Mshahara wangu Tsh. 600,000, nataka nikope milioni 15 nijenge na kuongeza mtaji wa biashara, naomba ushauri

Mshahara wangu Tsh. 600,000, nataka nikope milioni 15 nijenge na kuongeza mtaji wa biashara, naomba ushauri

Straight talk, hiyo hela ni kidogo sana ukijiingiza kwenye ujenzi kwa haraka, Fanya hivi: Kama ukikopa nunua kiwanja then ikiwa kuna biashara ulishaifanyia "feasibility study" ianze na fedha iliyobaki, hakikisha biashara yako inatawaliwa na uwepo wako kama hautaki stress kwa sababu uki-outsource tu probabilty ya kupigwa ni kubwa sana noways..
Endelea kupanga huku ukipiga mishe zako mdogomdogo utajikuta unasogeza malighafi za ujenzi taratibu na ukija kupigwa hatua inakuwa hatua kweli kweli.
 
Kwani mkuu haiwezekani kuishi kwa laki 3 kwa mwezi?

Unaweza kuishi kulingana na mazingira yako, lakini kulinda hadhi ya mfanyakazi, Kuna sheria ya kubaki angalau na theluthi moja ya mshahara basic. Inapigiwa kwenye basic sio net.
Angalau ubaki na 33% ya basic mkuu. Nafikiri hiyo imewekwa kulinda welfare mkuu. 😊
 
Unaweza kuishi kulingana na mazingira yako, lakini kulinda hadhi ya mfanyakazi, Kuna sheria ya kubaki angalau na theluthi moja ya mshahara basic. Inapigiwa kwenye basic sio net.
Angalau ubaki na 33% ya basic mkuu. Nafikiri hiyo imewekwa kulinda welfare mkuu. 😊
Inabaki 360000 kaka nijilipue au
 

Now you know, hapo 15M hawawezi kukupa. Sababu ukikatwa makato yote sasa, utabaki na 297,500/= toka kwenye 600,000/= take home yako, ambayo basic yake wenda ni Milioni moja, laki moja na visenti.

Maana yake kwa kanuni ya 33% ubaki nayo kwa 600k haifiki, utalazimika upunguze kiasi cha kukopa, labda 10M kwa miaka mitano, ili upunguze riba, ije ikuachie hata 400 hivi, sababu kutakuwa na riba pia kati ya 20-40% itaongezwa hapo kwenye rejesho la mwezi.

Tuhitimishe sasa: Kwa mshahara wako kuchukua 15M kwa kanuni ya 33% + Riba, Muda haiwezekani lazima upunguze kiasi cha mkopo mpaka angalau 9-10M kwa miaka mitano. 😊
 
Kuna ulazima wa wewe kujenga?, kuna ulazima wa kila mtu kuwa na makazi?, hapo unapoishi hupati amani, uhuru ama nafasi kubwa kwa familia na wageni?, au unatamani tu kupata sifa kwa watu kuwa fulani nae ana nyumba.

Mil15 haijengi labda uende mikoani huko au utaishia kujenga kijengo cha hovyo huku ukiendelea kulipa deni the same time salary yako ikiwa ndogo.

Kwanini usitafute wazo la biashara yenye low risk uwekeze kiasi fulani cha pesa ambayo itajizalisha ndani ya miaka kadhaa utakuwa umerudisha mkopo, na biashara/shughuli inayozalisha pesa ya ujenzi huku mtaji(pesa ya mkopo) ikiwa bado Active inazalisha.

Acha mawazo mfu
 

Attachments

  • Screenshot_20260830-011420.png
    Screenshot_20260830-011420.png
    141.1 KB · Views: 8
  • Screenshot_20260830-011357.png
    Screenshot_20260830-011357.png
    142.4 KB · Views: 8
Shikamoni wakubwa zangu.

Mimi ni mtumishi serikalini, mshahara 600K. Nataka nijilipue, nikope benki Tsh. Milioni 15. Zipi faida na hasara zake? Na vipi kuhusu makato yao? Nimepanga nichukue wa miaka 5.

Karibuni.
Nikushauri kutokana na uzoefu wangu. Wengine tulifanya hayo makosa sasa hivi tunaisoma namba. Usije ukafanya hivyo. Anyway, sijui uko mazingira gani, ila nakushauri angalia fursa ya biashara kwanza. Itategemea hobby zako na fursa zilizo karibu na wewe. Kama wewe unapenda biashara na hapo kuna fursa bora uanzishe biashara ambayo walau kila mwezi utakuwa unapata faida inayokuwezesha kujikimu nje ya mshahara. Biashara ikichangamka ndo biashara ije ikujengee nyumba. Kama wewe una hobby na mambo ya shamba au kufuga unaweza kupata shamba hata ekari moja jirani na hapo bora ukope hela kidogo tu ambayo itatosha kununua hiyo eka moja au mbili, Piga fence, inua hata chumba kimoja cha kibabe, pembeni yako jenga hata mabanda ya kuku fuga kisasa baada ya mwaka mmoja au miwili nakuambia utashangaa unapata hela ya kujenga nyumba kubwa kutokea kwenye hizo biashara
 
Back
Top Bottom