Mshikaji wangu ameanza kucheza forex, kila siku anauza vitu kidogo kidogo

Mshikaji wangu ameanza kucheza forex, kila siku anauza vitu kidogo kidogo

Status
Not open for further replies.
Dah mpaka hapa inabidi tu uendelee kusoma, ila km unasoma peke yake tu bila kupractise kwenye demo itakuwa kazi bure...

Simply buy when price is low and sell when price is high...

Sasa hapo ndo inatakiwa ujue high ni ipi na low ni ipi

Sent using Jamii Forums mobile app
Yani hilo ndo balaaa... Na pia kuna siku za kutrade mkuu...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Heeh! Kumbe akina mkuu wa kaya Maxence Melo na Ruge walipigwa vikali? Pole zao jamani.
Mwambie aache upuuz kuna ndugu Yangu alikuja kunambia hii kitu ya forex nikamwambia hii kitu naijua zaman sana kabla yako kuna akili kubwa inaitwa Ontario iliileta jf watu wakapigwa akiwemo mwenye jf mwenyewe bwana mello na akili kubwa mwingine anaitwa ruge naye alipigwa pia

Biashara ni uzalishaji mali na Huduma hizi zingine ni majanga tu

Ontario bhana nukuu yake moja kajamaa kanasema hii biashara ya forex hata bank hawaijui na hawatak kabisa uijue, duh salute sana ontario

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu wanapaswa kufahamu kuwa Forex ni tofauti kabisa na hizi network marketing kama foreveriving n.k. Hakuna kumleta mtu na mtu amlete mtu. Hii ni biashara kama ya beuro de change sema tuu yenyewe unakua online wakati yale maduka yanakuwa physically.
Forex ni biashara kama biashara nyingine , kuna kupata faida na wakati mwingine kupata hasara kama mambo yakienda vibaya. Kwa msingi huo niwaulize ni biashara gani ambayo mtu hutegemea faida tuu bila kufikiri kua pia kuna uwezekano wa kupoteza. Wangapi wanapoteza ktk biashara ya tikiti, wangapi wanapoteza ktk biashara ya nafaka n.k. Sasa kwa nin mtu akipoteza ktk biashara ya Forex inakua nongwa?
Forex ndiyo soko kubwa kuliko yote duniani ambapo daily turn over yake ni takribani dola trilioni tano. Taasisi kubwa na mabenki duniani znafanya biashara hii. Retail traders kama mimi na wewe tuna mchango mdooooogo sana ktk forex almost negligible. Volatility ya soko ndo itakupa faida kama soko likienda upande wako and vise versa.
Ndugu watanzania najua sisi ni wavivu saana kusoma, lakini nivema kasumba hii itutoke tujifunze vitu kabla ya kufanya siyo mara umekimbilia kulima mpunga, tikiti, mara umekimbilia ku tradr forex bila kusoma ukaijua ki undaaani kabisaa.
Halafu syo kila biashara kila mtu ataiweza au ataipendeza, kuna wengine wanapenda kuuza mtumba , wengine mafriji na wengine ku trade forex ndo wanapenda na ni vyema kufanya ukipendacho na usimdharau afanyae usichokipenda maana mwisho wa siku ni mkate ukae kwenye meza. Mimi siyo mkufunzi wa forex lakini ukitaka nitakuelekeza wapi ukasome maana maatifa ni kitu cha muhimu saana hata kama usipotaka kuwa trader lakini kujua vitu ni muhimu sana.

Sent using Jamii Forums mobile app

Mkuu naweza kupata hayo madesa wapi? haya ninayosoma huku tunachanganyana tu sijui utapeli najiuliza inakuaje utapeli wakati unauza na kununua mwenyewe?
 
Shida ya watanzania ni moja wanakurupuka na hatupendi kusoma wote wanaiponda forex na wanaoisifia forex hawajui hata kirefu chake (foreign exchange) na sio mchezo wala sio njia yoyote ya kupata utajiri ni soko la kubadili fedha za kimataifa....
 
Sizungumzii forex bali hilo jina au neno "walokole au ulokole". Neno hilo halina maana wala uhusiano na sisi TULIOMKIRI NA KUMPOKEA YESU KRISTO ALIYE HAI KAMA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YETU. Hilo ni jina au neno analotumia Shetani na mawakala wake kutaka kuudharirisha WOKOVU WETU. Na kwa kweli kwa kiasi fulani kafikia lengo lake ingawa hatafanikiwa milele. Sisi SIO WALOKOLE bali SISI NI WANA WA MUNGU TULIOPOKEA NEEMA YA WOKOVU, NI WATU TULIO OKOKA.
Nyie ndo wale mkikanyagwa bahati mbaya afu mkaambiwa sorry mnarusha maneno na ngumi kabisa...jamaa si kasema mniwie radhi walokole au inamaanisha nini hiyo sentensi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi forex ina shida gani? Kama unanunua kwa bei ndogo unauza kwa bei kubwa hapo shida inakuja wapi?
Hapo ndio utapeli ulipo lala sasa
unanunua nini kutoka kwa nani na ukafanyie nini
na una uza kwa nani na akafanyie nini
ni nani ana determine bei kupanda na kushuka na anatumia vigezo gani?

akili za kwako chamganya na zakuambiwa
 
Forex bila knowledge inaitwa betting, a.k.a kamari, forex with knowledge inaitwa trading, so tafuta forex type yako acha kuconfuse jamii, wakati unakamia hapa forex ni kamari makampuni yoooote makubwa duniani unayoyajua wewe yanatrade stocks zao kwenye forex market na share zinapanda na kushuka kutokana na currency volatility, sasa we kaa na knowledge ya easy cash thru forex trading uje uuze nyumba ya mdingi akutoe kafara kabisa, hizi currency usd, chf, jpy, eur nk zinamovement zake km unaweka tu pesa yako hujui huko duniani kunaendelea nini we unaloose, broker wako anakenua meno tu anataka uendelee hivyoooo hivyoooo na strategy yako ya kuweka hela bila taarifa yoyote, kisha urudi mtaani uza ulivyonavyo urudi tena uteketeze

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo ndio utapeli ulipo lala sasa
unanunua nini kutoka kwa nani na ukafanyie nini
na una uza kwa nani na akafanyie nini
ni nani ana determine bei kupanda na kushuka na anatumia vigezo gani?

akili za kwako chamganya na zakuambiwa
Kwenye forex hatuuzi bidhaa shida nyie mmeesha danganywa na wajanja wametumia jina forex kuwatapeli

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo ndio utapeli ulipo lala sasa
unanunua nini kutoka kwa nani na ukafanyie nini
na una uza kwa nani na akafanyie nini
ni nani ana determine bei kupanda na kushuka na anatumia vigezo gani?

akili za kwako chamganya na zakuambiwa
Mkuu unaonekana uko dunia ya mbaaaaaaali sana nyuma kama miaka 40 nyuma ya wakati. Dunia ya sasa ipo ktk information age ndugu, maarifa mengi yapo ktk mtandao. Hivi uliwahi hata ku google neno Forex trading hata siku moja?
Jaribu kuyatafuta maarifa mtandaoni mkuu usitegemee sana maarifa pekee ulosoma shule maana muda si mrefu yatakua useless kwa sababu ya kasi ya teknolojia ya sasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom