Fanton Mahal
JF-Expert Member
- Mar 22, 2024
- 1,597
- 4,661
- Thread starter
- #101
Alianza tuTunatakiwa kubalance Story yani yeye alianza tu kubadilika? Lazima kuna mahali uliteleza
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Alianza tuTunatakiwa kubalance Story yani yeye alianza tu kubadilika? Lazima kuna mahali uliteleza
Hajagegedua huko inje saa hzYesu na Maria na Yosefu nimekuhurumia ghafla hao wakiwa na jambo lao mpaka wakufyeke ndio maana jamaa yako kashtukia mchezo soon utakua RIP mkuu kua makini ilikuajekuaje ukamtia vitasa?
Ni kwelTafuta ka toto ka 2000 enjoy maisha,,,, ! Wanaume tunakufa mapema kwa stress!!!! Huyo usimfanyie mabaya, bado analea wanao,,,just move on
Hiyo nzuri basi katika maombi yako ... Uwe unaomba hii zaburiYah, nafunga 24 hrs every Tuesday na 12 hrs every Thursday
Nilikuta picha za hovyo kwenye simu yake, na video anaogelea kwenye swimming pool na wanaume1. Babako katukanwa mbele yako, nawe bado unamsihi arudi.
Arudi wapi?
2. Na kwa nini ulioa mtu aliyekuzidi umri?
3. Hizo ishu zinazohusu uaminifu ni zipi? Unachapiwa na bado unamng'ang'ania?
Daaah!! Hawa watu sijui wanakuwaga na shida gani......Nilisha hama, mwezi huu kwenda ku chill mwanza nihamishe harakat huko, alipo jua hilo ndio moto wa police ukaanza, nahisi hataki na mimi ni move on
Ni kweliAnhaa nimeshaisoma hii game, hapa unachoogopa ni mama watoto kupigwa juju !
Zaidi ya sanaUsihofu mkuu atakaa sawa juju ikimuingia vizuri inaonekana saivi ana kiburi pro max na anakudharau sana zaidi ya sana
Hamna, hatafanikiwa, nilikua najaribu peaceful ways kuona kama zita work outHuyu jamaa kama si bwege basi ni boya, huyo Mwanamke atakuendesha mpaka akuue
Sijui kwa nini imenijia taswira ya mheshimiwa spika🤣🤣🤣 Pole.Mnyakyusa
Ahahahah...yeye sio mbaya kama spika, ana nyama nyama angalau za kushika na tako pia lipoSijui kwa nini imenijia taswira ya mheshimiwa spika🤣🤣🤣 Pole.
juju ni vitu ambavyo vipo kikubwa tu asife muache apate dozi spesho ya sangoma, mkuu hio itamuweka sawa medulla we mwenyewe utarudi hapa kuanzisha uzi wa kushukuruNi kweli
Zaidi ya sana
Mwanamke anajua exactly kadi gani azicheze ili mwamba acheze ngoma yake.Ushauri makini sana aufuate, watoto isiwe sababu ya yeye kuendelea kupalilia jambo ambalo linahatarisha maisha yake.
Hakuna kitu kinaitwa uchawi wala kulogwa kwa mujibu wa mimi mwenyewe.Wakuu heshima kwenu.
Sipendelei sana kuingia deep kwenye mkasa mzima unaoihusu familia yangu , especially mimi na wife.
Ila kwa kifupi tu, wife alizingua big big big time (usiulize nini maana ni ishu serious sana inayoweza husishwa na suala la uaminifu moja kwa moja)
Na nilipotaka maelezo toka kwake, akanijibu shit kwel kweli, nikaona this is too much, nikamchapa vizuuri tu.
Ila akili ziliponirudia nikaona nimefanya sio kitu kizuri, nikamuomba radhi.
Huu ukawa mwanzo wa mambo mengi sana, wife na ndugu zake waka kaa kikao, wakamshauri kuwa aachane na mimi. Akaanza harakati za kutekeleza maazimio ya kikao chao
Baada ya 10 days, aka force akatafuta pf3, akatafuta cheti cha daktari (alihonga).
Baada ya hapo, akaenda polisi, akakata RB (koote huko alishatafuta watu yeye akisaidiana na ndugu zake). Haya yoote yalikua yanafanyika bila mimi kujua chochote, nimekuja kuyafaham too late.
Akatega siku niko ofisini, nimeondoka tumeagana vizurii kabisa kwa vicheko (Nisijue moyoni anaendelea na mipango ya kuniingiza kwenye 18 zake).
Ile narudi home, nakuta ,kabeba watoto wangu, kabeba hati ya nyumba na eneo, kabeba card ya gari na vyeti vyake vyooooote vya taaluma na ajira (mtumishi wa serikali yeye) akasepa.
Nikaja gundua kuwa ni kaka yake alimfuata.
Basi siku bother kumtafuta. Nikatoa tu taarifa nyumbani kwetu kwa wazee.
E bwana ee, baada ya hapo, nikaanza kupelekewa moto,
- nikapelekwa gender desk police kuwa nimetelekeza na situnzi familia na mimi ni mnyanyasaji, nikapangua mashtaka kwa hoja na vielelezo, kesi kule ikamgeukia yeye, hata hivyo nikamuomba radhi na kumsihi tuyamalize, akagoma kabisaa. Hakuridhika
- wazee wangu wakaja, wakakaa kama familia na familia yake, mbele ya kikao, akamtusi baba angu, akatamka kuwa hanipendi wala hanitaki tena, na hata watoto sitakaa nije kuwaona tena. Nikamsihi, kwann unafanya haya hali wewe ndio sababu ya yote haya mpaka nikakupiga , akagoma katakata, kikao hakikuisha na suluhu ila ndugu zake wakasema hii ndoa lazima ivunjike. Hakuishia hapo
- akanipeleka baraza la usuluhishi la kata, hapa lengo lake ni kupewa form no.3 ili akafungue shauri la kudai talaka mahakamani. Wale wazee wa baraza walipotusikilizaa, wakamuona hana hoja, wakamuuliza wewe ni nani aliyeingilia kati na anakuendesha na kukudanganya? Mmezaa watoto wa 4, unataka talaka ya nini?? Wakamwambia, nenda kajifikirie upya ndio urudi tena, tutakupa. Huku nako akaonekana hana hoja ya msingi, na bado nikawa namsihi aghairi maamuzi yake ila waaap. HAKURIDHIKA
- juzi kati, niko mkoa mmoja kanda ya ziwa, napigiwa simu na mkuu wa upelelezi , kuwa nahitajika kituoni.
NIkasafikiri mpaka dar, kufika na kureport, namkuta wife pale, nikakamatwa na kutiwa ndani ( lockup). Hapo polisi wakachukua funguo za nyumbani kwangu wakampa wife, akaenda akasomba vitu vya ndani, akaondoka kwenda kupanga na kuanza maisha mengine akiwa na watoto, ambao toka alipokimbilia kwao nao mwezi November 2024.
- nikatoka nje kwa dhamana, hata muda huu niko chini ya dhamana na ninatakiwa ku report kituon after every short period of time.
SASA KISA KINAANZIA HAPA JAPO NI KIFUPI
Currently ,nikagundua wife kadhamiria kunikomesha, kazi zangu ni za kusafir, ila kwasasa siwez enda safari zaidi ya week kwasababu natakiwa kituoni kila mara.
Baada ya kuondoka home, imani yangu kwake ikatoweka nikahisi huyu asije nifanyia kitu mbaya, kwa muda nikawa nalala lodge, hiz zote ni gharama natumia.
Kazi zangu ni kama zimekwama.
Kesi yangu kimsingi ni kama imeshatoka polisi, ila chaajabu ni kwamba hawataki kuipeleka mahakamani, wananisumbua sana na masuala ya ku report kila mara kituoni.
Yale matumaini yoote ambayo nilikua nahis huenda hiz za wife ni hasira tu, nikaja gundua she is seriously intending to destroy me.
Shida yangu kubwa, mimi siiwezi michezo ya ubaya ubwela. Mimi ni wale ambao Yesu alisema "mtu akikupokonya koti lako, mwachie na kanzu, pia, akikuambia twende maili moja, wewe nenda maili 2". Kwakifupi, mimi mambo ya kulipiza ubaya siyawezi.
Sasa siku moja nikiwa very frustrated, nikakutana na mwamba mmoja ni mshkaji wangu, class mate tukiwa chuo. Katika hapa na pale nikamsimulia madhira kwa uchache aliyonitendea shemeji yake. Huyu jamaa anamjua wife maana mimi nilizaa mtoto wa kwanza na huyu mama tukiwa chuo mwaka wa kwanza, na ile hustle ya malezi na matunzo walikua wanaiona maana tulikua tuna kaa hostel moja kigamboni nikiwa mwanafunzui ninaye survive kwa pesa ya boom.
Bas nilipomsimulia (hapo kabla sijawekwa ndani) , jamaa akasikitika sana. Akanitia moyo akasema yatakwisha.
Ila mshkaji niliona kalichukulia lile suala kwa uzito sana. Alitamka neno moja tu "ni yule shemeji uliyekua unamhangaikia enzi zile tukiwa chuoni??? (Over 10 years ago)"
Nikamwambia ndio huyo huyo nilioa.Basi jamaa akafikiria akasepa.
Sasa jana jioni nikiwa facebuk, akaniona online, akaniuliza "braza kimya sana, lile jambo vipi linaendeleaje?"
Nikamwambia "jambo limekaa vibaya sana, hapa penyewe nimetoka lockup nina siku 2 tu, niko nje kwa dhamana, shemeji yako kaamua kuninyoosha"
Jamaa hakua na maneno mengi, akaniuliza "hivi shemeji majina yake ni nani?"
Nikamtajia.
Akaniuliza anafanya kazi maeneo gani? Nikamtajia.
Akasema "braza, nitahangaikia hili suala kwaajili yako,wewe ni ndugu yangu tumetoka mbali, siwezi ona unateseka namna hii kisa mwanamke yeye kakaa tu ana enjoy na mmezaa watoto"
Nikauliza , "una plan kufanya nini"
Akasema "huyu, ningepata mchanga wa mahala alipokanyaga nyayo zake ingekua vizuri, ila sio kesi kwakua ushaniambia anafanya kazi maeneo gani, hii pia itasaidia"
Hapa nikashtuka, nikamwambia "braza , naomba kwanza utulie, next week natakiwa ku report kituoni pamoja na yeye, baada ya kusikia nini kinazungumziwa huko nitakupa feedback kwanza"
Akasema "sawa, na kabla hujakwenda huko, nitakuambia nini cha kufanya"
Wakuu, hapa kwa akili yangu ndogo kabisa, nikajua tu kuna "juju" linataka kuandaliwa, wife apigwe "kimbola/kombora" ila nikasema kwanza "hold on".
Wazee mimi si mtu wa mambo hizo.
Na hata kama huyu mama kashaamua kunipiga pini, ila bado tuna watoto nae na anao yeye, hata kama yeye kanikusudia mabaya, honestly mimi bado namuwazia mema.
Japo kwasasa nishaona kuwa hakuna dalili wala matumaini yoyote ya sisi kuwa pamoja tena, na nimeshaanza ku move on, na yeye alishaga move on kitambo i think ndio maana ananitenda ubaya huu.
Mke wa miaka 15, tulioana na kuzaa mapema sana, maana mimi ndio kwanza sasa nina 35 yrs na yeye 36 yrs.
Ila kiukwel kanikusudia mabalaa mabaya sana, na mshkaji wangu anataka kupambana nae kupitia teknolojia ya "anga za juu", ila mimi kiukwel, I DO NOT WISH HER ANYTHING BAD".
Ungechukua uamuzi ganu juu ya msaada kama huu ninaopewa na mdau wangu?
Jioni njema
Namaanisha vile anavyojipenda na kujikuta sistaduu.....Ahahahah...yeye sio mbaya kama spika, ana nyama nyama angalau za kushika na tako pia lipo
Solution: Uliza swali moja, anataka nini kifanyike ili muende your separate ways? Then mpe anachokitaka legally ili na wewe upate share yako kidogo.
Usiulize kuhusu watoto wala nini. Wanakufahamu, watakutafuta.
Once her hold on you is gone hiyo ya kukufanya kila siku chache uende polisi, fanya maisha.
Imagine first born yuko form 2, halaf mtu analeta usenge namna hiiNamaanisha vile anavyojipenda na kujikuta sistaduu.....
Hapo ushauri ni kumpotezea tu.....atarudi tu, mshazaa udugu wenu haufi.