Mshana Jr, agent wa Shetani JF?

Mshana Jr, agent wa Shetani JF?

mleta mada mi nakushauri tu kuliko kuonesha shuki au hasira wewe uwe una anzisha threads uwafundishe wana jf juu ya Mungu wa kweli unayemwamini.

wewe kitu kama hukiamini achana nacho unafuatilia cha nini? wengine wanafuatilia tu for fun( sawa na kuona horror movies)
kwanini nione kiuwazi kabisa mtu anawalead wenzie kwenye tatizo nikae kimya......kumbuka sijamshawishi mtu aend dini gani ila nimesema hayo ni mafundisho na matendo yanayomfata shetani....tahadhari kwa mwislamu na mkristo...
 
ya ni kweli ndio maana nami nimekushauri ulete mafundisho yanayotuelekeza kwa Mungu ... usiridhike kuona watu wanapote ukaishia kumshutumu anayewapoteza... uamuzi mzuri ni kuwaonesha njia iliyo sahihi.
 
mwaka 1999 nilisoma kitabu kinaitwa Yoga na Mkristu...nilishangaa mno...nilikinunua bookshop ya kanisa katoliki pale Moshi mjini...nilijiuliza maswali mengi mno...hv kitu hichi inaweza kuunganika na hichi? yaani mafuta yachanganyike na maji...no way....niligoma nikaenda hadi kwa paroko.....karibia nihame ukatoliki...bahati nzuri...tulikubaliana kile kitabu ni upotoshaji na kikaondolewa pale library....MUNGU....hachanganyiki na uovu...na yoga...na meditation...na budhism...na mambo yote ya tripitaka ni evil cult....hayo ndio maamuzi niliyoyafanya
Nianze kwa suala lako kuwa nipo team moja na Mshana Jr. Wewe huwaelewi watanzania wenzako? Je umesahau sisi ni wale watu ukiwaambia usiguse ndo tunagusa tujue kwa nini umetukataza kugusa? Na huoni post yako ilivyowasogeza hadhira kwa fanani wao?
Pili kuhusu kitabu hicho cha yoga na Mkristu, je ulipata kukielewa au ulimkurupukia mtumishi wa Mungu? Je hukusoma kile cha Imani Katoliki na Dini nyingine?
Mimi ni yogis na Pia ni Mkiristu. Ninafanya yogasanas na pranayama ila sifanyi zile yoga nyingine zinazohusisha miungu ya kihindi.
Neno la Mungu linatuasa tusitwezwe unabii au mafundisho, tuchukue yaliyo mema, tuache yaliyo maovu.
Tumsifu Yesu Kristu.
 
kwa signature yako na unayoyaandika...nachelea kusema........unajiingiza kwenye kitu kilichokuzidi umri...na akili...maaana hufatilii unavyoamini...ila unatamani maarifa mapya kutoka kwa binadamu....na unaacha maarifa ya Muumba wako...

Aisee kumbe unaujua umri wangu...............huo ni mtazamo wako siwezi kujenga chuki.
 
mwaka 1999 nilisoma kitabu kinaitwa Yoga na Mkristu...nilishangaa mno...nilikinunua bookshop ya kanisa katoliki pale Moshi mjini...nilijiuliza maswali mengi mno...hv kitu hichi inaweza kuunganika na hichi? yaani mafuta yachanganyike na maji...no way....niligoma nikaenda hadi kwa paroko.....karibia nihame ukatoliki...bahati nzuri...tulikubaliana kile kitabu ni upotoshaji na kikaondolewa pale library....MUNGU....hachanganyiki na uovu...na yoga...na meditation...na budhism...na mambo yote ya tripitaka ni evil cult....hayo ndio maamuzi niliyoyafanya

mimi ni mkristo lakini najua yoga na meditation sio dhambi, what matters ni unafanya kwa sababu gani...
watu wengi hufanya meditation kwa ajili ya afya, ku-settle mind, hata kwenye biblia wapo watu waliokuwa wakifanya meditation wakati wakimtafakari Mungu.
Yoga ni kama mazoezi pia..
 
maishapopote kwanza nikupongeze sana kwa kutoa dukuduku lako ikiwa ni mtazamo wako kwangu kuhusiana na mada zangu
Najua ni una mengi zaidi ya kuandika kunihusu mimi na mada zangu na mambo yote yanayohusiana nazo...nitapenda kuwa bega kwa bega nawe Katika kueleweshana na kujuzana kwa uwazi na kwa mifano stahili huku tukitumia nukuu na lugha za kistaarabu
Naomba ushirika wako wa Karibu Katika hili kwa manufaa ya jukwaa

Nimependa hili jibu...honestly mm napenda sana mada hizo ila sio kwa ajil ya kufanya ila kuelewa na pia burudan...

Usikatishwe tamaaa mshana, naamin huna lengo la kushawish watu ila kuwaelewesha juu ya hayo mambo..
 
Last edited by a moderator:
Akitumia elimu yake aliyoipata nchini Afrika kusini ya Budhisim...na mchanganyo wa vitabu mbalimbali vya kishetani...ujuzi wake katika meditation na ulozi...

Sasa amekua kinara katika mada zote za kishetani hapa jukwaani JF... Na kwa kuwa Jf kila mtu anavutiwa na mada hizi za kutisha na kustaajabisha...basi amepata wafuasi wengi akiwafundisha na kuwaelewesha na polepole kuwaelekeza namna ya kufanya...si tu katika meditation bali pia katika vitu hatari kama viapo vya damu,uzuri wa shetani,eti lucifer sio shetani...na mengine mengi ambayo amekua akiyatoa....

1) Kuweni makini na anayoyasema
2) Na muwaze na kuamua ni kwa faida ya nani mnajifunza haya
3) Mkajiulize je Mungu wenu anafurahia hayo?
4) Na kwann watu wengi mnaotaka sana kujua haya ni wakristu?
5) Muogopeni mno...anataka kuwapotosha imani yenu

Hayo ni maoni yangu..

Utuwache ......wewe inakukera nini?.....Kila mtu ataubeba mzigo wake mwenyewe...
 
Watz wengi hawajui kama kuna elimu zaidi ya shule na dini. Hawajui kama spirituality ni elimu kubwa sana ambayo imekatazwa na walioijua kabla.

Vitu vingine ni sayansi kabisa lakini kwa vile tulifungwa hatukubali. Kwa mfano. Meditation inafundisha kuvuta hewa na kupumua. Sayansi inasema bacteria, virus na microbes huuwawa kwa oxygen.

Wadudu hao hawawezi kuishi penye oxygen.Mtu akikosa oxygen anakufa. Hapa ndipo ukimwambia Mtz kuwa hydrogen Peroxide 35% inatibu magonjwa hatari kama cancer watakucharukia mbaya. Ukimwambia energy ya binadamu inatakona na oxygen hakuelewi.

Madaktari wote hawawezi kukuambiaa hilo kwa sababa nao wako cartel ya madawa ya binadamu ambayo ni mult trillion business.
Through meditation tunajitibu miili yetu na faida nyingi tu.Sio ushetani. After all shetani hakufanyi ufanye dhambi.Anakushawishi tu usimtii huyo unayemwita mungu na usipokubali basi hana madhara. Ukifika mwisho wa kufikiri watu huanza kumsingizia mungu au shetani. These are purely spirits which do not do anything until you do it yourself through your mind

Amkeni elimu sio dini au darasani tu.
 
Haya mambo yalikuwepo tangu kuumbwa kwa dunia kwakuwa navyo ni sehemu ya uumbaji wa Mwenyezi Mungu, hatuna jinsi ya kuviepuka na vitakuwepo mpaka mwisho wa dahari...

Kabla ya kuletewa dini hivi vilikuwepo Enzi hizo binadam aliishi miaka mingi sana kuliko sasa
 
Mleta Mada Hajui Hata Kwenye Biblia Kuna Meditation,hajui Shetan Ni Nani ? Hajui Kwa Nin Meditation Tatu Unasoma T Vitu Na Kuvitolea Hukumu Bila Kuelewa Ama Kuvitafakar Nimalize T Kwa Kusema Kama Unaon Ndugu mshanajr Anapotosha Anafundsha Kumwabudu Shetan Basi Tufundishe Njia Iliyo Njema, Nisawa Na Kumkataza Mtu Asitoe Ushuhuda Kuhusu Ujambaz Kwamb Watu Watakuwa Majambazi.
 
Last edited by a moderator:
Wale wale walio curious kufuatilia mada zake! Wao ndo wanaamini na kufuata!
Kila mtu ana kile anachoamini.
 
Akitumia elimu yake aliyoipata nchini Afrika kusini ya Budhisim...na mchanganyo wa vitabu mbalimbali vya kishetani...ujuzi wake katika meditation na ulozi...

Sasa amekua kinara katika mada zote za kishetani hapa jukwaani JF... Na kwa kuwa Jf kila mtu anavutiwa na mada hizi za kutisha na kustaajabisha...basi amepata wafuasi wengi akiwafundisha na kuwaelewesha na polepole kuwaelekeza namna ya kufanya...si tu katika meditation bali pia katika vitu hatari kama viapo vya damu,uzuri wa shetani,eti lucifer sio shetani...na mengine mengi ambayo amekua akiyatoa....

1) Kuweni makini na anayoyasema
2) Na muwaze na kuamua ni kwa faida ya nani mnajifunza haya
3) Mkajiulize je Mungu wenu anafurahia hayo?
4) Na kwann watu wengi mnaotaka sana kujua haya ni wakristu?
5) Muogopeni mno...anataka kuwapotosha imani yenu

Hayo ni maoni yangu..
Zima data
 
Back
Top Bottom