Msidharau BIMA za watoto wapendwa, ni muhimu sana kwa watoto zetu

Msidharau BIMA za watoto wapendwa, ni muhimu sana kwa watoto zetu

SEASON 5

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2020
Posts
481
Reaction score
1,008
Sijui niseme nini kwa wale wazazi mlio na watoto wa chini ya 18yrs na hamjawakatia BIMA bei ya bima ya mtoto ni 50,400 tu kwa mwaka mzima,mtoto anatibiwa kwa BIMA ugonjwa wowote utakaokatiza mbele yake.

Kwann nasema hivi, nina mwanangu wa kiume umri wake wa kwenda mfanyia circumsission/kumtahiri (3yrs) ukawadia nikajisemea ngoja nimpeleke mwanangu akafanyiwe kitu nijue akishapona basi nimuanzishe shule akacheze cheze huko.

Basi nikafika hospital daktari akahtaji muona mtoto na kuona uume wa mtoto,akamshika kisha akawa ana mminya minya kwenye korodani,Nikashangaa sana daktari ananiambia "mbona mtoto ana korodani 1?"

nikatoa macho! akasema hatuwezi mtahiri mtoto akiwa na korodani 1 n lazima tuishushe maaana itakua imebaki tumboni haijashuka, na ikishndkana basi tuitoe kabisa maana kuicha ndani ni hatari sana kwa mtoto kwa huko mbeleni.

Basi tukaambiwa tulazwe,nikalazwa na mwanangu Mtoto akaja akafanyiwa operation korodani ikashushwa kisha akatahriwa...

Baada kama ya wiki nzima kuspend hospital,ukafka muda turuhusiwe sasa tukajiuguze nyumbani tuwe tunarudi clinic tu kwa ajili ya kuangaliwa maendeleo ya vidonda vya mtoto.

Nikapewa discharge form na maform mengine mengine,kwakua kote huko BIMA ilikua inafanya yake,mimi nilikua na deal na malipo ya MSOSI TU.

My dear form ya gharama ikaonyesha total charges zote ni 3,221,000 Tsh yaani Milioni 3 na laki mbili na ishirini na moja.

Hebu JAmani fikirieni kipindi hiki umpeleke mtoto hospital halafu uambiwe ili tatzo lake liondoke inahtajika mil.3 na upuuzi wake kama sio kutaftiana kuhara ni nini?

Jamani nimetokea kuheshimu BIMA aseee nawasisitiza BIMA jamani,unaweza kwenda hospital ukfkiri unaumwa JINO daktari anakucheki anakwambia MDOMO mzima meno ni ya kureplace hahaha inahtajika 7Mil otherwise mapengo yanakuja very soooon.

Kuna.magonjwa mengi sana wapendwa tusiyoyajua hii dunia,kama hii ya korodani kubaki tumboni ndio kwanzaaaaaaa limekua brand new maskioni mwangu.

Anyway Narudia tena kuwasisitiza BIMA jamani kwa mnaoweza msipuzeeee msipuuzeee.

Asikiae na Asikie.
 
Mkuu ahsante sana kwa kutukumbusha,binafsi ninaposafiri popote ni kheri nisahau kadi ya Benki kuliko cadi Yangu ya BIMA ,I like it most.

Kuna kipindi mwaka 2018 niliugua sana ugonjwa usio julikana,nilienda pale muhimbili wakanipima vipimo vyote hawa kuona ugonjwa ,hakika kwa siku moja, vipimo pamoja na kumuona daktari iligharimu almost 1M ,baada ya kukosa ugonjwa nilitumwa kitengo cha tiba ya moyo ,JKC hapo hapo muhimbili,napo walikuta hakuna tatizo gharama zote kwa siku zote tatu nilizokaa muhimbili nilikuta ni sh 3M.lakini kwa kuwa nilikuwa na BIMA hakika sikuona shida.

Nadhani swala la BIMA si tu kwa watoto Bali ni kwa watu wote,maana tofauti na BIMA ni watanzania wachache sana wenye kumudu gharama za matibabu kwa nchi yetu.
 
Sijui niseme nini kwa wale wazazi mlio na watoto wa chini ya 18yrs na hamjawakatia BIMA bei ya bima ya mtoto ni 54,000 tu kwa mwaka mzima,mtoto anatibiwa kwa BIMA ugonjwa wowote utakaokatiza mbele yake.
Bima wanashindwa kulipia ampicloxy tu wanasema haipo kwenye mpango wa bima hiyo ya kushusha korodani wataiweza?
 
Mkuu ahsante sana kwa kutukumbusha,binafsi ninaposafiri popote ni kheri nisahau kadi ya Benki kuliko cadi Yangu ya BIMA ,I like it most.

Kuna kipindi mwaka 2018 niliugua sana ugonjwa usio julikana,nilienda pale muhimbili wakanipima vipimo vyote hawa kuona ugonjwa ,hakika kwa siku moja, vipimo pamoja na kumuona daktari iligharimu almost 1M ,baada ya kukosa ugonjwa nilitumwa kitengo cha tiba ya moyo ,JKC hapo hapo muhimbili,napo walikuta hakuna tatizo gharama zote kwa siku zote tatu nilizokaa muhimbili nilikuta ni sh 3M.lakini kwa kuwa nilikuwa na BIMA hakika sikuona shida.

Nadhani swala la BIMA si tu kwa watoto Bali ni kwa watu wote,maana tofauti na BIMA ni watanzania wachache sana wenye kumudu gharama za matibabu kwa nchi yetu.

Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
Ni kweli mkuuu ila nilishauri kwa watoto kwasababu atleast bima ya mtoto inalipika kama mtu akiamua.

Bima za watu wazima ni gharama mkuu,lakini BIMA ni.muhimu sana sana kwa mtoto na.mtu mzima.

Japo kuna maumivu flani mtu unayapata ukifikiria Mwaka mzima unaisha unalipia kitu na hujaumwa hata kichwa,ni kweli inauma lakini magonjwa hayana siku wala muda Likija huko linakuja double double.

Na kwa jinsi watanzania tusivyo na utamaduni wa check up ya afya zetu,wengi tunapoenda hospital kwa lengo la kucheki ugonjwa Mmoja ni lazima Tukutwe na ugonjwa mwingine na mara nyingi ugonjwa unaogundulikaga hospital unakuaga hatari kuliko huu uliotupeleka hospital.

BIMA wapendwa ni muhimu,Magari yapo tu ndugu zanguni tutayaendesha sana tu.
 
Back
Top Bottom