Mshituko: Rafiki yangu tuliyeshibana unamuoaje Dada yangu?

πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ kwahio jamaa afurahie tu maana anaonekana hata kazi hana.
 
DAAH na HAYO mapenzi yalianza kitambo sana sema tu niliona jau kukwambia ndio maana jamaa akahamia hapo kwenu

Alikuwa ananihadithia mkisoma mkichukuliwa na usingizi mwamba anaamka anaenda tafuna mdogo wako

ila shukuru bora ameoa
 
Watu wengi wanaonekana kuunga mkono jamaa kwa alichokifanya eti kisa anaoa, stupid.

Hawa ni watu ambao wako tayari hata washikaji wao wawaatafune mama zao na kama watawaoa haina shida.

Kuoa bado haku-justify ujinga alioufanya mshikaji.

Huyu mtu alikua anachukuliwa kama kaka, ndugu wa familia, wazo la kuanza kula wadogo zake hata kama mwishoni anaoa alilitoa wapi kwanza?

Hata kama ningekua mimi, hata kama anaoa ila ile heshima niliyokua nampa awali naiondoa yote.

Kupata tu wazo wa kuwatafuna ndugu zangu pale nyumbani baada ya mimi kumkaribisha ni uvunjifu wa heshima na uaminifu.

Mimi binafsi hiyo harusi uwezekano wa kutokwenda ungekua mkubwa sana.
 
Hapo ndio udugu umekolea na pengine ulikuwa mpango wa mzee wako toka mwanzo alivyokuona wewe boya akaona atafute mtoto mwingine wa kiume mwenye akili atakae simamia familia na atakuwaje mtoto wake bila kumuozesha binti yake.
Acha uboya huo ulikuwa ni mpango mkakati wa mzee na dada alijulishwa na mama yako toka mwanzo.
Mbali na hayo nampenda dada yako kamwe sitamtesa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mdogo wako alishafikisha umri wa kuolewa na amemaliza masomo au amemkatisha? Japo unasema amemuoa, na baadae unaongelea kuhudhuria harusi yao, inaonesha hawajaoana ila wameshapeana mimba.
Kwa ufupi, mlikuwa msaada kwa familia yao, mtapata baraka kwa wema wenu, na pengine hata udaktari umetokana na msingi wa elimu na malezi mliyompa.
Ukiwa mtu mzima utakuja kugundua kuwa asilimia fulani ya ndoa, huchipua kutokana na ujirani na kuingiliana kwa wakazi wa eneo fulani. Hivyo kukulia hapo kwenu ndio kumepelekea apate jiko hapo hapo, na mdogo wako apate mume hapo hapo.
Rafiki mlioshibana sasa anakuwa ndugu, hakuna ubaya.
Nina imani na wewe ulipiga hatua nzuri kimaisha kama rafiki yako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kweli kabisa mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe jamaa wa ajabu sana. Jamaa amefanya vema kwani hata wazazi wenye binti yao mpendwa wamebariki wewe kaka tu unamind. Tena dada yako kuolewa na jamaa yako unayemjua ni jambo zuri. Dumisha urafiki na shemeji yako acha utoto.
Uende usiende ndoa itafungwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…