Mshana JR amebadilisha maisha yangu, vijana wenzangu mtumieni mshana JR kabla hajaondoka duniani

Mshana JR amebadilisha maisha yangu, vijana wenzangu mtumieni mshana JR kabla hajaondoka duniani

Habari wakuu!

Nikama wiki mbili zimepita nilipata depression, frastruation na kukata tamaa kabisa kwenye Maisha, Hali iliyopelekea kutaka kunywa pombe kuvuta bangi nikiamini ntakuwa sawa.

Nilituma post humu JF juu ya Hali ninayopita Lakini cha ajabu ndugu yangu mshana jr alichukulia uzito wakati ninaopitia, akanambia fanya tuonane, nilifurahi Sana mana ilikuwa ndoto yangu kuonana na mkuu mshana jr.

Mazungumzo yalikuwa ya masaaa 3 maeneo X hapa dar es salaam.
Aisee nilipata counseling ya kutosha
Kuhusu

1.Afya
2.Imani
3.Mahusiano.
4.Uchumi

Aisee baada ya hapo nimekuwa MTU mpya.

Vijana wenzangu 20 kuendelea mtumieni mshana jr kabla hajaondoka duniani.
(Pokea Maua yako mshana jr)
Mimi Sio babalevo
Mimi Sio mwijaku
Mimi Sio doto magari

Mimi ni mtupori_tz
Hongera zake
 
Mie siamini kama jamaa anaweza kuwa kitengo na hata kama ni kitengo basi wameajiri mtu mwenye maarifa mengi ya kusaidia watu na ana roho nzuri pia hivyo sio mbaya cha msingi yeye sio kama wale wasiojulikana!
Sifa ya kitengo ni kufanikiwa kutojulikana, na lazima awe na mambo mengi ya kukuvutia mpaka unajivua ID yako ya JF, na kawaida kama kuna issue, yeye atatoa pasi tu, Mukwala anamalizia
 
Back
Top Bottom