- Thread starter
- #61
Kile ninachoona hapa ni tofauti ya tamaduni kati ya Kenya na Tanzania. Ni kama vile kule TZ huwezi kubaliwa kutumia neno dinda kwani maana yake ni erection. Ilhali huku kwetu, dinda ni kukataa. Wauguzi wamedinda kurudi kazini. Tusiwe na tabia ya kuiga mambo ya kizungu eti sababu wazungu hawafanyi hivi au vile. Unyanyapaa unatoka moyoni mwako na matendo unayoyafanya