Mshkaji wangu anataka kumroga mama watoto wangu

Mshkaji wangu anataka kumroga mama watoto wangu

Hili ni kwel, nakubaliana na wewe, watoto wangu ndio udhaifu wangu mkubwa
Wewe unatakiwa upigwe vibao vya shavu kama vitatu ubongo ukukae sawa.....mimi ni ke ila kuna siku baba watoto aliniletea pigo za kuondoka na akachukua mtoto.....wallahi naapa sikumzuia, sikupiga simu, sikushtakia ndugu....yani niliendelea na life langu kama hamna kilichotokea, na mtoto nimemzaa kwa shida uzazi wa nusu kifo na kisu juu.....ila sikukohoa, haikumaliza siku 3 alirudi na msamaha aliomba.
Sa wewe mwanaume hata labour huijui, unatishiwa watoto?
 
Wanakuja kwa kasi ya mwanga

Wakuu heshima kwenu.
Sipendelei sana kuingia deep kwenye mkasa mzima unaoihusu familia yangu , especially mimi na wife.
Ila kwa kifupi tu, wife alizingua big big big time (usiulize nini maana ni ishu serious sana inayoweza husishwa na suala la uaminifu moja kwa moja)

Na nilipotaka maelezo toka kwake, akanijibu shit kwel kweli, nikaona this is too much, nikamchapa vizuuri tu.
Ila akili ziliponirudia nikaona nimefanya sio kitu kizuri, nikamuomba radhi.

Huu ukawa mwanzo wa mambo mengi sana, wife na ndugu zake waka kaa kikao, wakamshauri kuwa aachane na mimi. Akaanza harakati za kutekeleza maazimio ya kikao chao
Baada ya 10 days, aka force akatafuta pf3, akatafuta cheti cha daktari (alihonga).
Baada ya hapo, akaenda polisi, akakata RB (koote huko alishatafuta watu yeye akisaidiana na ndugu zake). Haya yoote yalikua yanafanyika bila mimi kujua chochote, nimekuja kuyafaham too late.

Akatega siku niko ofisini, nimeondoka tumeagana vizurii kabisa kwa vicheko (Nisijue moyoni anaendelea na mipango ya kuniingiza kwenye 18 zake).
Ile narudi home, nakuta ,kabeba watoto wangu, kabeba hati ya nyumba na eneo, kabeba card ya gari na vyeti vyake vyooooote vya taaluma na ajira (mtumishi wa serikali yeye) akasepa.
Nikaja gundua kuwa ni kaka yake alimfuata.
Basi siku bother kumtafuta. Nikatoa tu taarifa nyumbani kwetu kwa wazee.

E bwana ee, baada ya hapo, nikaanza kupelekewa moto,

- nikapelekwa gender desk police kuwa nimetelekeza na situnzi familia na mimi ni mnyanyasaji, nikapangua mashtaka kwa hoja na vielelezo, kesi kule ikamgeukia yeye, hata hivyo nikamuomba radhi na kumsihi tuyamalize, akagoma kabisaa. Hakuridhika

- wazee wangu wakaja, wakakaa kama familia na familia yake, mbele ya kikao, akamtusi baba angu, akatamka kuwa hanipendi wala hanitaki tena, na hata watoto sitakaa nije kuwaona tena. Nikamsihi, kwann unafanya haya hali wewe ndio sababu ya yote haya mpaka nikakupiga , akagoma katakata, kikao hakikuisha na suluhu ila ndugu zake wakasema hii ndoa lazima ivunjike. Hakuishia hapo

- akanipeleka baraza la usuluhishi la kata, hapa lengo lake ni kupewa form no.3 ili akafungue shauri la kudai talaka mahakamani. Wale wazee wa baraza walipotusikilizaa, wakamuona hana hoja, wakamuuliza wewe ni nani aliyeingilia kati na anakuendesha na kukudanganya? Mmezaa watoto wa 4, unataka talaka ya nini?? Wakamwambia, nenda kajifikirie upya ndio urudi tena, tutakupa. Huku nako akaonekana hana hoja ya msingi, na bado nikawa namsihi aghairi maamuzi yake ila waaap. HAKURIDHIKA

- juzi kati, niko mkoa mmoja kanda ya ziwa, napigiwa simu na mkuu wa upelelezi , kuwa nahitajika kituoni.
NIkasafikiri mpaka dar, kufika na kureport, namkuta wife pale, nikakamatwa na kutiwa ndani ( lockup). Hapo polisi wakachukua funguo za nyumbani kwangu wakampa wife, akaenda akasomba vitu vya ndani, akaondoka kwenda kupanga na kuanza maisha mengine akiwa na watoto, ambao toka alipokimbilia kwao nao mwezi November 2024.

- nikatoka nje kwa dhamana, hata muda huu niko chini ya dhamana na ninatakiwa ku report kituon after every short period of time.

SASA KISA KINAANZIA HAPA JAPO NI KIFUPI
Currently ,nikagundua wife kadhamiria kunikomesha, kazi zangu ni za kusafir, ila kwasasa siwez enda safari zaidi ya week kwasababu natakiwa kituoni kila mara.
Baada ya kuondoka home, imani yangu kwake ikatoweka nikahisi huyu asije nifanyia kitu mbaya, kwa muda nikawa nalala lodge, hiz zote ni gharama natumia.
Kazi zangu ni kama zimekwama.
Kesi yangu kimsingi ni kama imeshatoka polisi, ila chaajabu ni kwamba hawataki kuipeleka mahakamani, wananisumbua sana na masuala ya ku report kila mara kituoni.
Yale matumaini yoote ambayo nilikua nahis huenda hiz za wife ni hasira tu, nikaja gundua she is seriously intending to destroy me.

Shida yangu kubwa, mimi siiwezi michezo ya ubaya ubwela. Mimi ni wale ambao Yesu alisema "mtu akikupokonya koti lako, mwachie na kanzu, pia, akikuambia twende maili moja, wewe nenda maili 2". Kwakifupi, mimi mambo ya kulipiza ubaya siyawezi.

Sasa siku moja nikiwa very frustrated, nikakutana na mwamba mmoja ni mshkaji wangu, class mate tukiwa chuo. Katika hapa na pale nikamsimulia madhira kwa uchache aliyonitendea shemeji yake. Huyu jamaa anamjua wife maana mimi nilizaa mtoto wa kwanza na huyu mama tukiwa chuo mwaka wa kwanza, na ile hustle ya malezi na matunzo walikua wanaiona maana tulikua tuna kaa hostel moja kigamboni nikiwa mwanafunzui ninaye survive kwa pesa ya boom.

Bas nilipomsimulia (hapo kabla sijawekwa ndani) , jamaa akasikitika sana. Akanitia moyo akasema yatakwisha.
Ila mshkaji niliona kalichukulia lile suala kwa uzito sana. Alitamka neno moja tu "ni yule shemeji uliyekua unamhangaikia enzi zile tukiwa chuoni??? (Over 10 years ago)"

Nikamwambia ndio huyo huyo nilioa.Basi jamaa akafikiria akasepa.

Sasa jana jioni nikiwa facebuk, akaniona online, akaniuliza "braza kimya sana, lile jambo vipi linaendeleaje?"

Nikamwambia "jambo limekaa vibaya sana, hapa penyewe nimetoka lockup nina siku 2 tu, niko nje kwa dhamana, shemeji yako kaamua kuninyoosha"

Jamaa hakua na maneno mengi, akaniuliza "hivi shemeji majina yake ni nani?"
Nikamtajia.
Akaniuliza anafanya kazi maeneo gani? Nikamtajia.

Akasema "braza, nitahangaikia hili suala kwaajili yako,wewe ni ndugu yangu tumetoka mbali, siwezi ona unateseka namna hii kisa mwanamke yeye kakaa tu ana enjoy na mmezaa watoto"

Nikauliza , "una plan kufanya nini"
Akasema "huyu, ningepata mchanga wa mahala alipokanyaga nyayo zake ingekua vizuri, ila sio kesi kwakua ushaniambia anafanya kazi maeneo gani, hii pia itasaidia"

Hapa nikashtuka, nikamwambia "braza , naomba kwanza utulie, next week natakiwa ku report kituoni pamoja na yeye, baada ya kusikia nini kinazungumziwa huko nitakupa feedback kwanza"

Akasema "sawa, na kabla hujakwenda huko, nitakuambia nini cha kufanya"

Wakuu, hapa kwa akili yangu ndogo kabisa, nikajua tu kuna "juju" linataka kuandaliwa, wife apigwe "kimbola/kombora" ila nikasema kwanza "hold on".

Wazee mimi si mtu wa mambo hizo.
Na hata kama huyu mama kashaamua kunipiga pini, ila bado tuna watoto nae na anao yeye, hata kama yeye kanikusudia mabaya, honestly mimi bado namuwazia mema.

Japo kwasasa nishaona kuwa hakuna dalili wala matumaini yoyote ya sisi kuwa pamoja tena, na nimeshaanza ku move on, na yeye alishaga move on kitambo i think ndio maana ananitenda ubaya huu.
Mke wa miaka 15, tulioana na kuzaa mapema sana, maana mimi ndio kwanza sasa nina 35 yrs na yeye 36 yrs.
Ila kiukwel kanikusudia mabalaa mabaya sana, na mshkaji wangu anataka kupambana nae kupitia teknolojia ya "anga za juu", ila mimi kiukwel, I DO NOT WISH HER ANYTHING BAD".

Ungechukua uamuzi ganu juu ya msaada kama huu ninaopewa na mdau wangu?

Jioni njema

Magumu ila yatapita, kula vizuri, Fanya kazi vizuri, mpe talaka mapema! Tatizo lako hutaki muacha, ungetaka muacha angeshatulia!
 
Wasinipige tu mawe, maana hawatakawia kuniita mwanaume dhaifu
Sasa unauliza makofi polisi. Kwani wewe huoni ulivyo dhaifu?

Unadhani kuna mwanamke wa kumchezea hivyo mwanaume serious na asiyetabirika. Mwanamke wako hakuogopi bali unamuogopa wewe mpaka unaenda kujificha lodge unaacha nyumba yako. Kisha unakuja hapa ukiamini wewe ni shupavu.

Wewe ni Khadija mmoja hivi, hamna kitu.
 
Wewe unatakiwa upigwe vibao vya shavu kama vitatu ubongo ukukae sawa.....mimi ni ke ila kuna siku baba watoto aliniletea pigo za kuondoka na akachukua mtoto.....wallahi naapa sikumzuia, sikupiga simu, sikushtakia ndugu....yani niliendelea na life langu kama hamna kilichotokea, na mtoto nimemzaa kwa shida uzazi wa nusu kifo na kisu juu.....ila sikukohoa, haikumaliza siku 3 alirudi na msamaha aliomba.
Sa wewe mwanaume hata labour huijui, unatishiwa watoto?
Ahahahahah...umenichekesha sana mkuu, ila umeni lift up my soul.
Kosa langu kubwa ni kuanza kufuata protocols
 
Mkuu kwa wakristo ,talaka ya namna hii inawezekana?? Nifundishe zaidi
Wewe mwite akifika mpe ushahidi wa maandishi na akuambie anataka nini hasa achukue kama ni nyumba Mali akae nazo na wewe hutamfuatilia!!!!

Na wewe nenda kaoe kienyeji hukooo vijijini!

We jaribu hiyo !utaona ataikubali TU hivyo hivyo!anachotaka huyo ni umiliki was Mali!we andika kwamba umemuachia Kila kitu alee watoto!
 
Nilisha hama, mwezi huu kwenda ku chill mwanza nihamishe harakat huko, alipo jua hilo ndio moto wa police ukaanza, nahisi hataki na mimi ni move on
Sasa ukimove on atamchezea nani na wewe ndo mnyonge wake 😅?? We mng'ang'anie tu mana mmezaa watoto mlazimishe mrudiane na mama si hakumtukana? We fosi fosi hapo mama nae apate tusi ! Ukitoka hapo lazimisha muishi pamoja akuchomee ndani.. safi kabisa! Braza wewe yani una moyo mwema sana kaza acha kusikiliza hawa watu wanaokushauri ubaya ubwela
 
Sasa unauliza makofi polisi. Kwani wewe huoni ulivyo dhaifu?

Unadhani kuna mwanamke wa kumchezea hivyo mwanaume serious na asiyetabirika. Mwanamke wako hakuogopi bali unamuogopa wewe mpaka unaenda kujificha lodge unaacha nyumba yako. Kisha unakuja hapa ukiamini wewe ni shupavu.

Wewe ni Khadija mmoja hivi, hamna kitu.
Ahahaha dah mwanangu usifanye hivyo bwana 🤣🤣
 
Piga chini haraka sana, mwanaume unakuwa mlaini laini kiasi hicho, huyo sio mke wako tena ana wanaume nje wanamla sana hana hisia na wewe tena na wana msupport, kuwa na roho ngumu mwambie sitaki kukuona usoni mwangu na koma, tena mwambie una oa mke mwingine mkali sana, akae mbali kabisa na wewe, acha urojo urojo, mwanaume kuna wakati unaamua maamuzi magumu ili kusonga mbele, huyo mkeo alikuwa analiwa nje hana hisia wala hafuati akili zako tena, yaani hadi anamtusi Baba yako mzazi umesema? Weeeeee, ana bahati sana, wengine sie angekula karate na kibao kimoja tu hapo na atakojoa na haja kubwa kwa pamoja hapo hapo na atakata pumzi au akiamka hapo hatadhubutu kukuona tena, huyo shetani tayari, piga chiniiii haraka plse
 
Wewe mwite akifika mpe ushahidi wa maandishi na akuambie anataka nini hasa achukue kama ni nyumba Mali akae nazo na wewe hutamfuatilia!!!!

Na wewe nenda kaoe kienyeji hukooo vijijini!

We jaribu hiyo !utaona ataikubali TU hivyo hivyo!anachotaka huyo ni umiliki was Mali!we andika kwamba umemuachia Kila kitu alee watoto!
Nakufuata pm
 
Mi nashangaa skuizi watu wanapenda maushauri! Baba zetu walikua wanajua wao wanaume maisha popote mama akizingua anaachiwa mji kimya kimya mnasikia tu baba enu anafamilia amenzisha Makambako amejenga huko. Wala mzee haongei ni watu tu wamekutana nae huko
 
Sasa ukimove on atamchezea nani na wewe ndo mnyonge wake 😅?? We mng'ang'anie tu mana mmezaa watoto mlazimishe mrudiane na mama si hakumtukana? We fosi fosi hapo mama nae apate tusi ! Ukitoka hapo lazimisha muishi pamoja akuchomee ndani.. safi kabisa! Braza wewe yani una moyo mwema sana kaza acha kusikiliza hawa watu wanaokushauri ubaya ubwela
Nimekuelewa japo umeongea kinyume nyume 😅
 
Back
Top Bottom