Mzee
Mohamed Said, kwanza namshukuru Mungu kwakuwa bado uko hai pamoja na kushudia mambo mengi ya zamani ambayo wengi wetu humu tunabaki kuwa wasikilizaji lakini wewe uliyaona na unayakumbuka.
Lakini pia umejitahidi kuandika mara nyingi haya mambo ya historia ya nchi yetu; wakati wa ukoloni, kutafuta mpaka kupata uhuru, mapinduzi ya Zanzibar na Muungano wa Tanzania.
Kwa haraka haraka nimeona kama vitu vingi unavifahamu kwa undani.
Niombe: uandike kitabu kinachoelezea hivyo vitu vyote ili tulio wengi tuisome historia sahihi ya Tanzania badala ya kuishia kusoma vitabu vya shule vilivyohaririwa kadri ya matakwa ya watawala waliopo.
Nimesoma comments za wenzangu hapo juu zikielezea kuwa unakuwa upande wa dini moja, hilo siyo tatizo maana ukweli unabaki kuwa ukweli, pengine hii itatupa changamoto ya kwenda kuwahoji wazee wetu waliopo katika maeneo unayowataja ili tujiridhishe na pengine kuongezea uliowasahau. Mimi ni mkrisito lakini elimu haijui dini hivyo sioni tatizo.
Najua kinaweza kikapata ugumu kusajiliwa hicho kitabu tukipata hata "raw" tutaelewa. Hii itapaki kuwa elimu kwa vizazi vingi.
Kama kitabu kipo tayari nitaomba ueleze hapa ili nijue namna ya kukipata.