Mshikaji wangu ameanza kucheza forex, kila siku anauza vitu kidogo kidogo

Mshikaji wangu ameanza kucheza forex, kila siku anauza vitu kidogo kidogo

Status
Not open for further replies.
Ni sawa boss stop loss inaunguza account ila si kwa mara moja, huwezi kusema stop loss iliondoka na account ina maana aliiweka wapi? Mimi kwa sasa acha tu niendelee kutumia nitaacha nikiwa guru kama wewe, hakuna kitu kinaniumaga kama ku cut loss

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndio maana nikasema ukitumia risk management nzuri hata kuunguza account itakuwa ngumu sana sana.
Mtu ana mtaji wa dola 100 anatumia lot size ya 0.09 hapo anatarajia nini. Ila kama akienda na lot size ya 0.01 au 0.02 with trend lazima atusue.

Hata kama ikienda against ni ngumu kuunguza.

Nikwambie tu Stop loss ni mbinu ya big financial institutions kwenye forex kutupiga sisi retail traders. Nakuomba utafute kitabu cha Quoter theory kilichoandikwa na Illian Yutov (Mtaalamu). Ujinze kutrade kwa Quoters

Sawa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna mtu Jana nilimuomba aweke taarifa au Salio lake la bank na Mimi niweke Salio la account yangu ya Tickmil, aliishia kuniita matusi ya kila namna.

NB. Si kwamba Mimi ni tajiri hapana. Ila Forex inanipa Pesa ambayo naamini kuna watu wanatuita wajinga hawawezi kuipata mpaka watakapopewa Pesa za pensheni.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahahaaaa... Umenikumbusha mwaka janaa nikiwa chuo, wenzangu wamesaini ka boom ka 500k mimi wala sina muda nasubiri watu wote wamalize, nilovyoulizwa kwanini sina haraka nikaingia kwa Templer nikawithdraw 900k(400$+)..[emoji23][emoji23][emoji23]
Jamaa wakaanza kunitukana....

NB; Sio tajiri lakini sina presha yoyote mtaani sababu ya ukosefu wa ajira.
Nakomaza knowledge yangu kuijua forex kiundani zaidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ha ha ha pole sana. Hukuwa na hawa magwiji wa JF ambao wao kila siku wanavuna pesa? Hivi ukila hela unamla nani na ukiliwa nani anakula hela yako?
Hili swali niliulizaga nikaambiwa ukiunguza account inakuwa ya broker lakini hawakunijibu ktk kula na kuliwa labda leo nitapata jibu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cheza na ww ili usiandikie mate nakati wino upo.

Prondo ni heri ukishindwa sana kufanya biashara yoyote basi uwe kama wale Mateja day worker wanaopiga debe kuhusu ukonda pale stendi Rafiki.

Hakuna utapeli unaoshamiri kwa kasi sana kama hizi biashara za mitandaoni.

Kuna Rafiki yangu m1 yuko Mwanza alinishawishi niingie QNET kwa mbwembwe nyiiingi za mafanikio ya rafiki zake nilitaka kuingia kwa 6,000,000/= lakini bahati mbaya nilipungukiwa kiasi cha 900,000/= na nilijitahidi kuitafuta zaidi ya wiki 1 niliipata kukamilisha 6,000,000/= lakini roho yangu ilisita sana.

Kifuatacho sasa hivi yule Rafiki yangu aliuza gari, nyumba na hadi sasa hivi anaishi kama shetani kwenye nyumba za kupanga.

Tafadhali kijana fanya biashara halisi(physically contact with customers) lakini hizi biashara za mitandao(online businesses) ni utapeli mtupu kwa 100%.

Sent using Jamii Forums mobile app
Qnet ni wezi
 
Hili swali niliulizaga nikaambiwa ukiunguza account inakuwa ya broker lakini hawakunijibu ktk kula na kuliwa labda leo nitapata jibu

Sent using Jamii Forums mobile app
Forex ni biashara Kama biashara zingine. Ina profit na loss...

Hivi biashara ya shares ikiwa na loss hizo Pesa zinakuwa zimeenda wapi ?? Ukiweza kunijibu hili swali basi utakuwa kwenye njia nzuri ya kujua loss za forex zinaenda wapi.

Mimi sijui na sichezi hiyo michezo (Kuna mtu kaita forex mchezo humu). We kama ni trader mzuri si unijuze kuliko kunipa homework umri huu

Pole sana ndugu yangu, bora wewe umekiri hujui. Nakuomba tu ujitahidi kujifunza kusoma literatures za forex zipo tele mtandaoni.

Naamini utaelewa vizuri sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom