na anaishi Mabwepande, ilhali kazi yake iko TAZARA (anamaliza hela anachezea hela). Hivyo, kila siku anasafiri kilomita 80 kwenda na kurudi kazini, hali inayomfanya ajiweke katika hali ya umasikini mwenyewe.
Ukimuuliza utasikia
"pale kazini tuna posho nyingi ndo nanunulia kiwese" Huyu posho zikikata tu anapaki kagari...ndio sababu mwisho wa mwezi magari huwa mengi sana barabarani hapa Dar.
Ni jambo la kusikitisha!