Msiba wa Magufuli umesaidia kufahamu Sababu za Mbowe kuendelea kuwa Kiongozi ndani Chama chake

Msiba wa Magufuli umesaidia kufahamu Sababu za Mbowe kuendelea kuwa Kiongozi ndani Chama chake

Kilemakyaaro

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2016
Posts
5,050
Reaction score
5,119
Tokea tetesi za kuugua hadi kufariki kwa Mzee wetu Magufuli, baadhi ya Viongozi wa CHADEMA wamekua wakitoa matamko mengi sana, wengine wakaanza kuandika katika mitandao hisia zao juu ya msiba huo lakini wengi sana walikuwa wakidhihirisha chuki zao za waziwazi juu ya Mh. Magufuli.

Maandiko yao na maneno yao kwa vyombo vya habari imesaidia sana kutupa picha halisi ya watu hawa kiasi kwamba sasa hata kesho wakija kuomba ridhaa kwetu tunawafahamu.

Kupitia maandishi yao imenipa sababu ya kufahamu kwanini wale wachache miongoni mwao wenye akili wanapambana kufa na kupona Mbowe aweze kuendelea kuongoza chama chao, na hii ni kwasababu Mbowe ni mtu Smart sana, kwanza sio wakuongea tu bila kujipanga, ni mtu anaweza zuia hisia, ni mtu ambae ana ile kitu naweza kusema "Leadership Ethics).

Sasa kwa sifa za hao wengine ukimlinganisha na huyu mwamba iko sababu kubwa ya yeye kuendelea kuongoza hicho chama kwakuwa wenye akili walishaona hao wengine ni wanaharakati wanaojificha ktk mwamvuli wa chama.

Katika hali ya kawaida kwa mwanasiasa kijana na aliekomaa hata afe adui yako alieua familia yako yote unatakiwa kuwa smart sana kuchagua maneno yapi ya kutumia (uchaguzi wa lugha), vinginevyo unaweza kuanika tabia yako halisia na ujinga wako wote na watu walafaham madhaifu yako kitu ambacho kisiasa ni kitu mbaya.

Mbowe namkubali sana, una tabia za kiuongozi. Big up Big brother Mbowe!
 
Magufuli anaendelea kuishi kwenye mioyo ya watanzania

Wacheni tuomboleze kwa amani




Mungu ibariki Tanzania Mungu mbariki rais wetu Samia Suluhu Hassan🇹🇿🙏

Alale salama Mwamba💔💔💔
 
Nnaona wakosa akili wameendelea kujitokeza, lkn nnawakumbusha akumulikae mchana, usiku hukuunguza, yaani kama mtu unaweza hadharani kusherekea kifo cha mtu eti kisa tu unamchukia, siku ukipewa mabunduki yote, vifaru, mabomu na deraya utamaliza wale usiokubaliana nao.
 
Yaani kuna vijana akili zao mpaka unashangaa hivi ndio anazotumia kuishi na kutafuta riziki, maana hata uandike nini yeye kutukana, hakuna muda wa kutafakar yeye anashuka tu kama kondoo, yaani akili unaona hata kuvukia barabara tu hazitoshi, nlichoandika hapo wenye akili wameelewa vyema kwamba Kua kiongozi ni pamoja na kua na uwezo wa kuzuia chuki na mdomo, ongea kidogo na kila ukisema hakikisha unayosema sio ya kuumiza watu, mbona simple tu ila kuna kondoo hazieelewi.
 
Magufuli anaendelea kuishi kwenye mioyo ya watanzania

Wacheni tuomboleze kwa amani



Mungu ibariki Tanzania Mungu mbariki rais wetu Samia Suluhu Hassan[emoji1241][emoji120]

Alale salama Mwamba[emoji174][emoji174][emoji174]
Naomba huyo mtu wako asifike kwenye moyo wangu, nitajachomfanya atawasimlia.
 
Back
Top Bottom