Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
- Thread starter
-
- #61
Bukoba...Yani Mzee unavoshupalia coincidence ya Uislam kuweko kwenye historia ya Tanganyika ni sawa na Urusi kujisifia kua wao ni walevi wazuri.
Sasa harakati zimefanyika mostly Pwani unategemea waislam wasiwemo?Hiyo ni kawaida sana.Waislam wao kila kuchwa ni kulia dhulma tu!..
Kwa mfano hizo harakati zingefanyikia Tukuyu halafu wanyakyusa waanze kujisifia.Coincidence tu!
Kituko unachekesha sana. Dk. Kyaruzi mie ndiye niliyemfufua na kuandika historia yake. Nitakuwekea jinsi nilivyomwandika ili wasomaji watuhukumu.Sina hila wala uongo maishani mwangu, na siwezi msingizia mtu chochote, ndivyo nilivyolelewa, sina haja sana ya kukulazimisha, kama huamini ni sawa tu
Kituko,
Hilo la kuwa Tanganyika ilipewa uhuru baada ya WWII ndiyo
leo nalisikia kwako.
Nimesoma kila kitabu kilichoandikwa kuhusu ukoloni Tanganyika.
Zaidi nimesoma hadi shajara za Kleist Sykes na nyaraka za
watoto wake sijakuta popote hilo limeandikwa.
Nimemsoma Martin Kayamba, ''The Autobiography of
Martin Kayamba...'' hakuna kitu kama hicho.
Nimewasoma Erika Fiah mhariri wa Kwetu na Ramadhani
Mashado Plantan mahriri wa Zuhra hakuna kitu kama hicho...
Kituko unachekesha sana. Dk. Kyaruzi mie ndiye niliyemfufua na kuandika historia yake. Nitakuwekea jinsi nilivyomwandika ili wasomaji watuhukumu.
Mzee Mohamed Said, kwanza namshukuru Mungu kwakuwa bado uko hai pamoja na kushudia mambo mengi ya zamani ambayo wengi wetu humu tunabaki kuwa wasikilizaji lakini wewe uliyaona na unayakumbuka.Chachu...
Siwezi kushangaa ikiwa hamumtambui Ali Migeyo.
Hakutambuliwa Abdul Sykes mwenye kadi ya TANU No. 3
Hakutambuliwa Ally Sykes mwenye kadi ya TANU No. 2 na
kadi ya TANU No. 1 ya Mwalimu Nyerere ni Ally Sykes
ndiye aliyeiandika.
Hajatambuliwa baba yao Mzee Kleist aliyejenga hiyo ofisi
ilipozaliwa TANU 1954.
Hajatambuliwa Iddi Faizi Mafungo aliyesimamia safari ya
Nyerere UNO 1955.
Kipi mimi leo kitanishangaza ikiwa hamumtambui Suedi
Kagasheki?
Ama kuhusu Uislam naam ulitumika sana katika kupambana
na ukoloni kuanzia Vita ya Maji Maji dhidi ya Wajerumani hadi
kudai uhuru kutoka kwa Waingereza.
Ilikuwa Salum Mpunga na Ali Ibrahim Mnjale ndiyo vijana
waliomleta Mwalimu Nyerere Jimbo wa Kusini kuja kupambana
na Kanisa lililokuwa linawatisha wananchi kujiunga na TANU kudai
uhuru.
Wala katika kuandika historia hii hakuna udini ni historia tu tupu
iliyokuwapo hatuwezi kuifuta hata kama kuna baadhi yetu kwa
sababu zetu binafsi hatuipendi.
Kipi kitanishangaza ikiwa wewe leo hii humjui Sheikh Yusuf Badi,
Sheikh Hassan bin Amir, Sheikh Suleiman Takadir waliokuwa
mstari wa mbele kupigania uhuru wa Tanganyika?
Ikiwa wewe una historia nyingine isiyokuwa hii tuwekee hapa Majlis
tuisome.
Pep ahsante sana kaka.Una Hekima sana mzee Said. Saf sana
Mwanyasi nimeandika kitabu The Life and Times of Abdulwahid Sykes kipo na cha Kiswahili kinapatikana Ibn Hazm Bookshop Msikiti wa Manyema na Mtoro Dar es Salaam bei elfu 10000.00.Mzee Mohamed Said, kwanza namshukuru Mungu kwakuwa bado uko hai pamoja na kushudia mambo mengi ya zamani ambayo wengi wetu humu tunabaki kuwa wasikilizaji lakini wewe uliyaona na unayakumbuka.
Lakini pia umejitahidi kuandika mara nyingi haya mambo ya historia ya nchi yetu; wakati wa ukoloni, kutafuta mpaka kupata uhuru, mapinduzi ya Zanzibar na Muungano wa Tanzania.
Kwa haraka haraka nimeona kama vitu vingi unavifahamu kwa undani.
Niombe: uandike kitabu kinachoelezea hivyo vitu vyote ili tulio wengi tuisome historia sahihi ya Tanzania badala ya kuishia kusoma vitabu vya shule vilivyohaririwa kadri ya matakwa ya watawala waliopo.
Nimesoma comments za wenzangu hapo juu zikielezea kuwa unakuwa upande wa dini moja, hilo siyo tatizo maana ukweli unabaki kuwa ukweli, pengine hii itatupa changamoto ya kwenda kuwahoji wazee wetu waliopo katika maeneo unayowataja ili tujiridhishe na pengine kuongezea uliowasahau. Mimi ni mkrisito lakini elimu haijui dini hivyo sioni tatizo.
Najua kinaweza kikapata ugumu kusajiliwa hicho kitabu tukipata hata "raw" tutaelewa. Hii itapaki kuwa elimu kwa vizazi vingi.
Kama kitabu kipo tayari nitaomba ueleze hapa ili nijue namna ya kukipata.
Uko sahihi kabisa
Yani Mzee unavoshupalia coincidence ya Uislam kuweko kwenye historia ya Tanganyika ni sawa na Urusi kujisifia kua wao ni walevi wazuri.
Sasa harakati zimefanyika mostly Pwani unategemea waislam wasiwemo?Hiyo ni kawaida sana.Waislam wao kila kuchwa ni kulia dhulma tu!..
Kwa mfano hizo harakati zingefanyikia Tukuyu halafu wanyakyusa waanze kujisifia.Coincidence tu!
Kituko Tanganyika ilikuwa chini ya udhamini lakini ili uhuru upatikane ilikuwa lazima tuidhihirishie UNO kuwa tuko tayari na tunaweza kujitawala. Waingereza hawakuwa wanalitaka hili walitaka wabakie kututawala. Turning point ya hili ilikuwa 1950 Abdul Sykes na Hamzah Mwapachu walipofanya mapinduzi na kuchukua uongozi wa TAA kwa nguvu. Nia ikiwa kudai nchi. Mwalimu Thomas Plantan aliyekuwa rais wa TAA wakati ule alikuwa hafanyi lolote la maana kudai nchi. Waingereza wakaingia kati na kudai akina Abdul waache fujo uitishwe uchaguzi. Katika mkutano wa pande mbili wa waliopinduliwa na waliopindua pale Arnautoglo Schneider Plantan aliwakabili Waingereza na kudai lazima uitishwe uchaguzi na yeye ndiye aliyesaidia kuwatia Abdul Sykes na Dr. Kyaruzi katika uongozi wa TAA. Hapo ndipo harakati za mawasiliano na UNO zikaanza kwa msaada mkubwa wa Earle Seaton. Waingereza wakahujumu uongozi huu...Vituko umeuliza kazi ya Waingereza Tanganyika...hiyo ndiyo ilikuwa kazi yao kuikalia Tanganyika. Baya zaidi ni kuwa Kanisa nalo likawa linawatisha wafuasi wake ati wachukue tahadhari na Waislamu wanataka kuleta vita vingine kama walivyoleta na Wajerumani kupitia Maji Maji. Ilipokuja Kamati ya UNO kukagua Tanganyika 1954 Said Chamwenyewe ndiye aliongoza ujumbe wa watu wa Tanganyika kuzungumza na ujumbe ule. Huyu Mzee Chamwenyewe ndiye aliyeipa TANU wanachama wake wa kwanza kutoka Rufiji wengi wao wakiwa murid wa Tariqa Qadiriyya ambao Khalifa wao alikuwa Mufti Sheikh Hassan bin Ameir. Sheikh Hassan bin Ameir alikuwa katika TAA Political Subcommitte pamoja Abdul, Mwapachu na wazalendo wengine kama Steven Mhando. Hii ndiyo historia ya TANU...inachoma nyoyo lakini tufanyeje tuifute kuwafurahisha wale ambao walikaa pembeni wakati wazee wetu wanapigania uhuru wa Tanganyika?Unataka iandikwe hivyo?, Je Tanganyika lilikuwa Koloni la Uingereza?, waingereza walikuwa na kazi gani hapa Tanganyika?
Ahsante, inamaana katika kitabu hicho zimo taarifa zote kama nilivoshauri? Au ni hiyo tu ya Abdulwahid Sykes? Kama zote zimo sawa, na kama ni vinginevyo, huoni kuna umuhimu wa kuandika kipana zaidi.Mwanyasi nimeandika kitabu The Life and Times of Abdulwahid Sykes kipo na cha Kiswahili kinapatikana Ibn Hazm Bookshop Msikiti wa Manyema na Mtoro Dar es Salaam bei elfu 10000.00.
Mwanyasi yapo mengi ni kitabu cha zaidi ya kurasa 350.Ahsante, inamaana katika kitabu hicho zimo taarifa zote kama nilivoshauri? Au ni hiyo tu ya Abdulwahid Sykes? Kama zote zimo sawa, na kama ni vinginevyo, huoni kuna umuhimu wa kuandika kipana zaidi.
Hicho kilichopo nitakifuata hapo,ahsante.
Hakukua na uamsho sababu ilikua ""kijijini" ukilinganisha na Dar ambako ndio Uingereza alifanya makao yake ya utawala..Au unataka niseme sababu hawakua na Uislam mwingi kama watu wa Pwani?Mzee bwana si useme tu unaeneza Udini kupitia hiyo Historia yako yaishe! Na hakuna hata siku moja watu wameuinua Ukristo wa Nyerere na kuuunganisha na harakati alizokua anafanya.Bukoba...
Nitakuuliza swali kwa nini Tukuyu wakawa nyuma katika kudai
uhuru?
Hujajibu swali, au ndiyo njia yako ya kukwepa maswali?
Alama Mohamed Said kaandika historia ambayo mpaka leo hii hakuna wa kuipinga.
Kama unapenda isome kama hupendi isome halafu tuletee historia yako tuuone ukweli wako.
Mmekazana humu porojo ndeefu na kuponda kisichopondeka.
Ukweli ukidhihiri uongo hujitenga.
Umesoma kuhusu Mshume Kiyate?
Bukoba...Hakukua na uamsho sababu ilikua ""kijijini" ukilinganisha na Dar ambako ndio Uingereza alifanya makao yake ya utawala..Au unataka niseme sababu hawakua na Uislam mwingi kama watu wa Pwani?Mzee bwana si useme tu unaeneza Udini kupitia hiyo Historia yako yaishe! Na hakuna hata siku moja watu wameuinua Ukristo wa Nyerere na kuuunganisha na harakati alizokua anafanya.
Kituko Tanganyika ilikuwa chini ya udhamini lakini ili uhuru upatikane ilikuwa lazima tuidhihirishie UNO kuwa tuko tayari na tunaweza kujitawala. Waingereza hawakuwa wanalitaka hili walitaka wabakie kututawala. Turning point ya hili ilikuwa 1950 Abdul Sykes na Hamzah Mwapachu walipofanya mapinduzi na kuchukua uongozi wa TAA kwa nguvu. Nia ikiwa kudai nchi. Mwalimu Thomas Plantan aliyekuwa rais wa TAA wakati ule alikuwa hafanyi lolote la maana kudai nchi. Waingereza wakaingia kati na kudai akina Abdul waache fujo uitishwe uchaguzi. Katika mkutano wa pande mbili wa waliopinduliwa na waliopindua pale Arnautoglo Schneider Plantan aliwakabili Waingereza na kudai lazima uitishwe uchaguzi na yeye ndiye aliyesaidia kuwatia Abdul Sykes na Dr. Kyaruzi katika uongozi wa TAA. Hapo ndipo harakati za mawasiliano na UNO zikaanza kwa msaada mkubwa wa Earle Seaton. Waingereza wakahujumu uongozi huu...Vituko umeuliza kazi ya Waingereza Tanganyika...hiyo ndiyo ilikuwa kazi yao kuikalia Tanganyika. Baya zaidi ni kuwa Kanisa nalo likawa linawatisha wafuasi wake ati wachukue tahadhari na Waislamu wanataka kuleta vita vingine kama walivyoleta na Wajerumani kupitia Maji Maji. Ilipokuja Kamati ya UNO kukagua Tanganyika 1954 Said Chamwenyewe ndiye aliongoza ujumbe wa watu wa Tanganyika kuzungumza na ujumbe ule. Huyu Mzee Chamwenyewe ndiye aliyeipa TANU wanachama wake wa kwanza kutoka Rufiji wengi wao wakiwa murid wa Tariqa Qadiriyya ambao Khalifa wao alikuwa Mufti Sheikh Hassan bin Ameir. Sheikh Hassan bin Ameir alikuwa katika TAA Political Subcommitte pamoja Abdul, Mwapachu na wazalendo wengine kama Steven Mhando. Hii ndiyo historia ya TANU...inachoma nyoyo lakini tufanyeje tuifute kuwafurahisha wale ambao walikaa pembeni wakati wazee wetu wanapigania uhuru wa Tanganyika?