Mshuhudie Mwanamke wa shoka, baada ya kuhitimu Chuo Kikuu, alikosa Ajira, akajiongeza kwa kusoma VETA

Mshuhudie Mwanamke wa shoka, baada ya kuhitimu Chuo Kikuu, alikosa Ajira, akajiongeza kwa kusoma VETA

Pascal my brother, wewe ni zaidi ya hili, yule bwana mkubwa aliteleza kuendelea kushabikia ni kutetea ujuha.

Tatizo liko kwenye mfumo wa elimu hautoa competent graduates, hatujui watu wasome nini katika kila level. (Hili ni tatizo la hao hao watawala sio shida ya graduate).

Hata hao graduate wa Veta wengi nao wanakosa competence yaani bado huwezi kufananisha na graduate wa vocation za Ulaya na America, wengi pia ni magumashi.

Shida ni tatizo la ajira kiujumla, tatizo hili lipo kuanzia kwa graduate wa degree mpaka hawa wa Veta, Serikali imeshindwa kusolve hii equation.

Graduate wa degree ya Kila aina ya fani anapaswa kuwa na uwezo kulingana na level yake aweze kucompete ndani na nje ya nchi.
Competence inaanzia chini ni kama zege kwenye column lazima iwe compacted Kila mahala, kuanzia msingi, sekondari mpaka chuo kikuu mfumo ukiwa sawa lazima huyu mhusika awe competent kukiwa na vacuum mahala katikati lazima mhusika awe kimeo tu.

Uwanja mtaani ni mdogo kiasi cha kushindwa kubeba graduates wa kuanzia degree, Engineers kuna mahala wanafiti kama nchi Ina shughuli nyingi za uzarishaji mali.
Kazi anayopaswa kufanya engineer hakuna mahala Veta anaweza kufanya.
Nimependa sentensi yako ya mwisho….
 
Kwenda VETA siyo shida, swali ni VETA inatoa elimu bora kuliko Chuo kikuu? Kama ndiyo watunga sera wanasubiri nini kufuta vyuo vikuu au waboreshe mitaalama? Yaani tuache wafanye design Power plant? Au hydropower plant?
Kwa mawazo ya Wazir Majaliwa elimu ya chuo kikuu si lolote kuliko elimu ya VETA
 
No sio kila mtu lazima asome VETA, wasomi wa chuo kikuu, wanaopaswa kusoma, ni wale waliohitimu fani fulani kwa mategemeo ya kupata ajira za kisomi, wamekosa ajira, badala ya kukaa tuu, kama ma jobless , na wale dada zetu kulazimika ku danga, bora wasome VETA na kujiajiri!.
P
Kwan mkuu umeshafanya utafiti kujua ni idadi Gani ya hao wanaomaliza VETA wamejiajiri?
 
Kuna vijana wengi mitaani wanasubiri ajira lakini hakuna ajira ,ili waendelee kusubiri lazma tutafute utaratibu wa kuwakopesha kwa degree ya pili hii itaondoa vijana tegemezi kwenye familia zetu,maama hawana KAZI ya kufanya wanakula ugari tu
Mkuu Makwa, makwagejo , nakuunga mkono hoja yako ya vijana wote degree holders walio mtaani, wakopeshwe kurudi shule, ila sio kwenda kusoma masters, bali waende kusoma VETA au elimu ya biashara, kusomea kitu chochote cha elimu ya kujitegemea, wakimaliza wakopeshwe mitaji, waanze kujitegemea.

Wakirudi tuu darasani kufanya masters ya walichosomea, kama kwa first degree walichosoma hakina demand kwenye job market, hata wakirudi darasani kufanya masters, itakuwa ni wastage of time and resources, baada ya miaka miwili ya masters, watarudi tena mitaani na kuwa na jobless wenye masters!.

Solution ni kwenda kusoma VETA au elimu yoyote ya kujitegemea, iwe ni elimu biashara, kilimo biashara, uvuvi biashara, wakimaliza wanapewa mikopo na kuanza kujitegemea na kuanzia sasa wanafunzi wasiendelee kusoma chochote tuu ali mradi kafika chuo kikuu, waangalie trends za demands za job market zinataka nini.

Ushauri huu wa Waziri Mkuu Mstaafu Majaliwa Kassim Majaliwa, ni ushauri kuntu na muafaka sana, https://www.jamiiforums.com/threads...kukuza-ujuzi-wa-vijana-wa-kitanzania.2319397/


na https://www.jamiiforums.com/threads...veta-japo-chungu-ndio-ukweli-wenyewe.2320751/

na https://www.jamiiforums.com/threads...u-homa-veta-ndio-tiba-ya-joblessness.2319563/



Mzee Pasco
 
Wanabodi,

Ule mjadala wa wasomi wa Chuo Kikuu, kusoma VETA, unaendelea,

Mshuhudie Mwanamke wa Shoka, Baada ya Kuhitimu Chuo Kikuu, Alikosa Ajira, Akajiongeza kwa Kusoma VETA, Sii Mwingine ni Paulina Chuma, Fundi Chuma!


View: https://youtu.be/hrFHfkk06Wk

Utafiti wangu mdogo, umebaini, hawa wasomi waliokwenda kusoma VETA, ndio wanaofanya vizuri zaidi sokoni, kuliko wasomi plain wa chuo kikuu au mafundi plain wa VETA, kwasababu hawa wana kitu cha ziada!, wanafanya ufundi kisomi zaidi, na wamefanikiwa zaidi kuliko VETA plain!.

Hii maana yake, umuhimu wa wananchi wengi kusoma kiwango cha chuo kikuu bado ni muhimu, na ikitokea umehitimu elimu ya chuo kikuu, ukakosa kazi, na kwa elimu uliosomea, ukajikuta huwezi kujiajiri, then nenda VETA!.

Paskali

One in a thousands.
Wengine wanaoendelea kufanikiwa walipita VETA?

Usiwalazimishe watu kuamini na kufuata unayoyataka. Wapo watafanikiwa, wapo watakaoendelea kusota
 
One in a thousands.
Wengine wanaoendelea kufanikiwa walipita VETA?

Usiwalazimishe watu kuamini na kufuata unayoyataka. Wapo watafanikiwa, wapo watakaoendelea kusota
Mimi ni mwandishi wa habari na mtangazaji, kazi yangu ni moja tuu, kusema na kuandika, hakuna mwandishi yeyote anayemlazimisha mtu yeyote kuamini chochote, kazi yetu ni kuandika na kutangaza kitu cha ukweli tunachokijua, kisha uamuzi wa kuamini ni kwako msomaji, mtazamaji na msikilizaji.
P
 
Back
Top Bottom