Mshana JR amebadilisha maisha yangu, vijana wenzangu mtumieni mshana JR kabla hajaondoka duniani


Hongeera kwako na kwake Mshana Jr
 
Mwaka 2020 nilipitia hali ngumu sana kiuchumi hali iliyonilazimu kuondoka nyumbani.

Huko nilipoenda, maisha hayakunipa furaha. Nilikuwa na simu smart nzima kabisa, ilinilazimu kuiza tsh 8,000 (elfu nane) ili kukimu familia. Wakati huo wife kajifungua ana wiki 2 tu na korona ndio imepamba moto (ilikuwa wiki ya kwanza ya mwezi wa nne). Mtu ambaye alikuwa akinitia moyo ni Mshana Jr


Ilifika mahali nikakata tamaa sina tumaini. Nilimuomba niende dar angalau anisaidie nipambane. Alikubali, nikakopa nauli nikaanza safari. Ninao ndugu dar lakini walijitenga nami,. Lakini huyu Mshana alinipokea, alitoa kiasi cha pesa tsh 750,000 ninunue vifaa vya kazi (mtaji) na tsh 100,000 kama kodi ya frem. Sio kwamba yeye ni tajiri saaaaaana, hapana. Alitoa pesa ambyo haya yey kwa wakati ule alikuwa akiihitaji zaidi. Japo kikazi kuna sehemu hatukufika malengo, lakini Mungu alinisaidia kuvukq kipindi cha mpito kupitia kwa Mshana. Brother alinipambania sana wakati hata nyumbani kwetu hapajui zaidi ya kuniona jf.

Ilinilazimu tena kulikimbia jiji baada ya mambo kwenda mrama, lakini angalau nilivuka wakati mgumu. @mshanni hazina, na kutoka moyoni bila unafiki wala kumkweza nasema Asante, pia aniwie radhi kwa changamoto zilizojitokeza nami ni mwanadamu.

Mbali na kutoa pesa yote hiyo ambayo nikiweka na matumizi mengine ya mwanzo inazidi milioni moja na ushee, sijawahi kuona ama kusikia akijinasibu sehemu yoyote. Anaishi kama vile hakuna kitu amefanya. No camera, No show off. Wema ni akiba brother, kuna siku utapokea mafao hapa hapa duniani. Mungu akutunze na akupe mwisho mwema wenye kuona matunda ya ulichokipqndq kwa watu na mavuno yako yakajae na kusukwasukwa. Kazi za mikono yako zibarikiwe.

NB: sijatumwa kuandika haya, wala sijaandika haya kusifia. Nimeamua kusema ya moyoni ambayo sikuwahi kuandika popote pale. Na kama nitakuwa nimemkwazq yeyote pia, anisamehe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…