Msidanganyike watanzania , pesa ya madini ni pesa ngumu na kuipata kwake ni mtihani

Msidanganyike watanzania , pesa ya madini ni pesa ngumu na kuipata kwake ni mtihani

mwanyaluke

JF-Expert Member
Joined
Jan 22, 2015
Posts
904
Reaction score
2,987
Baada ya harusi ya huko sijui katoro ,watanzania wengi wamehama na akili zao na kuamini pesa inapatikana kirahisi kama mtu atajichanganya kuingia kwenye chain ya biashara ya madini .


Ni kweli huko pesa inapatikana sawa na maeneo mengine tu , yaani huko pia kuna hitaji commitment, Imani na bahati.


Nina rafiki zangu waliojichanganya huko wapo waliofanikiwa wapo amboa wako broke totally, Moja ya rafiki yangu amewahi kuniambia pesa ya madini ni chafu kuliko tunavyodhani na kusema matajiri wengi wa madini hawadumu na hata yeye hata dumu kwa sababu huko kumejaa uchawi ,Pepo na dhuluma . So nilijochifunza kwake ni kwamba pesa ni ile ile yaani commitment,Imani ( hapa unachagua wewe uamini katika MUNGU au shetani lakini katika utaftaji lazima uwe na upande wa Imani na tatu ni bahati hapa haijilishi unajituma vip , unaimani kiasi Gani bahati inahusika
.
nilichojifunza watu wafanye kazi , pesa nyepepesi ipo tu serikalini ambako unaiba na hakuna wanachokufanya , nje ya hapo kunako Baki mafanikio ya kiuchumi ni mchakato na siku zote short cut ni wrong cut, hakuna eneo Lina pesa nyepesi ukitoa pesa ya kuiba ya serikali
 
matajiri wengi wa madini hawadumu na hata yeye hata dumu kwa sababu huko kumejaa uchawi ,Pepo
Una uhakika na haya uliyooandia huku ukiwa na reports zenye mashiko?

Maana uwekezaji wowote duniani haswa wa madini kwa watu walio micro una risk sana ila pia una reward kubwa sana lakini pia una hasara kubwa ya pamoja.

Sasa vitu kama hivi sisi ngozi nyeusi tunaona kama mazigaombwe wakati ni sayansi mbele yako kabisa.

Acha watu wafanye kazi mkuu.
 
Siyo mitazamo hasi alichokisema ni sahihi kabisa vijana ukiwakuta wanasimuliana habari za madini unabaki kuwashangaa tu mambo ya dhahabu ni kujitoa haswa kifedha maana inatakiwa uwekezaji na subira
Ulicho kieleza wewe ni sahihi sana, siyo alicho kieleza mtoa mada.
 
Siyo mitazamo hasi alichokisema ni sahihi kabisa vijana ukiwakuta wanasimuliana habari za madini unabaki kuwashangaa tu mambo ya dhahabu ni kujitoa haswa kifedha maana inatakiwa uwekezaji na subira
Binafsi nikishaona tu mtu kwenye hoja yake ameingiza visingizio sijui mambo ya giza kwa walio fanikiwa, napuuza kabisa hoja yake nzima.
 
Mkuu

Haya mambo kila mtu na imani yake niliwahi kwenda mtwara kuanzisha kilimo mambo niliyokuwa naambiwa na wenyeji, kuna muda huwa nacheka tu yaani mtu anaamini bila mizizi hutoboi
Na mtu mwenye imani ya aina hii, hauwezi kumuelewesha akakuelewa, ni ngumu mno.
 
Una uhakika na haya uliyooandia huku ukiwa na reports zenye mashiko?

Maana uwekezaji wowote duniani haswa wa madini kwa watu walio micro una risk sana ila pia una reward kubwa sana lakini pia una hasara kubwa ya pamoja.

Sasa vitu kama hivi sisi ngozi nyeusi tunaona kama mazigaombwe wakati ni sayansi mbele yako kabisa.

Acha watu wafanye kazi mkuu.
Wewe sikiliza jamaa alichokueleza leta habari sijui ni mazingaombwe na elimu za darasani.Nimeona hao wazungu mnaowakubali wakifanya matambiko tena makampuni makubwa ya uchimbaji madini yanayofahamika duniani.(ingekuwa sio kulinda usiri wa taarifa za watu ningekueleza hapa)

Dhahabu usiiletee wenge sijui elimu zako hizo kama ulishawahi kufanya kazi underground utajua dhahabu ina mauza uza kiasi gani.Kiufupi pesa ya dhahabu inahitaji kafara(Elimu yako tunza itakusaidia kwingine sio imani ndio ukweli)
 
Mi mnapoongelea madini nawazoom tu, madini sio karanga wakuu kama mnajifanya nyie wajuaji pelekeni hela zenu huko mje mrudi kwa miguu
 
Kiroho kazi ya dhahabu ni iliktengenezwa kwa ajili ya
1)kama rawa material kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya ibada hekalu la Mungu,vyombo vya madhabahuni katika hekalu la Mungu
1 Wafalme 6:21
Sulemani akalifunika Hekalu upande wa ndani kwa dhahabu safi na akaitandaza mikufu ya dhahabu kutoka upande mmoja hadi ule mwingine mbele ya mahali patakatifu, palipofunikwa kwa dhahabu
.
2) Kwa ajili ya kujenga nyumba za kusishi ambazo zitatadumu milele mana saruji zina chakaa expire date ila dhahabu inadumu milele,na lengo la kuumbwa mwanadamu ilkuwa aishi milele,
Ufu 21:1-25
Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya; kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza zimekwisha kupita, wala hapana bahari tena barabara kuu ya jiji ilikuwa ya dhahabu kama kioo safi"

Ndivyo ilivyo hata miji ya mbinguni nyumba za watakatifu mbinguni ni majengo ya dhahabu na ndivyo itakavyokuwa mbingu mpya YERUSALEMU MPYA mji wa dhahabu

DHAHABU INAPOTUMIKA KWA UREMBO NA MAPAMBO YA KUVAA MWILINI(VITO)
Kutoka 32.
Haruni aliwaambia wavue mafumbo na maua ya dhahabu yaliyokuwa masikioni mwao na kumletea.Kutengeneza Sanamu: Haruni akaipokea dhahabu hiyo, akaifinyanga kwa patasi, na kuitengeneza kuwa sanamu ya ndama wa dhahabu.Matokeo: Watu walianza kuiabudu sanamu hiyo na kusema, "Hii ndiyo miungu yenu, eyenu Israeli, iliyowatoa katika nchi ya Misri." Jambo hili lilimkasirisha sana Mungu

TULIPOFIKA
Nchi nyingi zinakusanya dhahabu nyingi sana hususani kutoka AFRICA kama CONGO DRC ZAIRE na Tanganyika n k ,zikakusanya dhahabu kwa wingi na kurundika kuhifadhi kama hazina ya duniani,kama akiba hazina ili itumike kama mbadala wa US PETROL DOLLAR ambapo hii US dollar itaanguka,na haitatumika tena kununulia petrol,utaanza mfumo mpya wa digital currency,na nchi tajiri zenye mafuta mengi zitaungana zitaanzisha pesa yao tofauti na US dollar na zitakataa kuuza mafuta kwa US DOLLAR..dhahabu itakuwa ni thamani ya pesa hata dola itakapo anguka siku za DHIKI KUU ambayo itaanza 2027 ama imeshaanza tuseme.
lakini hizi nchi tajiri pamoja na kukusanya FEDHA na DHAHABU nyingi bado hazitawasaidia katika KIPINDI CHA DHIKI KUU

Ezekieli 7:19
Watatupa fedha yao barabarani na dhahabu yao itakuwa kama kitu najisi. Fedha na dhahabu zao hazitaweza kuwaokoa katika siku hiyo ya ghadhabu ya Mwenyezi-Mungu; wala hawataweza kushiba au kuyajaza matumbo yao fedha na dhahabu waliyojirundikia; kwani mali hiyo ndiyo chanzo cha dhambi yao.
 
Back
Top Bottom