Mshana Jr ndiye GOAT wa JF

Yaani wanaume wengine wamekuwa kama mademu siku hizi. Hivi kama mtu anasifiwa kwa mazuri anayofanya kuja kumchafua unapata faida gani hizi ni tabia za kike.

Naonaga hata huyu dogo GENTA watu wakimsema sasa hata ukimsema unafaidika nini. Kama mada zake hauzikubali unauchuna tu unapita hivi, hiyo imekaa KIUME zaidi

Members wote humu iwe ni maarufu na wasio maarufu wana umuhimu wake. Uwepo wao na uchangiaji wao ndio unafanya JF isonge

Tujifunzeni kuwa dis-minder wanetu
 
Abarikiwe Mshana Jr
 
Sina cha kusema nilijukuta namkubali sana.
 
Asante sana kwa compliment Mpangumbe napokea kwa shukrani na unyenyekevu mkuu[emoji1545]
 
Yaani wanaume wengine wamekuwa kama mademu siku hizi. Hivi kama mtu anasifiwa kwa mazuri anayofanya kuja kumchafua unapata faida gani hizi ni tabia za kike.[emoji23]

Mzee wa kupambania maisha yana mengi ya kutufunza na kwenye uzao wa kiumbe mwanadamu kuna mengi zaidi yenye kufunua uhalisia wa ndani ya mtu hasa kwenye kipengele kinachoitwa CHUKI!
Kwa hali yoyote unapokutana na mtu physically au non physically AKAKUPENDA/AKAKUKUBALI kwa lolote lile pokea kwa moyo wa shukrani kisha mshukuru yeye na Mungu pia.. Lakini pia unapokutana na mtu hasa huku mitandaoni halafu kwa sababu binafsi akakuchukia, pokea hilo kwa tafakuri kuu maana chuki ni matokeo hasi ya
.Wivu
.Kijicho
. Husuda
. Kushindwa nk nk!

Washindwa wengi huwa na tabia zinazofanana .. Maana wamejaribu kwa NGUVU zao zote kuwa kama wewe lakini wakashindwa.. Ni watu waliojawa na fukuto la sononi na vinyongo . wanatamani ushindwe washangilie sana.[emoji23]
Hakuna kitu kinachomuumiza hater kama kumdharau na kumpotezea.. Anapoona ID yako roho inamruka anajiona mchafu na juha na mpuuzi wa viwango vya juu sana! Sasa kujiponya na haya maumivu huja na reply za kudiss na uzushi[emoji16]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…