Inaweza kutosha kama ni bachelor na huna mambo mengi. Ili uweze kuwa na uhakika wa kumaliza mwezi mzima basi angalau on average kwa siku moja usizidishe shilingi 7,000/-
(Breakfast 1000, Lunch 2000, Dinner 2000, Nauli na Voucher 2000). Hapo maana yake usiwe na matumizi mengine ya ziada (yasiyo ya lazima). Hii itakusaidia walau kuwa na akiba kidogo mfukoni kwaajili ya dharura. Hapo tuki assume kuwa kodi, maji na umeme havipo kwenye hiyo hela.
Hapo sahau mambo ya kupiga gambe, kutembelea viwanja vikali na pia pisi kali utakula kwa macho labda upate wakukuhurumia tu.
Ila ndio harakati za maisha pambana kuna siku utatoboa jomba.