a sinner saved by Christ
JF-Expert Member
- Feb 19, 2017
- 4,014
- 4,600
Dhahabu hakukusudiwa itumike kama mapambo ya mwilini.Kiroho kazi ya dhahabu ni iliktengenezwa kwa ajili ya
1)kama rawa material kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya ibada hekalu la Mungu,vyombo vya madhabahuni katika hekalu la Mungu
1 Wafalme 6:21
Sulemani akalifunika Hekalu upande wa ndani kwa dhahabu safi na akaitandaza mikufu ya dhahabu kutoka upande mmoja hadi ule mwingine mbele ya mahali patakatifu, palipofunikwa kwa dhahabu
.
2) Kwa ajili ya kujenga nyumba za kusishi ambazo zitatadumu milele mana saruji zina chakaa expire date ila dhahabu inadumu milele,na lengo la kuumbwa mwanadamu ilkuwa aishi milele,
Ufu 21:1-25
Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya; kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza zimekwisha kupita, wala hapana bahari tena barabara kuu ya jiji ilikuwa ya dhahabu kama kioo safi"
Ndivyo ilivyo hata miji ya mbinguni nyumba za watakatifu mbinguni ni majengo ya dhahabu na ndivyo itakavyokuwa mbingu mpya YERUSALEMU MPYA mji wa dhahabu
DHAHABU INAPOTUMIKA KWA UREMBO NA MAPAMBO YA KUVAA MWILINI(VITO)
Kutoka 32.
Haruni aliwaambia wavue mafumbo na maua ya dhahabu yaliyokuwa masikioni mwao na kumletea.Kutengeneza Sanamu: Haruni akaipokea dhahabu hiyo, akaifinyanga kwa patasi, na kuitengeneza kuwa sanamu ya ndama wa dhahabu.Matokeo: Watu walianza kuiabudu sanamu hiyo na kusema, "Hii ndiyo miungu yenu, eyenu Israeli, iliyowatoa katika nchi ya Misri." Jambo hili lilimkasirisha sana Mungu
TULIPOFIKA
Nchi nyingi zinakusanya dhahabu nyingi sana hususani kutoka AFRICA kama CONGO DRC ZAIRE na Tanganyika n k ,zikakusanya dhahabu kwa wingi na kurundika kuhifadhi kama hazina ya duniani,kama akiba hazina ili itumike kama mbadala wa US PETROL DOLLAR ambapo hii US dollar itaanguka,na haitatumika tena kununulia petrol,utaanza mfumo mpya wa digital currency,na nchi tajiri zenye mafuta mengi zitaungana zitaanzisha pesa yao tofauti na US dollar na zitakataa kuuza mafuta kwa US DOLLAR..dhahabu itakuwa ni thamani ya pesa hata dola itakapo anguka siku za DHIKI KUU ambayo itaanza 2027 ama imeshaanza tuseme.
lakini hizi nchi tajiri pamoja na kukusanya FEDHA na DHAHABU nyingi bado hazitawasaidia katika KIPINDI CHA DHIKI KUU
Ezekieli 7:19
Watatupa fedha yao barabarani na dhahabu yao itakuwa kama kitu najisi. Fedha na dhahabu zao hazitaweza kuwaokoa katika siku hiyo ya ghadhabu ya Mwenyezi-Mungu; wala hawataweza kushiba au kuyajaza matumbo yao fedha na dhahabu waliyojirundikia; kwani mali hiyo ndiyo chanzo cha dhambi yao.
1 Pet 3:3-6
Kujipamba kwenu, kusiwe kujipamba kwa nje, yaani, kusuka nywele; na kujitia dhahabu
na wakati mwingine waliambiwa WAVUE VUOMBO VYA UZURI mapambo ikiwemo dhahabu.
Eze 16:17 S
Pia ulivitwaa vyombo vyako vya uzuri, vya dhahabu yangu na vya fedha yangu, nilivyokupa, ukajifanyia sanamu za wanaume, ukafanya mambo ya kikahaba pamoja nazo
kutoka 33
Ninyi ni watu wenye shingo ngumu; kama mimi nikiingia kati yenu dakika moja, nitawaangamiza; basi sasa vueni vyombo vyenu vya uzuri ili nipate kujua nitakalowatenda. Basi wana wa Israeli wakavua vyombo vyao vyote vya uzuri, tangu mlima wa Horebu na mbele.