Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
😂😂😂😂😂😂 kwahio jamaa afurahie tu maana anaonekana hata kazi hana.Happ Kuna faidambili. Kwanza atalipa fadhila kwa kuwalea n kuwasomesha wajomba zako mzigo ambao pengine mngeulea ninyi Kama familia endapo angezalia home. Pili na wewe umepata chansi ya kwenda kulala sebuleni kwa shemeji huku ukiangalia TV usiku kucha Kama wenzio wengi wanavozililia hizo nafasi.
Hana kazi Wala demu ndio anaona gere dadake anafaidi.😂😂😂😂😂😂 kwahio jamaa afurahie tu maana anaonekana hata kazi hana.
Mdogo wako alishafikisha umri wa kuolewa na amemaliza masomo au amemkatisha? Japo unasema amemuoa, na baadae unaongelea kuhudhuria harusi yao, inaonesha hawajaoana ila wameshapeana mimba.Hili ni jambo la kushangaza sana, huyu jamaa kwao walikuwa masikini alafu nyumbani kwao ni mbali na shule, hivyo kwa kuwa tulikuwa marafiki tulioshibana na discussion tulikuwa tunafanya pamoja nikamkaribisha nyumbani kwetu akawa kama mtoto wa familia yetu kabisa.
Baba yangu alikuwa anamlipia ada, nguo za shule kuanzia form 3 mpaka form 4 amenunuliwa na baba yangu cha ajabu baada ya kumaliza chuo na kupata kazi amemuoa na kumtundika mimba Dada yangu wa mwisho kweli hii ni sawa!
Niende kwenye harusi yao au nisiende? Nimsalimie au nisimsalimie?
Cha ajabu baba yangu na mama yangu wamekubali umuoe Dada eti kisa wewe ni Dr ataishi maisha mazuri!
Kwa hili rafiki yangu hufai kabisa na sijui umekula maharage ya wapi .
Sent using Jamii Forums mobile app
Kweli kabisa mkuuWatu wengi wanaonekana kuunga mkono jamaa kwa alichokifanya eti kisa anaoa, stupid.
Hawa ni watu ambao wako tayari hata washikaji wao wawaatafune mama zao na kama watawaoa haina shida.
Kuoa bado haku-justify ujinga alioufanya mshikaji.
Huyu mtu alikua anachukuliwa kama kaka, ndugu wa familia, wazo la kuanza kula wadogo zake hata kama mwishoni anaoa alilitoa wapi kwanza?
Hata kama ningekua mimi, hata kama anaoa ila ile heshima niliyokua nampa awali naiondoa yote.
Mimi binafsi hiyo harusi uwezekano wa kutokwenda ungekua mkubwa sana.