Mshahara wangu Tsh. 600,000, nataka nikope milioni 15 nijenge na kuongeza mtaji wa biashara, naomba ushauri

Hakika wabongo 😂
 
Mkuu weka mkeka wa namna utaitumia hiyo hela, lasivyo utaugua depression mbaya baadae.

Na kingine mke wako anapaswa kuwa mwenye juhudi na nia bora ya kusimama biashara lasivyo, atakukimbia, kaa na mkeo mwongee na mjue naweka je mkakati wa mafanikio

Kingine hiyo m15 ni ndogo sana kwa ujenzi ndugu. Tusikudanganye
 
Kwani unataka kusema nini?

12 months × 5 yrs= 60 Instalments.
Sasa 60 Instalments ÷ 15,000,000= 250,000 per month.
Atatakiwa kukawa 250k kila mwezi!
Sasa hakusema kama mshahara wake huo ni gross au net. Maana kuna PAYE, BIMA, MFUKO WA JAMII n.k.

Nimekosa la kusema sas hapo mkuu!
Hapo akikopa hela nyingi labla 5M kwa miaka mitano. Hesabu haipigiki mkuu.😊

Kama mshahara huo utakuwa ni gross hatoweza. Kama ni Net, pia hatoweza. Maana kuna sheria ya % ya kukopa ka mtumishi mkuu.
 
Shikamoni wakubwa zangu.

Mimi ni mtumishi serikalini, mshahara 600K. Nataka nijilipue, nikope benki Tsh. Milioni 15. Zipi faida na hasara zake? Na vipi kuhusu makato yao? Nimepanga nichukue wa miaka 5.

Karibuni.
Fanya majaribio kwa miezi 6, chukua hiyo laki 6 utoe makato ya mikopo uishi na Baki kila mwezi kwa miezi 6 uone maisha yatakuwaje kwa miaka 5 ukiwa na huo mkono
 
Shikamoni wakubwa zangu.

Mimi ni mtumishi serikalini, mshahara 600K. Nataka nijilipue, nikope benki Tsh. Milioni 15. Zipi faida na hasara zake? Na vipi kuhusu makato yao? Nimepanga nichukue wa miaka 5.

Karibuni.
Kama una imani na biashara yako, weka mzigo wote hapo, Biashara ikifanya vizuri itajenga nyumba..Milioni 15 utajenga kibanda siyo Nyumba.
 
Tuseme mil 5 unapeleka kwenye biashara na mil 10 unapeleka kwenye ujenzi. Hiyo nyumba labda kama ulishaanza unaenda kumalizia ila kama ndio unaanza kuanzia kuchimba msingi kitakulamba mzee. Nyumba hutahamia na maumivu ya makato yatakuwa makali zaidi
 
Kivipi nipo tayari kupokea mshahara wa laki3
 
Net au take home mkuu baada ya makato yote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…